Ukiwa DOMO ZEGE Kuwa Mbunifu Kama Huyu Mlokole.

The Great Emanuel

JF-Expert Member
Apr 3, 2015
2,695
2,000
Ilikua zamani kidogo miaka ya 2007 kijiji flani hivi Tz hapa, Kulikua na Dada mmoja hivi mcha Mungu kweli kweli yani mlokole vibaya mno.

Sasa kuna kijana mmoja hivi aliitwa Emanuel walikua wanasali kanisa moja huyu kijana alimpenda sana yule Dada shida ikawa kwenye kumwambia, Maana mdada ana misimamo hatari.

Na jamaa ndo wale mdomo zege basi akajitafakali sana afanyaje ampate yule Dada amuoe kabisa yani, Basi akapata njia........... Unajua alifanyaje hehehe..
Alienda town akanunua bonge moja la tochi lina mwanga hatari siku hiyo usiku akaenda kwao na yule mdada, Sasa kama mnavyojua nyumba za kijijini nyingi zimeezekwa na nyasi.

Basi mchizi akapanda kidogo kwenye chumba cha binti akafunua nyasi kidogo kwa juu akapiga tochi aisee chumba kizima kikawa na mwanga mkubwa sana. Basi yule binti mlokole akastuka sana jamaa akaanza kuongea huku kabadili sauti kabisa akasema

" USIOGOPE MWANANGU MIMI NI MALAIKA NIMETUMWA NIKULETEE UJUMBE, BWANA AMENITUMA NIKWAMBIE KUWA ANAJUA UNASUBIRIA MUME MWEMA NA AMEMUONA KIJANA UNAESALI NAE YANI EMANUEL YA KUWA ANAFAA NA NDIE ATAKAEKUA MUMEO WA MAISHA YAKO YOTE HIVYO TII SAUTI YA BWANA, KWAHERI MWANANGU".

Jamaa akazima tochi akashuka akasepa baada ya siku tatu akamfuata akamwambia nia yake mdada hakuvunga akasema bwana alishanifunulia kuwa wewe ndo Mume wangu na nimekubali sababu Bwana anajua kilicho chema kwangu.

Hivyo wakaoana na sasa hivi wana watoto jamaa akaamua kumwambia ukweli mkewe wa mwanga wa tochi hahaaha wanaishi raha mustarehe sasa hivi.

Sasa je huu uongo mzuri au mbaya?
NB: Msiniite shigongo ni true story hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom