Salaam wakuu,
Hii ndoa ina miaka 7,watoto 3.
Tatizo la kibinadamu-kama walivyo baadhi ya binadamu wengine,bwana akapata mpenzi,akazaa nae.
Akawa akijitahidi kutimiza mapenzi sehemu zote 2 na matumizi nyumbani, lakini baada ya kujulikana siri , mke wa ndoa akazua vita kali na akaamua kuingia kanisa la wokovu.
Mapenzi yakaporomoka kwa mke wa ndoa.Mama wa ndoa muda mwingi akaanza kuuweka kwenye hilo kanisa na uhusiano na familia ya mme na yake umepungua zaidi ya asilimia 70.
Mme halali nje ya nyumba yake. Lakini mapenzi anafanya kote.Wake wote wana pesa za kujitosha.
Shida ni moja tu,mama wa ndoa hana muda wa kushughulikia watoto, wala nyumba yake na wala hataki hawa watoto wake wajuane na mtoto wa bi mdogo.
Katika kukosa amani katika nyumba yao,mama wa ndoa akaanza kutembea na ndugu wa karibu na mume na siku walipokuwa na tafrani akamwambia mumewe kuwa ana revenge.
kwa sababu hii nauliza kiukweli tu,kama mume anahitaji kuishi humu duniani afanyeje mkewe wa ndoa akitaka penzi?atembee nae kwa condom au wakapime kila mara akimtaka au amuache-divorce au separation maana yeye anajijua kuwa ana makosa na anakubali, lakini adhabu yake isiwe kuikubali revenge na ategemee kifo cha ukimwi.?
Asante.
Kwa kuwa zinaa imeingia,na maelewano hakuna,bora watengane.. Waende kwenye vyombo husika,watengane...

Unaona mkewe ataleta gonjwa je hiyo nyumba ndogo. Huyo bwana ana makosa Kosa limetokea akae na mkewe wasuluishe
Wanawake ni watu wa msamaha... sijuhi mwanamke mjinga uvunja ndoa yake mwenyewe na bla bla bla kibao za kumnyanyasa mwanamke kijinsia.
Twende kwenye mada; wewe una makosa mengi tu na wala mkeo hakuwa na sababu yeyote ya kukusamehe. Kwanza umetembea nje ya ndoa na kithibitisho ni mtoto ulozaa. Sawa ningekuwa mkeo labda nasema tena labda ningekusamehe baada ya miaka kadhaa ya kuishi na hasira kichwani mwangu kila nikikumbuka kuwa umezini na una mtoto nje ya ndoa.
Ila kwa nini basi hustahili msamaha; kwa kuwa uhitaji kusamehewa kwani wewe si kuwa unajuatia kosa lako bali huoni kama umekosea. Kwa nini nasema hivyo; kwa sababu mwenyewe umekiri hapa kuwa unaendelea kuzini na huyo hawara yako. Masamaha wanapewa wale wanaotubu na kukusudia kuacha wewe huna kusudi la kuacha. Na soon utaongeza mtoto mwingine nje ya ndoa yako. Wewe unadhani huyo kimada hana akili, nia yake ni kukuteka jumla na maugomvi ya ndoa yako kwake ni sherehe.
Naona umekuja kutafuta jibu la kuku suport na uzinzi unaoendelea kuutenda. Kumbuka msahara wa dhambi ni mauti.
Najaribu kufikiri; hivi wababa wanaozaa nje ya ndoa wana nafasi gani katika malezi ya watoto wao?... Kwa maneno mengine unaweza kuwakanya watoto wako waache kuwa mcharuko wakati wewe una watoto nje ya ndoa?
Tena asivyokua na haya............eti mkewe ndie atakaye mletea magonjwa.............Ahhh some pipo wanachefua kweli:smash::smash::smash::smash::smash:
Afu anasema mkewe hataki watoto wao wamjue mtoto wa nje. Si ajiulize ni kwa nini mkewe hataki. Anaona aibu ataanzia wapi kuwaambia watoto kuwa baba yenu ni mzinzi na hili ndo tunda la uzinzi wake. Au wewe mleta mada huoni aibu kuwambia watoto huyu mwanangu wa "nje"? Well unless hao watoto wako ni wadogo sana; kama ni wakubwa wataungana na mama yao kukuchukia.
Saa ingine mtu hata unashindwa kunashangaa kwani anatumia nini kuwaza???
Anasali kanisa la wokovu halafu tena kaamua kurevenge kwa kutembea na ndugu wa mumewe! Hii kali wokovu utatoka wapi hapo.
Ila mumu ana makosa kama kweli anataka amani ndani ya ndoa yake arudi amuombee mkewe msamaha wa kweli then wakapime afya zao maisha yaendelee na aachane na nyumba ndogo.
Kama vipi, wanaona mambo ni magumu basi watengane