Ukithubutu kukutwa UTATUMBULIWA

GLOBE 360

New Member
Aug 27, 2016
3
45
Imefika mahali watumishi wa umma watambue kuwa muktadha wa ufanyaji kazi katika sekta ya umma umebadilika sana. Hali imebadilika sana na tabia ya kufanya kazi kwa mazoea haipo tena. Kwa sasa, taka usitake lazima uwe makini (proactive).

Mfano, kama mtumishi wa umma (boss au mtu wa kawaida), unatakiwa umsome Rais na kujua na kutambua maono yake kuhusu masuala mbalimbali. Ikiwa Rais anazunguka nchi nzima akisema anataka gharama za kuishi kwa watanzania zipungue, yakupasa wewe na taasisi yako mtafute mikakati ya kuhakikisha kuwa azma ya mwenye maono (Rais) makuu ya nchi inatimia.

Nyie watu wa mamlaka ya anga, je, nini maono ya Mhe. Rais Magufuli kuhusu sekta yenu? Watu wa TANESCO, watu wa reli, watu wa maliasili na wengine wote, lazima mjue na mtambue nini matarajio ya Rais wa nchi kuhusu kazi mnazozifanya.

Kazi ya Rais ni kutoa maono (Vision) na Dira (Direction) wakati taasisi kupitia kwa wataalamu wake zinatakiwa zitengeneze mikakati ya jinsi ya kufikia malengo ya nchi. Kazi yako ni kuhakikisha unashauri kitaalamu na kufikia muafaka na boss wako. Tengeneza mikakati ya kuleta ahuweni kwa wananchi na si mikakati inayoongeza mzigo kwa wananchi.

Haiwezekanani taasisi au wakuu wa taasis mwangushe Rais juu ya maono yake kwa nchi na ziendelee kunyamaziwa. Yafaa nini taasisi au mtu anayeshindwa kuwa sehemu ya maono ya mkuu wa nchi?

Hata ingekuwa mimi, ningemtumbua mtu yeyote ambaye simwamini au naona hawezi kufanya kazi, na nikiona ananikwamisha, nitamtumbua sawasawa. Kwa hiyo Mhe. Rais Magufuli, endelea kufanya kazi, na ambaye anakuwa kikwazo basi na afutiliwe mbali.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,374
2,000
Mikakati mizuri kwenye makaratasi tunayo mingi,tatizo ni funds to finance development projects,and when we think we are almost there,out of the blue anatokea mtu,mtu huyo anaweka makodi ya ajabu yanayowakimbiza wafanyabiashara,mkiwa hamjamaliza machungu mnafatwa huko huko kwenu mnachambwa kwa kuwa na mabalaa na majina ya ajabu ajabu ..kweli wamsome mkuu na wamfatishe. Makondakta ni mfano wa kuigwa!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom