Wengi huwa tunaenda sehemu na kufikia kwa ndugu, jamaa na marafiki. Haya ni mambo hayafai kufanya ugenini.
1. Usishangaeshangae sana vitu vya mwenyeji wako kama dalali anayethaminisha mali.
2. Jitahidi kuwa msafi muda wote, hakuna mtu anapenda mgeni mchafu.
3. Usichelewe kurudi na ikitokea basi toa taarifa. pia ukiondoka aga.
4. Usikatae chakula kwa mwenyeji wako hasa cha usiku.
5. Usisifu sana watu wengine kana kwamba wenyeji wako hawana maana. mfano umepikiwa wali unaanza kusema "mke wa John akikupikia wali! utajing'ata kidole".
6. Usiwe mbishi, muongeaji na kujidai unajua sana ugenini.
7. Kama kuna kazi au kitu unaona unaweza kununua fanya hivyo.
8.......................
Source: Kitabu haifai cha Abdu Baka