Ukitaka kumla Bata

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,136
4,298
1)Bata hakosi kasoro,eti anakula nini
Mwenye manyoya nyororo,yapendwa take maini
Bandani awe mtoro,usimfuge kwanini
Ukitaka mla bata,usimchunguze sana.

2)Bata hakosi kasheshe,aendapo mtaroni
akulacho si kutishe,we jifanye hauoni
chunga sije kuangushe,litakutoka kooni
ukitaka mla bata, usimchunguze sana

3)Bata hakosi ubabe,penda kupanda kichwani
siyo yote umbebe,mpe sheria bandani
so makofi umzabe,umwadhibu yadharani
ukitaka mla bata,usimchunguze sana

4)Bata hata akinuka,usijizibe puani
cha kufanya we inuka,ukamuweka uani
chunga sije kurupuka,atakuacha juani
ukitaka mla bata,usimchunguze sana.


5)Bata anayo mabawa,haweza ruka hewani
linda lako sana bwawa,asitoroke ziwani
mamba wataja mgawa,akuone hayawani
ukitaka mla bata,usimchunguze sana.


6)Bata akusumbuapo,mnunulie kidani
kisha umpe kiapo,asirudi makosani
akikosa ni kichapo,ila siyo cha usoni
ukitaka mla bata,usimchunguze sana.


7)Bata japo ni mtamu,nyama ye sana laini
kumla huishi hamu,hasa sehemu za chini
Miguu haina sumu,ukiichoma jikoni
Ukitaka mla bata usimchunguze sana

SHAIRI -UKITAKA MLA BATA.
MTUNZI-Idd Ninga,Arusha
iddyallyninga@gmail.com
+255624010160
 
Back
Top Bottom