Ukishindwa kutajirika hapa Tanzania, huwezi fanya hivyo nchi nyingine Afrika

Melki the Storyteller

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,701
9,779
Ukiondoa nchi zilizoendelea na zenye uchumi mkubwa kuliko wetu kama vile Kenya na Afrika kusini, nchi nyingi zilizobaki zinaishi maisha ya ujima isipokuwa kwenye miji yake mikuu. Mfano hapo Zambia mpakani, vijana wao wengi ni wa ovyo, kazi zao hufanyika asubuhi mpaka saa nne, baada ya hapo ni mwendo wa tungi na kuzagamuana Sio wao tu, hata na nchi nyingine kama hiyo, nimetolea mfano kwa kuwa nina experience nayo! Hawawazi kuhusu kesho, mara kujenga, mara maisha mazuri hapo baadae Yanini kujipa presha wakati maisha yenyewe mafupi? Hapo utawakuta wamezunguka mbuyu wa bia wakisafisha nyoyo taratiiibu

Katika udadisi wangu nilioufanya inaonesha wazi tatizo kubwa lililopo ni mifumo tu ya kupata pesa. Mifumo haipo na hata inayohisiwa kiwepo haieleweki, imebaki kwenye miji mikuu Ukiji overdose kwenye kazi, pesa ya muda wa ziada inawezekana usiipate! Vijana wanachakarika asubuhi hadi saa nne, wanapata kiujira wanaibukia vitambaa vyeupe WALIOJALIWA UWEZO WA KUDADAVUA MAMBO NAHISI WAMENIELEWA!

Nchi kama Kenya, kupata pesa kwa mtu ambaye si mtumishi wa umma hasa vyeo vikubwa vikubwa, au kama baba yako hakuwahi kumiliki ardhi, au wewe ni mtu usio na connection hata zile za kuwa chef kwa hotel ujue tu habari yako imekwisha! Kusema eti ngoja nisome ili baadae nije kuwa na pesa za kulaza chini ya magodoro utakuwa unajidanganya tu

Hapa kwetu nchini ukiwa na mtaji tu, basi umetoboa kimaisha! Japo connection ni kitu cha msingi saana hasa ukiwa Dar es salaam. Mara ya kwanza nakuja Dar, nilikuwa na 500k ya mtaji, niulize iliishia wapi! Ukubwa wa mtaji wako hapa bongo, ndo kasi ya utengenezaji wa utajiri wako!

Nchi kama kenya wanaishi kibepari sana, biashara zilizo nyingi ziko chini ya makampuni, sasa we mwenzangu na mie kimbilia huko bila kuwa na connection, uende na mtaji wako wa 3M kufungua mashine ya kusaga mahindi kama hujageuka kuwa kibarua wa soko lako WENGI HAMUWEZI ELEWA VITU HIVI

Napenda sana kuwa motivational speaker na siku zote huwa niko pamoja na babu mmoja hivi ambaye naye ni motivational speaker wa miaka hiyo ya 60 akijaribu kunipatia story ya jinsi upatikanaji wa pesa ulivyokuwa mkubwa enzi hizo jijini Dar es salaam, enzi za utawala wa mzee wa Ruksa! Kwamba pesa zilitapakaa mitaani, Dar es salaam ya zamani ilikuwa hata ufanye biashara ipi, ni lazima tu utatoboa.

Kikubwa tafuteni mitaji. Wekeza pesa upate pesa zaidi! Tia pesa nyingi uwezavyo ili upate mafanikio makubwa yawezavyo! Karibu matajiri wote Tanzania hawakutoka familia za kitajiri (ila motivational speaker bhana ) lakini nchi kama Kenya, kama wewe umezaliwa maskini, ni maskini tu hadi kizazi chako!

Wala elimu sio njia ya mafanikio, bali ni namna fulani ya kufuta ujinga wa kimwonekano! Msomeshe mwanao mpaka ma vyoo makubwa, ili utujazie server zetu za mitandao ya kirumi kutoka mabwenini mwao

Usikubali kushindwa, tafuta kaupenyo ujipenyeze, hii nchi ni yetu sote Ukipata nafasi itumie uwezavyo Kuna kijana kaja ofisini na shida nimempa milioni Laki si pesa! Usikubali wafaidi wachache, kaa kwenye mstari!

Ukifikisha miaka 35 hapa nchini halafu hata nyumba ya vyumba viwili huna, jipige kifuani mara tatu kisha jisemee moyoni kuwa "Mimi ni mbw* k*k*", kisha zamisha kichwa chako kwenye ndoo ya maji baridi!
TAFUTA HELA

NAISHIA HAPO, MWENYE KUSKIA NA ASIKIE, ALIYETOKA KAPA, BASI APITIE KULE MMU KUREFRESH MIND
 
Ukifikisha miaka 35 hapa nchini halafu hata nyumba ya vyumba viwili huna, jipige kifuani mara tatu kisha jisemee moyoni kuwa "Mimi ni mbw* k*k*", kisha zamisha kichwa chako kwenye ndoo ya maji baridi!
TAFUTA HELA

Ulianza poa ila hapo ndipo ulipoharibu uzi.... Kwenye suala la nyumba kuna factors nyingi sana....

Sababu wewe ni motivational speaker najua utakuwa umenielewa...
 
Nimewahi kupiga story na jamaa watatu ambao wako vzuri sana kiuchumi one of their regrets ni kuhusu kujenga nyumba mapema wanadai mil 100 ya kujenga nyumba ukiizungusha kwny biashara una pesa nying sana kwa muda mfupi
 
Huu Uzi umeandikwa na mtu mwenye akili ndogo sana
Utajirike kirahisi nchi ambayo Ina GDP ya $62billion??
 
Bongo ngumu weekend zinaanzaga jumatano
JPEG_20220805_135809_8019652951306186594.jpg
 
Huu Uzi umeandikwa na mtu mwenye akili ndogo sana
Utajirike kirahisi nchi ambayo Ina GDP ya $62billion??
Kwa mbaali ukifikiria jamaa yupo sahihi,sijasoma Uzi sababu Ni mrefu ila Title ina ukweli,

Kwa mfano, Tanzania kupata ardhi Ni Rahisi Sana kuliko huko Marekani,huku mikoani unaweza ukanunua hata heka 20 kwa less than 5 millions, tatizo tulilonalo Ni Soko tu ndio hakuna kwa baadhi ya mazao mfano parachichi nk

japo sizugumzii utajiri mkubwa,lakini nazungumzia maisha Yale ya kumiliki vijumba vinne,gari tatu yanawezekana kwa urahisi kuliko USA
 
Gradueta huyu
 

Attachments

  • Screenshot_20220805_141157_org.mozilla.firefox.jpg
    Screenshot_20220805_141157_org.mozilla.firefox.jpg
    114.6 KB · Views: 38
Back
Top Bottom