Samawia
JF-Expert Member
- Dec 6, 2017
- 592
- 466
Wewe ni dereva wa masafa marefu, wakati mwingine miezi miwili huonekani nyumbani, mkeo naye mjasiriamali muda mwingi anakuwa kutafuta riziki, ma house girl nao ndio hivyo mara leo yupo mara kesho kaondoka, mkeo ana mdogo wake wa kike baada ya kuona usumbufu wa ma wa mabinti wa kazi anaamua kuja kukaa kwa dada yake ili awe anamsaidia kazi.
Baada ya miezi kama minne mkeo anagundua mdogo wake anatoka na majirani wawili (waume za watu), baadaye tena anakuja kuambiwa mdogowe ana wanaume wengine kadhaa. Mkeo anaamua kukushirikisha mumewe kuhusu mienendo michafu ya shemeji yako, shemeji yako 1,2,3,7,9 30.
Mume unaanza kuwaza namwamini sana mke wangu. Je, kwa tabia hii ya mdogo wake haiwezi kumletea vishawishi naye akaanza tabia chafu? Sijui nimwambie dada yake amtimue au nimtimue mwenyewe? Mkeo naye anawaza, wake za hawa michepuko wa mdogo wangu tunaheshimiana sana je wakijua itakuwaje si watajua mimi na mdogo wangu letu moja. Je, nitaheshimiana nao kama zamani? Je, nimwambie mdogo wangu aachane na hayo mambo au nisimwambie ila nimrudishe tu nyumbani?
Vaa uhusika wa mume au mke, utafanyaje?