Ukoloni Mamboleo na namna viongozi wa Afrika walivyonaswa

Hashimu lwenje

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
415
359
Ukoloni ni nini?

Ukoloni ni mfumo wa taifa moja kuvuka mipaka yake na kutawala maeneo ya mbali yanayokaliwa na watu wengine kwa nyanja za uchumi , utamaduni na jamii. Maeneo hayo yanaweza kuitwa ma koloni ya kawaida au maeneo lindwa tu.

Utawala wa kikoloni
Utawala wa kikoloni ni utawala ulioanzishwa
hasa na Wazungu kwa lengo la kunyonya na pengine kuwabagua Waafrika na watu wengine wenyeji wa Asia , Oseania na Amerika. Utawala huo ulitegemea hali ya taifa husika pamoja na hali ya jamii zilizokuwa
zinatawaliwa.

Baada ya kuanzisha utawala huo wakoloni walibadilisha utawala wa jadi na kuufanya utawale kwa masilahi ya wakoloni; pia utawala huo uliharibu hadhi ya utawala wa jadi na misingi ya jadi.

Muundo wa utumishi katika utawala wa kikoloni yaani wazungu

(a) Kazi katika ngazi za juu zilifanywa na Wazungu, hasa kazi zilizohitaji ujuzi .

(b) Kazi katika ngazi za chini zilifanywa na wenyeji kama vile ukarani , utarishi, ufagizi na ukorokoroni .

(c) Wakoloni walitoa elimu duni kwa wenyeji ili waendelee kuwaajiri katika ngazi za chini.

Ikumbukwe kwamba tangu karne ya 15 hadi karne ya 19 bara la Afrika lilikuwa sehemu muhimu pengine
kuliko sehemu yoyote duniani kwa sababu ndilo lilikuwa mzalishaji mkuu wa malighafi kwa ajili ya mataifa ya Ulaya.

Mwaka 1884-1885 ulifanyika mkutano wa mataifa ya Ulaya nchini Ujerumani kuhusu namna ya kuligawana bara
Afrika. Mkutano huo ulisimamiwa na aliyekuwa Kansela wa Ujerumani kwa
wakati huo, Otto Bismark na kufikia makubaliano ya kila nchi inayoweza kutawala sehemu yoyote ya Afrika na rasilimali zake, ichukue.

Ukoloni Mamboleo ni neno linalotumiwa na wakosoaji wa ukoloni kuelekezwa kwa nchi tajiri kuendelea kuingilia masuala ya nchi
zinazoendelea baada ya ukoloni wenyewe kwisha kwa ukiukaji wa azimio la Umoja wa Mataifa . Wanakosoa mataifa ya kibepari kuhusika na dhuluma katika biashara ya kisasa na yaliyokuwa makoloni.

Wakosoaji wanasisitiza kwamba wafanyabiashara binafsi na makampuni ya
biashara ya kigeni huendelea kunyonya rasilimali za mataifa baada ya enzi ya ukoloni kama ilivyotekelezwa kutoka karne ya 16 hadi karne ya 20. Ikumbukwe kwamba tangu karne ya 15 hadi karne ya 19 bara la Afrika lilikuwa sehemu muhimu pengine kuliko sehemu yoyote duniani kwa sababu ndilo lilikuwa mzalishaji mkuu wa malighafi kwa ajili ya mataifa ya Ulaya.

Historia inatuambia kwamba mataifa ya Denmark, Ufaransa, Urusi, Ureno, Italia, Hispania, Uturuki, Uholanzi yaligawiwa maeneo huku Ubelgiji na Marekani
wakiwa kama wageni waalikwa.

Kweli mkutano huo ulileta mafanikio katika kile walichokidhamiria ikiwa ni
pamoja na kuepusha migongano kati yao, kwani kila taifa lilikuwa na uchu wa, rasilimali za bara hili.

Masuala yaliyoafikiwa katika mkutano huo yalikuwa ni kukomesha biashara ya utumwa, kueneza kile walichokiita ustaarabu na dini na kukomesha vita vya
wenyewe vya wenyewe vilivyopiganwa na
makabila na koo mbalimbali zilizokuwapo wakati huo. Hata hivyo, masuala haya hayakuwa mambo ya msingi sana kwao.

Hapo awali niligusia kwamba Afrika ilikuwa sehemu muhimu sana duniani kwa kuwa ilikuwa mahala pekee ambapo wangeweza kupata malighafi kwa ajili ya
viwanda huko Ulaya na Marekani. Kila nchi wakati huo ilitamani kumiliki ardhi
ya Afrika yenye rutuba, madini na kila nchi ilitamani iwatumie Waafrika kama
nguvukazi katika mashamba yao. Kupitia mtifuano huo ndipo Bismarck akawaita
wenzake mjini Berlin. Hapa ndipo historia inapotuambia kwamba Afrika ikakatwa vipandevipande, wakaingia
kama mtu aliyeingia kwenye shamba ambalo alipanda yeye na kuvuma mazao yake. Wakakubaliana kwamba kila nchi miongoni mwao inaweza kuchukua koloni lolote kwa sharti tu la kuweza kutawala, hakuna taifa la Ulaya ambalo lingezuiwa kwa namna yoyote kufanya biashara
katika bara la Afrika, hapakutakiwa kuwa na ongezeko la kodi kwa bidhaa yoyote kutoka au kuingia Afrika.

Vitabu vinaniambia madini yote na misitu minene ya mbao na magogo ya Kongo akapewa Mfalme Leopold II wa Ubelgiji, Uingereza ikachukua shaba ya Zambia,
mafuta na ardhi yenye rutuba ya Nile huko Misri, Kenya, Sudan na dhahabu ya Kimberley, Afrika Kusini, Ghana na almasi ya Zimbabwe. Ufaransa ikapewa kila kitu kilichopatikana Jamhuri ya Afrika ya kati, Mauritania mpaka Gabon na Chad. Ureno akaambiwa ajichukulie Msumbiji na Angola. Italia ilichukua
Somalia na sehemu za Ethiopia. Bahari, madini, mbuga za wanyama na ardhi nzuri ya Tanzania bara (Tanganyika kwa wakati huo) na Namibia alijichukulia Mjerumani.

Katika hayo yote Mwafrika hakuhusishwa, alikuwa hana hili wala lile mpaka alipokuja kujua kwamba yeye anapaswa kulima na kuchimba madini yake mwenyewe kisha awape hawa watu wapeleke kwao kisha watulete sigara,
vioo, mafuta na nguo watuuzie, inauma sana.

Kwanini nimeanzia huko?

Huku ikiwa imepita miaka zaidi ya 50 tangu mataifa haya yaiache Afrika kwa
kila kinachoitwa uhuru, mataifa haya yanaonekana kurudi tena kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. Wakuu wa mataifa yaleyale yalikaa mwaka 1884-1885
yameanza kupishana kwa kasi ya ajabu katika anga la bara la Afrika. Wanakuja
kwa njia ya makubaliano na mikataba ya kiuwekezaji.

Tujiulize, kwa nini?

Katika makosa ambayo Afrika haipaswi kuyarudia ni kuacha mataifa haya
yajichagulie cha kuchukua. Kwa sasa mataifa haya yanajua Afrika ina wasomi,
wanaelewa wazi kwamba sasa hivi Afrika ina watu wenye uwezo wa kuchakata mambo, hivyo wanapaswa kutulia na kuja na mikakati inayoonekana kama pipi
kumbe ndani shubiri.

Kwa sasa mataifa haya hayawezi kutumia mbinu waliyoitumia mwaka 1884-1885 au nyingine walizozitumia huko nyuma. Ni wakati wa kuwa makini.

Tusizubaishwe na mikopo yao ambayo huja kama neema kwa Afrika. Fikiri
kuhusu Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia na mashirika mengine namna yanavyoinyemelea Afrika baada ya kushindwa kurejesha madeni. Suala la mikopo halijaanza leo, suala la mahusiano ya kibiashara hayajaanza leo, yalikuwepo tangu miaka ya 1,700 walipotudanganya kwa vioo, sigara, bunduki na nguo, kisha wakachukua rasilimali ambazo mpaka leo hazijulikani thamani yake kwa sababu nyingine
hazipimiki.

Kwa sasa Afrika ina viongozi na wataalamu wenye ufahamu wa kutosha kabisa kugundua mitego na hila iliyoko katika mikataba yao. Kumbuka haya mataifa yanataka Afrika iendelee kuyategemea ili yenyewe yaendelee kunawiri, kwa hiyo yale yote
yanayosemwa kwamba yanatoka kwao kutusaidia yachunguzwe mara nyingi
iwezekanavyo. Kuna haja ya kuwa makini sana na hawa watu.

Hebu tuwatumie wataalamu tulionao hata kama ni wa kiwango kidogo lakini kwa manufaa yetu. Mataifa ya Kiafrika yanapaswa kuwaamini wasomi wake wa masuala mbalimbali kwa sababu hata wataalamu tunaowaamini kutoka mataifa ya nje ya Afrika walianza kama sisi tu,
hawakuzaliwa wanaweza, walijifunza.

Afrika kwa sasa ina wataalamu karibu kila idara, watumike watatusaidia. Sisemi kwamba tusishirikiane wala kuwatumia wataalamu kutoka nje, tushirikiane nao
huku tukiwekeza nguvu kubwa kwa hawa wetu, tufanye hivyo, lakini kwa umakini mkubwa kuliko umakini ambao tumewahi
kuwa nao siku za nyuma.

Afrika isitegemee misaada

Hivi inakuaje bara kama Afrika lenye kila kitu tena kwa kiwango cha kutisha bado.linaishi kwa kutegemea misaada? Ni ajabu lakini ni kweli kwamba Afrika
inategemea misaada kutoka kwa watu ambao wanatutegemea sisi kupata wanachotuletea.

Ifike mahala tutambue na tuamini kuwa haya mataifa hayawezi kufanya chochote bila Afrika, yaani tuume meno na tukamate breki hata kama tutaumia lakini baadaye watatuheshimu.

Kuishi kwa kutegemea misaada kwa watu ambao wanatutegemea sisi kupata wanachotuletea ni kichekesho kinachoweza kumfanya mtu acheke karne nyingi, niamini mimi kwamba hata wao wanatung’ong’a. Tusiwe waoga, kuna baadhi ya mambo ambayo tunaambiwa tuyatekeleze ndipo tusaidiwe, lakini
ukiangalia nyuma yake kuna madhara makubwa. Hata hivyo, baadhi ya viongozi wa Afrika hukubali tu kusaini ili tupate misaada, lakini baadaye tunaingia kwenye mtego unaotulazimu kufia ndani.

Mfano, mataifa mengi yamekuwa yalikubali kuingia kwenye madeni ambayo yanakuwa matamu kwa nje, yaani kikitajwa kiasi cha hilo deni wanafikiri watanufaika lakini baadaye tunashindwa
kulipa.

Kutokana na hili unakuta uzalishaji unapungua, uzalishaji ukipungua maana yake tunajikuta tukitegemea bidhaa za vyakula kutoka nje. Sio hivyo tu, hata vile
viwanda vilivyopo katika nchi za Afrika vinakufa kwa sababu bidhaa zake
hazinunuliwi kwa sababu ya Waafrika hususani Watanzania kutokuviamini vya kwetu. Tujifunze kutumia vya nyumbani, licha ya kuamini kuwa vya nje vina ubora, vipo vingi pia vina ubora.

Serikali za kiafrika ziimarishe mifumo ya elimu. Kila kitu kinachofanyika kwa ufanisi katika ulimwengu huu
kinategemea elimu. Ikiwa bidhaa zitakosa ubora, majengo yatakosa uimara, barabara hazitadumu, utawala utayumba, sekta za kilimo zitayumba, sekta ya fedha itayumba, sekta ya afya itayumba usiende
mbali, chunguza elimu inayotolewa Afrika.

Elimu ikiwa mbovu hatuwezi kupata wataalamu wazuri wa masuala mbalimbali jambo ambalo litatufanya tuendelee kutegemea wataalamu wa afya, uchumi, wahandisi, wataalamu wa viwanda na
madini ambao wakija wanaambatana na masharti kutoka nchi husika.

Elimu ikiwa mbovu mikataba mibovu hatuwezi kuikwepa, tutasaini tu kwa sababu hatuelewi. Zamani walituchukua, safari hii tusijipeleke wenyewe.
 
pale mkoloni mweusi anapojaribu kuwadanganya watu wake kuwa "wazungu" ndio maadau! adui wa maendeleo ya africa ni madikteta wa kiafrica.
 
pale mkoloni mweusi anapojaribu kuwadanganya watu wake kuwa "wazungu" ndio maadau! adui wa maendeleo ya africa ni madikteta wa kiafrica.
Masuala yaliyoafikiwa katika mkutano huo
yalikuwa ni kukomesha biashara ya utumwa,
kueneza kile walichokiita ustaarabu na dini na
kukomesha vita vya
wenyewe vya wenyewe vilivyopiganwa na
makabila na koo mbalimbali zilizokuwapo wakati
huo. Hata hivyo, masuala haya hayakuwa mambo
ya msingi sana kwao.
 
Mzungu amewashika koni
Masuala yaliyoafikiwa katika mkutano huo
yalikuwa ni kukomesha biashara ya utumwa,
kueneza kile walichokiita ustaarabu na dini na
kukomesha vita vya
wenyewe vya wenyewe vilivyopiganwa na
makabila na koo mbalimbali zilizokuwapo wakati
huo. Hata hivyo, masuala haya hayakuwa mambo
ya msingi sana kwao.
 
Ccm wakishabanwa na watoa misaada wao huko huwa mnakuja na theories nyiiingi mara mkutano wa berlin mara sijui ukoloni utadhani hayo ndiyo yanasababisha tuwe masikini hadi leo. Umasikini wa Tanzania unasababishwa na ccm na siyo ukoloni wala mkutano wa berlin
 
Acha sisi wasomi tuwaeleweshe jinsi mambo yalivyo, maana nyie michidima mmezoea kudandia mambo bila kureason na 2020 mtakua mmechuja sana
Kadri chadema na upinzani unavyochuja na kudumazwa na udhalimu wa serikali yenu ndivyo na ccm wanavyozidi kufilisi nchi na kuiacha masikini kuliko jana
 
Hivi chadema wavuta bangi wanaweza kuongoza nchi kweli, kijiji changu mpaka leo kinajuta kwa kuchagua chama chenu hicho, yule mwenyekiti kazi kuuza viwanja tu na mapori ya serikali
Nyie mna nn cha kujivunia kuwa mnaweza kiendesha nchi kama zaidi ya miaka 50 bajeti inafadhiliwa na mabeberu?
 
Kadri chadema na upinzani unavyochuja na kudumazwa na udhalimu wa serikali yenu ndivyo na ccm wanavyozidi kufilisi nchi na kuiacha masikini kuliko jana
Sio kweli, Rais wetu anafanya kazi nzuri sana, ulizoea vya bwelele, leo umetaitiwa kooni, unapumulia mashine, umeishiwa ajenda, umebaki kufuata ajenda za wazungu.
 
Sio kweli, Rais wetu anafanya kazi nzuri sana, ulizoea vya bwelele, leo umetaitiwa kooni, unapumulia mashine, umeishiwa ajenda, umebaki kufuata ajenda za wazungu.
Kazi ipi nzuri anayoifanya zaidi ya kufilisi nchi na kuonea raia?
 
Nyie mna nn cha kujivunia kuwa mnaweza kiendesha nchi kama zaidi ya miaka 50 bajeti inafadhiliwa na mabeberu?
Sisi tunajivumia Rais mwenye upeo asiyependa kuuza nchi yetu, Rais mwenye maono, Rais anayejua kutafuta pesa kwa kutumia Rasilimali za nchi, kwa kusanya kodi, mngekua ni ninyi mngeuza makampuni yetu, na Rasilimali zetu, ili mpate hela za kuendeshea nchi
 
Sisi tunajivumia Rais mwenye upeo asiyependa kuuza nchi yetu, Rais mwenye maono, Rais anayejua kutafuta pesa kwa kutumia Rasilimali za nchi, kwa kusanya kodi, mngekua ni ninyi mngeuza makampuni yetu, na Rasilimali zetu, ili mpate hela za kuendeshea nchi
Acha utani ww. Waliouza/wanaouza mali za umma na rasilimali zetu huwajui au unajitoa ufahamu tu? Hivi unahabari viwanfa vya korosho mliuza kwa mil 75 tu kwa wahindi halafu leo mnabwabwaja korosho hazibanguliwi! Acha kujitoa ufahamu ewe mwana lumumba
 
Back
Top Bottom