Ukitazama malengo yako unaona nini?

Ukitazama malengo yako unaona nini?

Vicent Stephen

New Member
Joined
Mar 30, 2018
Posts
1
Reaction score
0
UKITAZA MALENGO YAKO UNAONA NINI?

Unapotazama na kufikiri juu ya NDOTO na MALENGO yako unaona nini? Ni maswali gani yanakujia kichwani kwako unapoitazama ndoto yako? Je wewe ni mmoja kati ya watu wanaotazama NDOTO zao na HALI zao za sasa na kisha kusema kwa hali walizonazo ni vigumu kufikia ndoto hizo?. Kama unamtazamo huu ni wazi kabisa itakuwa vigumu kufikia ndoto yako.

Naomba nikueleze mambo matatu ambayo yatakusaidia kufanikisha ndoto yako bila kujali hali uliyonayo sasa.

1. USIOGOPE KUWA NA NDOTO KUBWA - bila kutazama hali yako ya sasa ainisha unataka nini katika maisha yako. Hali yako ya sasa isiwe kikwazo katika kuchagua nini unataka katika maisha yako.

2. FANYA TATHMINI YA VIKWAZO vyote ambazo vinaweza kukukwamisha kufikia ndoto yako kisha tengeneza mpango wa kukabiliana na vikwazo hivyo.

3. USIOGOPE KUSHINDWA - mtu anayeogopa kushindwa hawezi kufanya chochote . Ni lazima hofu hii upambane nayo ili uweze kusonga mbele.

Uwezo wako wa sasa na hali yako ya sasa isikufanye uogope kuwa na ndoto kubwa.

You Deserve The Best!
Vicent Stephen
 
Back
Top Bottom