Ukizubaa tu, imekula kwako!!!!!!!!!!

Nakumbuka enzi hizi Kama kuna nyama nzuri katikati ya sinia basi unakuka kwa style ya njia kuielekea hiyo nyama bila wenzio kushtukia hadi inaangukia upande wako! Hahahaaa!
 
Inakula vipi kwako wakati.ni maharagwe? Kungekuwa na finyango hapo sawia, lol

Ukienda taratibu utatoka empty, chote ulichokula kinakuwa kimechamba koo tu.
 
Nakumbuka enzi hizi Kama kuna nyama nzuri katikati ya sinia basi unakuka kwa style ya njia kuielekea hiyo nyama bila wenzio kushtukia hadi inaangukia upande wako! Hahahaaa!

Enzi hizi nyama ndo kinakuwa kitu cha kwanza kushambuliwa, halafu mambo mengine baadae.
 
Duh! umenikumbusha ubwabwa wa shughulini...njemba nyingine udenda unawachuruzika kwa uchu wa msosi, basi unasepa zako taratibu.
rafiki wewe kijijini unakusikia kwa jirani?
ukikulia kijijini halafu familia imejaliwa watoto wengi huo ndo mwendo wa kila siku. hapo ni milo miwili tu kwa siku halafu mtindo wa kugombania. yaani hapo lazima utajifunza kula.
nakumbuka watoto wa dadangu walikuwa wanasumbua sana kula akawapelea kwa wakwe zake wiki moja tu walirudi wanakula kama hawana akili nzuri. hii technic inafaa sana kwa watoto wanaosumbua kula
 
Imenikumbusha mbali kweli......Siku moja umetengwa ubwabwa wa maharage, mwenzetu mmoja akawa anasinzia, kustuka akakanyaga ubwabwa (tulikuwa tunauzunguka tukiwa tumekaa kwenye vigoda). Basi bibi alichofanya ni kukusanya ule uliokanyagwa akamwaga, tukaendelea kuula.....
 
Hii ilikuwa nzuri sana, kwanza inafundisha kushare pili inawafanya watoto wawe sharp !
 
hawa wamependelewa mbona mboga ni nyingi namna hiyo?
 
Hapo kama kuna nyama unaidaka fasta unaiweka benchi mkono wa kushoto afu unaendelea na ligi, yenyewe utaila mwisho
aisee wewe ni mzoefu haswa umetisha mkuu,maana ukijifanya unapiga nyama na msosi pamoja unakuta sinia inatabasam tupuu
 
Nakumbuka enzi hizi Kama kuna nyama nzuri katikati ya sinia basi unakuka kwa style ya njia kuielekea hiyo nyama bila wenzio kushtukia hadi inaangukia upande wako! Hahahaaa!
kama chui unanyatia watu wanaangusha maujuzi tu
 
Ugali kwenye sinia? Tena wa vipande?
Nimeamini 'Maguzu masese'
 
Ugali kwenye sinia? Tena wa vipande?
Nimeamini 'Maguzu masese'

Ugali ulikua unamoto sana hivyo ikabidi wakatiwe matonge ili iwe rahisi mtu kucheza rafu.
 
Hata mijini hii ni kawaida kwa wana familia lakini shughulini nomaaa, maana wengine udenda unaishia kwenye sinia basi appetite yote inapotea inabidi usepe tu!!!!

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…