kmbwembwe
JF-Expert Member
- Aug 16, 2012
- 10,870
- 7,752
Ni jambo la kutia huruma kuona Chama cha Demokrasia na Maendeleo - Chadema, leo kimeishiwa hoja kinaporomosha matusi kumtukana mtu aliyewashinda kwenye uchaguzi mkuu mwaka jana nafasi ya urais. Chadema walijiweka kama chama chenye kutetea utawala bora kwa karibu miongo miwili wakipinga rushwa serikalini na kwenye jamii kwa nguvu zote. Walifikia kiwango cha kuwataja mafisadi nchini kwa majina na kuiburuza serikali ambayo wakati huo ilivuta miguu kushughulikia tatizo la ufisadi na hata wakati mwingine kuonekana kuwalinda mafisadi.
Hivi sasa chadema inaona demokrasia ni pale tu wao wangeshinda uchaguzi. Sijui chadema kwa nini wanaona ni wao waliyostahili kushinda uchaguzi wa mwaka jana kwa kumkabidhi ugombea urais mtu aliyekua kama sera yao kumwita fisadi pale alipokua akiwania urais kupitia ccm. Mara mwenyekiti wao alipomfanya kimizengwe mgombea huyo aliyebwaga ccm kua mgombea wa chadema akabatizwa jina kama ni mwanamageuzi.
Chadema kumwita jpm dikteta na kumkejeli itaiangamiza chadema kwa sababu ni uongo na waliyomchagua jpm sio mazuzu.
Jpm ndio Deng Tsiao Ping wa Tanzania. Wananchi hawajali tena rangi ya paka ila wanataka paka anayeshika panya. Paka huyo ni jpm.
Viva jpm, a luta continua, a vitoria e certa.