Ukistaajabu ya Sophia Simba utaona ya Chiza

The Planner

JF-Expert Member
Dec 1, 2010
357
118
Nilikuwa nasoma thread inayomhusu Sophia Simba na vioja vyake ktk C10, hapohapo nikakumbuka Statements za naibu waziri wa kilimo akiongea na waandishi wa habari kwamba serikali haiwezi kudhibiti mfumuko wa bei za vyakula., Napata shida kujua hawa watu wanafanya nn? kama unakili huwezi kufanya mabadiliko si unajiachia wanaoweza wachukue nafasi,.inakera kusikia utumbo kila siku
 
Baraza la mawaziri wengi wao wapo pale kwa ajili ya maslahi ya chama,vikundi na familia zao ndio maana hawana uwajibikaji na ni mbumbumbu ambao hawajua hata nini maana ya kuwa kiongozi,hivi kiongozi mwenye kutoa maneno ya kukatisha tamaa anawafundisha nini walio chini yake?
Badosina imani na uongozi wetu hapa Tanzania mpaka pale tutakapopata mabadiliko ya kweli chini ya chama kingine.
 
Kama Waziri mkuu amesema pamoja na matatizo ya umeme uchumi wetu umeendelea kukua wakati hata mtoto mdogo hawezi kuamini unategemea nini jipya toka kwa walio chini yake?
 
Nchi zingine zote ktk maswala ya kuteteleka kiuchumi huwa na mikakati mbalimbali kuhakikisha kuwa wananchi wao hawathiriki. Ukisikia kauli za PM na kina Sofia Simba unapata shida kujua kweli serikali yetu iko kwa ajili ya wananchi au ni kwa ajili ya viongozi na vibaraka wao au hata wanajua wajibu wao.

I magine kwenye swala la umeme wananchi wanateseka na mgawo ambao haujulikani utaisha lini huku unasikia migodini hawana rationing yeyote! Kweli wandugu?

Ni bahati mbaya sana kuwa watu tuliowakabidhi nchi kuiongoza wamezoea kuwa wananchi ndio wanawajibika kwao na si wao kuwajibika kwa wananchi
. SHAME. As long as hiyo itaendelea kuwa hivyo tukae tukijua kuwa hakuna mabadiliko yeyote yatatokea kwa maana ya kuwapunguzia wananchi ukali wa maisha.
 
Ndiyo maneno ya majuha wetu. Hawana jambo jingine lolote. Mimi huwa siwasikilizi kujiepusha na hasira. Sitaki kupata presha mimi.
 
Timu ni ile ile jamani...uwanja ndio tofauti................................
 
Back
Top Bottom