Ukiritimba katika huduma za kibenki Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ukiritimba katika huduma za kibenki Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Manyanza, Jan 28, 2011.

 1. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nimekuwa nikiishi na kufanya kazi visiwani zanziba kwa muda wa mwaka mmoja, nimelazimika kutoa malalamiko yangu kupitia JF kwa sababu naamini watu wengi wanaingia humu ikiwemo viongozi wakuu wadau wa mabenki hapa nchini.
  Malalamiko yangu ni katika kwenye huduma ya ufunguaji wa akaunti visiwani Zanzibar, kuna masharti magumu sana ambayo ni vigumu kuyatekeleza…
  Ukitaka kufungua akunti katika benki yoyote hapa Zanzibar timiza yafuatayo
  1. Barua ya Sheha: ambaye tunasema ni mwenyekiti wa serikali za mitaa kwa upande wa bara, utata unaokuja wakati wa kwenda kuchukua barua ya utambulisho hapa ni kwamba utapata usumbufu wa kutoa hela ya wino, ( hii ni rushwa) au wakati mwingine ukionekana wewe una jina la kikristo ni tatizo tupu napo, na baadhi ya sehemu za mashekha huwa linaangia suala la uanachama wa kisiasa hapo napo inakua ishu kupata barua ya utambulisho.

  2. Kitambulisho cha uraia: hii moja ya kero kubwa sana hapa Zanzibar wenzetu hawatambui kadi ya mpiga kura eti wanasema inawezekana ni feki na haikubaliki wao wanachotaka kitambulisho cha uraia, na wakati tunajua kabisa kwa upande wa bara hali halisi ilivyokua kuhusu sakata la vitambulisho vya uraia na waziri wa mambo ya ndani alivyozua utata katika zabuni ya utengenezaji wa vitambulisho wakati ule, na ukijaribu kuwafafanulia hali hali halisi hawataki kabisa kuelewa wanaegemea msimamo wao, halafu ishu nyingine kukipata kitambulisho chao ambao kinaitwa cha Mzanzibari mkaazi ni ishu masharti magumu hata ya karumanzira yana unafuu “ ili upate hicho kitambulisho cha ukaazi ni lazima uwe umeishi hapa Zanzibar sio chini ya miaka miwili ( sina uhakika sana maana sijakutana nalo) na masharti mengine mengi yasiyo kua na maana, na bila kitambulisho cha ukaazi huwezi kuchukua pesa zako benki hasa ukiwa na cheque ambayo imeendikwa jina lako ( hii ilinitokea kwenye Benki ya BPZ niliandikiwa cheque kwenda pale wakagoma kunipa pesa mpaka ikapigwa simu kwa mtu aliyeniandikia cheque ili aje athibitishe na kunitambua) vilevile huwezi kupata hata leseni ya udereva utasoma katika shule zao za driving wakati wa kuchukua leseni utaombwa kitambulisho cha ukaazi(lengo langu sio kuchanganya mada hapa nilikua najaribu kutolea mfano ni jinsi gani serikali ya Zanzibar isivyo thamini kadi yetu ya mpiga kura.
  3. Pasipoti au cheti cha kuzaliwa: huwa ninashngaa sana kwa hawa ndugu zetu hivi hawajui kwa upande wa bara passpoti na cheti cha kuzaliwa unavipata kwa kutumia kadi ya mpiga kura? Basi wao huwa wana demand zaidi Pasipoti au cheti cha kuzaliwa nakuidharau kadi ya mpiga kura. Sina haja ya kulifafanua sana hili kwa sababu humu wote ni Great Thinkers mtalitafakari kwa kina na mapana.
  Hivyo ni baadhi ya vitu ambavyo ni vikwazo katika kufungua akaunti katika Benki yoyote hapa Zanzibar, na ukiaangalia masharti hayo yanayolewa na benki zote ambazo hata bara zipo, mimi nashindwa kabisa kuelewa ni kwanini huku Zanzibar hali ipo namna hii?. Ingawa wengi wetu tunafahamu kabisa masharti ya kufungua akaunti ambayo ni rahisi kuyatimiza lakini kwa huku zanzubar ni ngumu sana kwa sisi watu tunaotoka Tanzania bara.
  Nina mifano michache ya Benki ambazo nimeenda kuomba kufungua…
  1. EXIM BANK: nilifanikiwa kufungua akaunti pale na hapa kua na masharti magumu kwa sababu Bank ndio ilikua imeanzishwa na ilikua inakusanya wateja. Nilitakiwa kupeleka
  · Picha mbili passpoti size
  · Photocopy ya kitambulisho cha kupigia kura
  · Refarii mwenye akaunti Exim
  · Kianzio cha kufungulia akaunti

  2. NBC BANK: kutokana na usumbufu unaojitokeza mara kwa mara kwa Benki ya Exim nikaona bora nitafute option nyingine ili kuepuka usumbufu usio wa lazima, NBC Bank nikagonga mwamba na vikwazo vilikuwa kama vifuatavyo…..
  · Barua ya utambulisho kutoka kwa Shekha
  · Passport ya kusafiria au cheti cha kuzaliwa ( sina Passpoti na sijawahi kusafiri nchi yoyote)
  · Kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi
  · Kitambulisho cha ofisi ninayofanyia kazi na barua kutoka kwa bosi wangu ( ishu ya kufungua akaunti ni private bosi wangu au mtu yoyote haimhusu kabisa)
  3. FBME,CRDB,NMB niliyokutana nayo kwa zaidi ya asilimia 98 yanafana na niliyoyakuta NBC BANK
  Orodha ya Bank ambazo zipo Zanzibar na Tanznia bara ni
  NMB,CRDB,NBC,FBME,POSTA BANK,BARCLAYS,DIAMOND TRUST,
  Swali langu kwa viongozi wa mabenki, wizara ya fedha, benki kuu ya Tanzani, kwa nini hapa znzibar kunakua na mfumo ambao ni tofauti sana na Tanzania bara? Na kwanini wageni hasa wazungu inakua ni rahisi kwao kufungua akaunti katika Benki yoyote wanayotaka? ( sio kupata huduma za kutoa pesa bali kua na akaunti katika mabenki), na kwanini huku Zanzibar masharti ni magumu utadhani naenda kuomba mkopo wakati naenda kuhifadhi fedha zangu?
  Nadhani kuna haja ya kuliangalia hili na kulifanyia kazi ili uwiano uwe sawa katika kufungua akaunti kwa Zanzibar na Bara na masharti ya kipuuzi yaondolewe ,
  Hitimisho: Viongozi na wadau wanaohusika na mabenki wawape semina na maelekezo wafanyakazi wa mabenki wote hapa Zanzibar ili huduma zao ziwe sawa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar. Na vile vile wana JF wenye sauti na wenye ushawishi katika ngazi za juu naomba mlipigie kelele hili kwa viongozi wote wanaohusika ili lifanyiwe kazi…. Maana huku wabongo tunazinguliwa sana ……
  NAWASILISHA..
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Pole sana ahali yangu kwa hayo unayodai kuwa ni usumbufu.

  lakini kumbuka Zanzibar ni nchi na ina sheria zake katika kuhakikisha kuwa kunakuwa na usalama wa mali za bank. ndio maana masharti ya kufungulia bank ya NBC ukiwa Dar, Arusha au sehemu yoyote ile Bara ni tofauti kidogo na unapokuwa visiwani kwa maana ya unguja na Pemba (Zanzibar)

  Cha msingi ni lazima ukubali kufata sheria ili mradi tu uhakikishiwe pesa yako ipo salama. Kumbuka sheria ni zile zile ukiwa bara utatakiwa ulete barua ya utambulisho toka kwa mtendaji,( Zanzibar ni barua toka kwa sheha wa shehia yako). wadhamimi wawili wawe na account kwenye tawi lile,na pesa za kufungulia account. na kwa Zanzibar since kuna vitambilisho vya uraia ni lazima ukipeleka na kama umetoka Bara basi cheti cha kuzaliwa, kitambilisho cha mpiga kura ni lazima upeleke kwa uhakiki zaidi.

  Sio taabu bali ni sheria za hapo zanzibar, kama umekubali kuishi basi lazima ufate sheria zake.
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 29, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 589
  Trophy Points: 280
  Pole mkuu, nafikiri malalamiko yamefika.
  Tusubiri utekelezaji.
   
Loading...