Ukitaka kumjua anayelia kinafiki msibani zingatia haya tafadhali

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,214
  1. Hulia kwa ' timing ' ambapo kama akiona Waombolezaji wanaoingia ni ' Walalahoi ' hufuta machozi haraka au hunyamaza lakini pindi amwonapo Muombolezaji ' Tajiri ' ameingia hulia ghafla na kwa kutoa sauti ya juu ili hata baadae akimpiga ' mzinga ' ( akimuomba Hela apewe kihuruma huruma )
  2. Hulia sana lakini ukimwangalia kabisa ' machoni ' utamkuta ni ' mkavu ' na wengi wao ndiyo hupendelea kwenda ' Chooni ' mara kwa mara ili kujiuliza huku wakijimwagia maji ' usoni ' na kurudi kwa wenzao kuendeleza ' Unafiki ' wao na wapo wengine ambao hudiriki hata tu kujipaka pilipili machoni ili ama macho yawe ' Mekundu ' sana au yatoe ' michozi ' mingi.
  3. Hulia muda mchache halafu mara nyingi utamwona anaulizia wenzake Chakula ni saa ngapi na ukweli hapa ni kwamba wengi wetu tunahudhuria ' Misibani ' kwa sababu ya kula ' Msosi ' ili tubane ' Bajeti ' zetu ambazo kimsingi kwa sasa nyingi zimetetereka ' kimtindo '.
  4. Nijuavyo kikawaida Mtu anapolia basi kila kitu chake kinakuwa hakipo sawa na hata ' akili ' yake muda huo inahama lakini utakuta Mtu analia tena kwa nguvu kabisa lakini Simu yake au Pochi yake haviachii au havidondoki ( hiki ni Kiashirio Kikubwa cha Unafiki Msibani )
  5. Mnaweza mkawa mnasafirisha kabisa ' Maiti ' kuelekea kuzika labda huko Mkoani lakini cha kushangaza mpo ndani na ' Mwili ' kila mkikaribia ' Baa ' mnapaki Basi lenu pembeni ' Marehemu ' mnamwacha peke yake na Wote mnaenda ' kupombeka ' huku kuna wengine hata hutumia muda huo kufanya ' Ufuska ' na kuonyesha ' Unafiki ' wao mkiwa tu mnakaribia pale Kijijini kwenu utaona wale wale Watu ambao walikuwa ' wakipombeka ' na kupiga kila aina za ' kelele ' njiani ndiyo huanza kulia tena huku hadi ' wakigalagala ' sakafuni na kujizungusha utafikiri ' Chatu ' kameza ' Mbuzi.
  6. Hulia huku wanajipiga ' Selfie ' na ' michozi ' yao na wapo wengine ambao unaweza ukawakuta muda wote ' wameuchuna ' zao tu hawalii wanapiga ' Umbea ' lakini ikitokea tu wameona Chombo Kimoja cha Habari kipo pale kufanya coverage ' mubashara ' utaona Mtu analia halafu ' Msura ' wake wote anaulazimisha kabisa kuelekea ilipo lens ya Camera na ole wako Wewe Cameraman usimchukue vizuri utaambulia ' Mitusi ' ambayo hujawahi kukutana nayo.
  7. Utakuta muda wote ' analia ' tu tena kwa sauti zote uzijuazo na kwa nguvu zote kama za ' Goliati ' lakini ikitokea tu bahati mbaya hapo katika ' mjumuiko ' wenu Msibani mmoja wenu ' Kajamba ' utamkuta yule yule aliyekuwa akilia sana ananyamaza ghafla na kuanza kulalamika kuwa kuna ' Muombolezaji ' kati yenu ' amejamba ' huku akisonya sonya na kutoa ' mitusi ' ( hivi mwenye uchungu hasa na Marehemu akisikia Mtu Kajamba tu tena wakati mwingine kwa bahati mbaya na harufu anaisikia anaweza akasitisha kweli kulia na kuisikilizia harufu na kuanza kupovuka hovyo kwa Waombolezaji wenzake? Huo ndiyo Unafiki wenyewe ninaousema )
Kama upo Msibani sasa au karibuni utaenda Msibani jaribu kufuata haya mambo saba ' makuu ' niliyoyaorodhesha hapa ili ' ujiridhishe ' mwenyewe na ikiwezekana ukikutana na hao ' Wanafiki ' ama uwape ' makavu ' yao au hata uwafukuze kabisa hapo kwani hawatakuwa na msaada wowote ule.

Asubuhi njema.
 
Back
Top Bottom