Ukiona hii unakumbuka nini

Hivi ndo vilikuwa vitabu, achana na hivi vya kina Manzi na Nyambari Nyangwine. Watoto wanasomea mtihani tu na ukitwist tu swali wamefeli wote!!!! Na huo mpira ulikuwa na majina mengi kweli, "gozi", "kidaso" na mengine kibao. Si kuharibu "chachacha" na vile viatu vya "bora" lazima ununuliwe oversize tangu ukiwa la tatu na hapo hadi la saba unatinga tu. Soka unapigia, maji unachotea, shamba la mwalimu na kuni umevaa tu na Jumapili kanisani unavyo, siku ya sherehe ya LY unavyo tu!!!!
 
Tulikuwa tunatoroka class kwenda kucheza kitenesi..
 
Ukiona hicho kitabu na hako ka mpira unakumbuka enzi zipi?? Nini kilikua cha maana sana kwako wakati huo???




Nakumbuka Mitaala iliyokuwa na akili! Na mitaala hii ndo iliyotuletea Maprofesa tulionao leo.
 
Nakumbuka enzi zile wote tunasoma kitabu cha aina moja na tunatungiawa mtihani wa aina moja....sasa vitabu vya akina Nyambari Nyangwine vimeingizwa mtaani mmh
 
Hivi vitabu havikutufundisha kujibu tu mtihani... Kilikuwa kimesheheni nidhamu na maadili mema!
 
Ukiona hicho kitabu na hako ka mpira unakumbuka enzi zipi?? Nini kilikua cha maana sana kwako wakati huo???





..., nimekumbuka BULICHEKA na MKE WAKE LIZABETA..., na wagagagigikoko na mfalme wao...
 
Umenikimbusha uwanja wa mpira wa ushirika (sasa MUCCoBS)....good old days!!!
 
Nakumbuka magoli ya mawe. hakukawii kuzuka ubishani: "sio goli, imekata goli!"

Alaf si unajua kutofautisha timu, lazima tim moja wavue mashati? nilikua mwembaba kiasi kwamba ikitokea timu yetu wanatakiwa kuvua shati inabidi nitoke au nihame timu dah.

Ukiwa na viatu unaambiwa uvue kwa sababu wenzako wote hawana viatu, inabidi mcheze pekupeku....
 
Mwendelezo wa vitabu vya Mr &Mrs Daudi, ulikuwa na mafunzo makubwa sana. licha ya kutufundisha kusoma, kuandika na kuelewa hadithi nzuri za familia hiyo, vilitujenga sana kwa yale yaliyokuwa yanasimuliwa kwenye stori zao, kilimo, malezi na hata michezo kwani nakumbuka kitabu cha darasa la tano kilikuwa na simulizi ya mechi ya kirafiki. Nawakumbuka walimu wangu ambao kwa sasa wote ni Marehemu Shule ya Msingi Bukumbi, Missungwi huko Mwanza. Walikuwa noma kwa kufundisha R.I.P
 
Hii lazima uikumbuke Elimu supplier limited enzi hizo vitabu na madaftari yote lazima mletewe shuleni. hakuna kununua daftari wala pensel na kichongeo
 
Sie tulisoma vya mkoloni "mudhungu" Namkumbuka mwalimu wangu wa hesabu akivaa kaptura na kalamu akiichomeka kwenye stockings. Mpira tulicheza wa ngozi, ukishajaza upepo ile bladder unaifungia ndani ya gozi kwa kufungia Kamba za viatu.
 
kipindi hicho stationary ni mbili tu Taafif na elimu supplier shule zikikaribia kufungua foleni hadi wanawatangazia mje kesho:nono:
 
Nikikiangali hicho kitabu Mr and Mrs Daudi namkumbuka sana mwalimu wangu Amina Shabani wa shule ya msingi Mtunduru Singida vijijini mwaka 1988
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…