Uko kundi lipi kati ya haya?

Tutor B

JF-Expert Member
Jun 11, 2011
9,025
6,582
Imanuel - Mungu pamoja nasi ..

Kundi la kwanza ...
Ni wale wanaowazia mambo ya kila mwaka .... hawa wanapenda kupanda mbegu za mda mfupi na kuvuna kwa mwaka huo. Kazi yao ni kupanda na kuvuna.

Kundi la pili ...
Hawa ni wale wenye mawazo ya kuanzia miaka miwili / mitatu hadi kumi ... Kazi yao kubwa ni kupanda miti na kuvuna baada miti hiyo kukomaa. Wanapanda miti na kuvuna natunda ya miti.

Kundi la tatu ...
Hawa ni wale wenye kuwaza zaidi ya miaka kumi ijayo hadi miaka mia moja na kuendelea ... hawa kazi yao kubwa ni kufundisha wengine ili na wengine wafundishe wengine ... zoezi la kufundishana ni endelevu.

Jichunguze wewe uko kundi gani?
 
Na sisi wenye mawazo ya siku moja- tunaobeti leo kesho tunachana mikeka.
Tunakaa kundi gani?
 
Enzi zangu (ujana) sikuwahi kuwazia mambo ya bahati nasibu! Hivyo nisamehe kuhusu akina ku-bet ... binafsi nawashangaa sana!

Ila naona ni kama kukosa mwelekeo ukajaribu lolote.
 
Kubet ni mfano tu! wazo kubwa hapo ni mawazo ya muda mfupi chini ya mwaka (kama ulinielewa vema)
kwani wote wenye mawazo ya mwaka mmoja ulimaanisha ni wakulima? mi nikuelewa kama ulikuwa ni mfano tu!

BTW, unaonesha utafiti wako huu ni wa muda mrefu sana, inabidi uu-Update aisee..!
maana wapo hadi watu wenye mawazo ya lisaa limoja tu! hujawahusisha kabisa.
 
Kuanzia sekunde, dakika, siku, wiki, mwezi, mwaka, miaka kumi vyote vimejumuishwa! Miaka 100 haipatikani pasipo sekunde moja / siku / .......

Tunapokuwa tunafanya grading .. let say C = 50 - 64%, B = 65 - 79%, A = 80 - 100% ... kunakuwepo na wenye 0 - 49% ambao kwenye grading yangu mimi siwahitaji kabisa ... hao huwa wanaambiwa ahsante kwa kushiriki.
 
Kuna watu tunaishi kwa siku
Hakuna anayeishi kwa miaka mia mkuu! wote ni mmoja -- miwili ... kumi .... ishirini ... na kuendelea. Ila kifikra, kama fikra zako ni za siku moja ... mwingine ni za wiki, mwingine za mwezi ... mi naanzia mwaka
 
Imanuel - Mungu pamoja nasi ..

Kundi la kwanza ...
Ni wale wanaowazia mambo ya kila mwaka .... hawa wanapenda kupanda mbegu za mda mfupi na kuvuna kwa mwaka huo. Kazi yao ni kupanda na kuvuna.

Kundi la pili ...
Hawa ni wale wenye mawazo ya kuanzia miaka miwili / mitatu hadi kumi ... Kazi yao kubwa ni kupanda miti na kuvuna baada miti hiyo kukomaa. Wanapanda miti na kuvuna natunda ya miti.

Kundi la tatu ...
Hawa ni wale wenye kuwaza zaidi ya miaka kumi ijayo hadi miaka mia moja na kuendelea ... hawa kazi yao kubwa ni kufundisha wengine ili na wengine wafundishe wengine ... zoezi la kufundishana ni endelevu.

Jichunguze wewe uko kundi gani?
Mazingira uliyoko ndiyo yatakuchagulia uwe kundi gani! Mfano,huu mwaka familia yangu haina chakula,je nitakuwa na mawazo ya miaka kumi mbele? La hasha. Mfano mwingine ,nikiwa raisi leo,nitawaza mipango ya mwaka mmoja tu! La hasha. Kwa hiyo,mwaka huu naweza kuwa kundi hili,mwakani nikapanda daraja,nikawa kundi lingine au nikashuka daraja.
 
Mwenye kuwa kwenye kundi la tatu, ina maana anaishi maisha ya kawaida ila anatumia kila liwezekanalo kuhakikisha fikra zake hazifi japo yeye anaweza kufa hata dakika mbili mbele. Ndiyo maana anafundisha wengine...
Wenye kuwaza miaka kumi ... unawajua?
Wa mwaka mmoja tu je?
 
Imanuel - Mungu pamoja nasi ..

Kundi la kwanza ...
Ni wale wanaowazia mambo ya kila mwaka .... hawa wanapenda kupanda mbegu za mda mfupi na kuvuna kwa mwaka huo. Kazi yao ni kupanda na kuvuna.

Kundi la pili ...
Hawa ni wale wenye mawazo ya kuanzia miaka miwili / mitatu hadi kumi ... Kazi yao kubwa ni kupanda miti na kuvuna baada miti hiyo kukomaa. Wanapanda miti na kuvuna natunda ya miti.

Kundi la tatu ...
Hawa ni wale wenye kuwaza zaidi ya miaka kumi ijayo hadi miaka mia moja na kuendelea ... hawa kazi yao kubwa ni kufundisha wengine ili na wengine wafundishe wengine ... zoezi la kufundishana ni endelevu.

Jichunguze wewe uko kundi gani?
Past and future only exist now!
 
Mwenye kuwa kwenye kundi la tatu, ina maana anaishi maisha ya kawaida ila anatumia kila liwezekanalo kuhakikisha fikra zake hazifi japo yeye anaweza kufa hata dakika mbili mbele. Ndiyo maana anafundisha wengine...
Wenye kuwaza miaka kumi ... unawajua?
Wa mwaka mmoja tu je?
Ahh,nimekupata,kumbe ni kuwaza tuu!
 
Bila kuwaza huwezi kutenda,
Elewa vizuri,saikolojia na sosholojia kwa mtu ni dynamic,havigandi. Mtu huwaza,ni sawa. Kutenda hutegemea mazingira. Kwa mantiki ya thread yako siamini kuwa akiwaza,akapanda na kuvuna mwaka huu,mwakani hawezi kuwaza na kutenda vitu vya miaka 10 au 1000 mbele. Mtu huyu unamweka kundi gani hapo? Asante.
 
Biblia inasema "...aonavyo mtu nafsini mwake ndivyo alivyo" thread hii inauliza hivi .. wewe uko kundi gani?
 
Back
Top Bottom