Ukiwa tajiri haimaanishi utakuwa na furaha muda wote

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
16,515
28,487
xgettyimages-519517489.jpg.pagespeed.ic.F60PsVfFd-.jpg


Pengine ule msemo kuwa pesa haiwezi kununua furaha una ukweli zaidi ya hata unavyofikiri.

Hii ni kwasababu kuna tafiti nyingi zinazohitimisha kuwa utajiri na furaha si vitu vinavyoendana kama inavyotegemewa. Sababu moja kwa mfano, ni kwamba watu matajiri huonekana kuwa watu wasio na moyo wa ukarimu zaidi. Utafiti mmoja ulibaini baada ya washiriki kupewa $10 na kuambiwa kuwa wanaweza kuitoa sehemu au yote kwa mtu mwingine, wale matajiri walitoa chini kwa asilimia 44.

Kwenye ulimwengu halisi, watafiti wamebaini kuwa watu matajiri hutoa kiasi kidogo ukilinganisha na walichonazo kwa misaada. Matajiri pia ni watu wa kujitenga zaidi na watu wa kawaida – kitu ambacho kina madhara kwenye furaha.
Kingine kadri watu watu wanavyokuwa na fedha hupenda uhuru zaidi na kupunguza kujichanganya na watu wengine.

Matokeo kutoka kwenye utafiti wa Notre Dame ni kuwa dalili za ukaribu kama vile kugawa fedha, kujitolea na kuwepo kwa ajili ya marafiki zilihusishwa zaidi na furaha. Pia ukarimu ulikuwa na madhara chanya kwa asilimia 93 katika nchini 136.

Hiyo ni kwasababu binadamu huonekana kuwa na furaha zaidi pale tunapojichanganya. Tafiti zinaonesha kuwa hatuwezi kuwa na furaha bila kuwa na walau uhusiano wa karibu wa maana. Kadri tunavyofurahia maisha ya kujichanganya, ndivyo ambavyo tunapata hisia chanya.

Kama umebahatika kuwa tajiri, elewa madhara yaliyothibitishwa kisayansi ya kujitenga.
 
I can't agree more with you mkuu. Ni ukweli kabisa. Japo hela/mali ni muhimu sana katika maisha as a resource lakini hazimpi mtu hakikisho la moja kwa moja la furaha.
 
Kuwa masikini ni matokeo ya kushindwa kutafuta hela hii ndio huzuni namba moja
 
Mara nyingi ktk familia tajiri, amani au furaha ni vitu vinavyotokea kwa nadra na kupotea haraka hasa upande wa uaminifu ktk ndoa, mama hunyanyasika sana hapa maana bos huwa anatumia pesa kupata msichana ampendae na akiwa na mkewe huwa ni kutimiza wajibu tu kama kupiga mswaki asubuhi.
 
Hii mada inafurahisha sana kwa jinsi inavyoongelewa sana kwamba rich people are not happy but the funny thing is everybody wants to be rich sijui ili athibitishe kama ayo maneno yana ukweli au la?

Kwa jinsi navyojua mimi being happy is an emotion which can be triggered by different actions/ circumstances.

Kwa dunia ya sasa ambayo pesa ina nafasi kubwa kwenye maisha ya binadamu nadhani ukiwa nayo you will be more happier, healthier and have a better sex life compared to when you are broke.

Sizani kama nitakuwa nimekosea nikisema watu wengi waliofanikiwa wanakuwa na marafiki wachache coz they choose their friends carefully na kama unavyojua it is lonely at the top, unavyozidi kwenda juu ndio pyramid inavyozidi kuwa ndogo. Sioni sababu ya kuwa na marafiki wengi ambao hawana mchango positive kwenye maisha yako.
 
Usipende kukumbatia umaskini by believing in such myths, siamini kama Mungu amekuleta duniani uteseke maisha yako yote.

It so sad so many people go through life without realizing their full potential.

Unajua pesa ni sababu kubwa ya mahusiano mengi kuvunjika, chunguza watu wengi wanaoachwa au kugongewa mademu zao utagundua mara nyingi huko ambako mchumba anaenda, the guy is doin better than you in life, may be it is just a coincidence(LMAO)
Mara nyingi ktk familia tajiri, amani au furaha ni vitu vinavyotokea kwa nadra na kupotea haraka hasa upande wa uaminifu ktk ndoa, mama hunyanyasika sana hapa maana bos huwa anatumia pesa kupata msichana ampendae na akiwa na mkewe huwa ni kutimiza wajibu tu kama kupiga mswaki asubuhi.
 
Usipende kukumbatia umaskini by believing in such myths, siamini kama Mungu amekuleta duniani uteseke maisha yako yote.

It so sad so many people go through life without realizing their full potential.

Unajua pesa ni sababu kubwa ya mahusiano mengi kuvunjika, chunguza watu wengi wanaoachwa au kugongewa mademu zao utagundua mara nyingi huko ambako mchumba anaenda, the guy is doin better than you in life, may be it is just a coincidence(LMAO)
Mkuu wewe umeongea ukweli zaidi ya ukweli,hao wanaosema mwenye pesa hana furaha wamechemsha au vipi? labda mwenye pesa mgonjwa wa asiopona,eti tuwe masikini ili tupate furaha?,huu ni uchizi sasa.
 
Kila mtu ana upande wake ila wengi mnatamani utajiri ila kwa upande wangu ntapenda utajiri ambao hautakuwa na shari na mimi,kwann nasema hivyo taeleza kwa ufupi matajiri wengi wanateseka sababu ya ubinafsi au njia waliopatia hizo pesa zao!.me miaka ya 2000 nilipata mil700 baada kuuza tanzanite wale marafiki toka udogoni pmj na ndugu niliwavuta karibu zaidi niliwasaidia sana kila siku niliwapa mitaji ila hakuna alienishauri me nifanyie nini hizo pesa!sikuwa na mkono wa birika yaani walinigeuza vikoba sijui saccos na wala sikuwachoka.ila siku zilipoisha undugu na urafiki uliisha pia.ukaribu ukatoweka nikajikuta nateseka sio kwa ajili ya pesa kuisha ila ule ukaribu wa toka enzi.nikagundua bora ukiwa na pesa iwe kimyakimya tu
 
Furaha hainunuliwi but natural,so kupotea kwa Furaha inategemea na kipi kinakusibu tym hiyo....so haijalishi you are poor or rich tatizo ni kisababishi cha Furaha kuondoka.
 
Umasikini ndo sababu kubwa ya huzuni duniani. Na jamii nyingi zenye masikini wengi huwa zinaongoza kwa kuwa na maovu ya kila aina.

Unasemaje utajiri haukupi furaha?
Angalia pale ndugu yako wa karibu anateseka kwa ugonjwa ambao anatakiwa akatibiwe nje ya nchi na huna uwezo wa kumudu hiyo gharama.
Utaendelea kuwa na furaha pale unapokosa chakula? Au familia haijui kuwa itakula nini?
Pesa inaleta furaha, inavuta marafiki na ndugu, inaleta connection, inakufanya uende sehemu yeyote na kufanya lolote.
Ukiwa na pesa kila mtu atataka awe karibu nawe, ila usipokuwa nao utaishia kubaki na ndugu zako tu.
Ukiwa na pesa itakufanya ununue accessories zitakazokufanya upate furaha mfano magari mazuri, nyumba nzuri, wanao watasoma shule nzuri, utakula vizuri, kulala vizuri nk.
Hao wasio na hela ndo hawana furaha kabisa. Na hawatakaa wawe na hiyo furaha.
 
Ndio karibu wote tunazitaka pesa tena sana, ndio pesa ni chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika ambayo zimejengwa kwa msingi huo huo wa pesa, lakin ukweli kwamba Furaha hailetwi na kwa kuwa na pesa mingi, unaweza ukawa na pesa bado ukagongewa sawa na yule ambaye hana tuu na kukongewa kunaumaa kwa wote aliyenazo na asiye nazo, na hapa sijasema kama et masikini ndo wanafuraha la hasha Furaha huletwa na namna ulivyoridhika na maisha yako, aman uliyonayo pamoja na Uhuru hivi huleta furaha
 
Back
Top Bottom