Wana jamii siku zote tujifunze kwamba ili mali yako isalimike mkabizi mwizi akulindie kwa sababu mwizi anajua mbinu zote wezi wanazotumia kuwaotea watu wawaibie, pia anajua njia zote wezi wanazopita kuja kuiba.
Mheshimiwa wetu tuliyemweka magogoni kesha kuwa mbunge kwa zaidi ya miaka 15 anajua kuwa wabunge huwa wanasainiana, moja anamsainia mwenzake mwisho wa siku wanavuta posho bila kuhudhuria kikao, yaani wanapata hela bila kufanya kazi kwa sababu vikao vinachosha asikudanganye mtu, ukitaka kujua vikao vinachosha angalia kikao cha misa kirefu sana ni saa moja na nusu lakini mtu unachoka kweli.
Kudhibiti wizi huo wa kuvuta posho bila kufanya kazi mahudhurio ya wabunge yatahakikiwa kwa kutumia alama za vidole (finger print) . Ukitega huna chako.
Pili matumizi ya waheshimiwa mengi huwezeshwa na makatibu wakuu wao, anamwambia katibu mkuu niandikie night ya siku 10 halafu na yeye katibu mkuu anapitisha za kwake humo humo, sasa Mheshimiwa anakwenda mwenyewe bank kufuta ili kumaliza matatizo yake binafi sasa ole wako katibu mkuu umwibie kama hajakukata mguu.
Ni hayo tu kwa leo