Idd Ninga
JF-Expert Member
- Nov 18, 2012
- 5,539
- 4,854
1>peku peku kutembea,mwiba waweza kuchoma.
Na domo lenye umbea,la tetemeka kwa homa.
Waloanza kulegea,sindano tumewachoma.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
2>usiku ule wa giza,mwenyewe chini dondoka.
Harufu ya yai viza,imeanza kuondoka.
Kifo ukijiapiza,mipaka umepetuka.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
3>limepigwa shuti kali,macho walitumbulia.
Wewe ni dhoufu hali,matibabu kimbilia.
Kiri ama ukubali,mbona unajililia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
4>siyo mganga wa jadi,ramli wajipigia.
Ushindi yako miadi,mwenyewe wajipangia.
Mtapofuta ahadi,wema mtajipatia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
5>utadondokea pua,hakika utazimia.
Hasara yako yakua,hilo hujaligundua.
Akili imeungua,mawazo yajifukia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
Shairi=UKISHINDWA LA MKONO.
mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 au 0655519736
Na domo lenye umbea,la tetemeka kwa homa.
Waloanza kulegea,sindano tumewachoma.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
2>usiku ule wa giza,mwenyewe chini dondoka.
Harufu ya yai viza,imeanza kuondoka.
Kifo ukijiapiza,mipaka umepetuka.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
3>limepigwa shuti kali,macho walitumbulia.
Wewe ni dhoufu hali,matibabu kimbilia.
Kiri ama ukubali,mbona unajililia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
4>siyo mganga wa jadi,ramli wajipigia.
Ushindi yako miadi,mwenyewe wajipangia.
Mtapofuta ahadi,wema mtajipatia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
5>utadondokea pua,hakika utazimia.
Hasara yako yakua,hilo hujaligundua.
Akili imeungua,mawazo yajifukia.
Ukishindwa la mkono,la mguu hutoweza.
Shairi=UKISHINDWA LA MKONO.
mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 au 0655519736