Ukiwa muongo jitahidi kufanya utafiti

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
UONGO HUU WA VIJANA WA LUMUMBA NI WA KITOTO KABISA.

Kwambá viongozi wakuu wanatoka upande mmoja, upande upi? Au CHADEMA ni chama cha kaskazini???
Viongozi wakuu wa CHADEMA wako sita. Kama hujui basi jina na mkoa ambao kila mmoja anatoka ni kama ifuatavyo.
1. Mwenyekiti Freeman Mbowe (Kilimanjaro)
2. Makamu Bara Prof Safari (Tabora)
3. Makamu Zanzibar Said Issa (Kaskazini Pemba)
4. Katibu Mkuu Dr. Mashinji (Mwanza)
5. Naibu KM Bara J. Mnyika (Mwanza/Dar)
6. Naibu Zainzibar Salum Mwalim (Unguja)

Mwanasheria Mkuu wa Chama, Tundu Lissu (Singida)

Kurugenzi ziko tano tú. Wakurugenzi wake kwa majina na Mikoa wanayotoka ni kama ifuatavyo;
1. Fecha na Utawala, Roderick Lutembeka (Kagera)
2. Sheria na Haki za Binadamu, Peter Kibatala (Morogoro)
3. Ulinzi na Usalama, Benson Kigaila (Dodoma)
4. Bunge na Halmashauri, Josephine Lemoyang (Singida)
5. Mawasiliano, Mahusiano na Mambo ya Nje, John Mrema (Kilimanjaro)

Kuhusu wabunge wa Viti Maalum, kwa utaratibu wa Chama kila Mkoa una mbunge mmoja. Lakini kuna mikoa mingine ina zaidi ya mmoja kutokana na kukidhi vigezo vilivyowekwa.

Kuhusu wagombea wa Ubunge wa Africa Mashariki, ni uongo mkubwa kusema kwamba matangazo hayakutolewa. Matangazo yalitolewa nchi nzima. Kuomba au kutoomba ni hiari ya mwanachama. Lakini hakuna kanuni yoyote inayolazimisha kwamba moja atoke bara na mwingine visiwani au mmoja awe mwanamke na mwingine mwanaume. Hata kama watu waliomba, je walikidhi vigezo vya ndani ya chama?

Lumumba kaeni kimya na kufikiria vitu vya maana na vyenye ukweli sio kupotosha.
 
Back
Top Bottom