Ukimya wa watumishi wa umma juu ya kikotoo kipya, ni upole wao au kutojielewa?

Wao hujitetea kwa misingi ya kisheria kwani nchi hii ni ya utawala wa sheria.

Kwa mjibu wa sheria ya kazi Na. 6/2004 na kanuni zake za mwaka 2007 zinawataka kutumia TRADE UNION kama mwakilishi. Na tayari TUCTA, na CWT kama TRADE UNION wamesha wasilisha hoja zao serikalini.

Je mleta maada yeye kafanya lipi tofauti na kuleta hapa JF ambapo sio mahara sahihi pa kutatua kero za watu??.

Hizo trade unions zao ndio zinazotumika na watawala kuwakandamiza. Hizo hoja zao zitagonga mwamba wakienda serekalini, na hata wakienda mahakamani, kwani watawala wa kiafrika hawaogopi mahakama bali huogopa nguvu ya umma tu.
 
Watumishi hawawezi kuongea maana mkuu wao haoni ugumu kuwapiga chini akaajiri wengine afu wakasubiri mafao yao nyumbani, so ugali wanaulinda, kila mtu anapenda ugali wa serikali sio kila mtu anaweza kupanga akili yake akajiajiri
hawezi kuwapiga chini. hawezi
 
Wale wa Kenya juzi walitishia kugoma kisa kuhamishwa nyie mnapelekeshwa tu. Hamna nyongeza, hamna marupurupu, nauli za likizo unadai milioni 1 mtu anakulipa kalaki.

Enyi watumishi amkeni sasa, semeni basi! Ukimya wenu huo mtakuja chapwa bakora mcheke kwa kale kawimbo ka hapa kazi tu
Kwa nini hamtaki kukubali kuwa Tanzania imejaa "kondoo wa Nyerere?". Baada ya Nyerere tumekabidhiwa kwa AHM, BWM, JMK na sasa kibiko yetu JPM ambae pamoja na ukondoo wetu anatupiga mikwara mizito. Si watumishi tu karibu wote labda kule Zanzibar hufurukuta furukuta lakini huku mainland ni shida. Hata wanafunzi siku hizi si unawaona poa tu.
 
facebook_1545052137132.jpeg
 
Ukiwasikia wakuu wa vyama vya wafanyakazi wanaoongea lugha za kitoto. Kuna siku yule rais wa walimu alipongezwa na rais na tangu hapo sijui kama yupo. Sijawahi kusikia kauli zake akiwasemea walimu waliotunukiwa madaraja kipindi cha kuelekea uchaguzi was 2015. Hadi Leo walimu hawajapewa mapunjo kutokana kucheleweshewa marekebisho yao. Wapo wanaodai kwa miezi 6, 12 ,36, na wengine walipandishwa kisha kunyofolewa na wengine hawajapanda hadi Leo. Wapo baadhi ya walimu wa chini yao walipandishwa ila wao wakarukwa hadi Leo.
Tatizo ninaloliona kwenye uuongozi wa vyama vya wafanyakazi hawataki kuingia kwa wanachama wao kuibua matatizo ambazo ndizo wazitumie kuhoji mamlaka za ajira Bali wenyewe hujikita kupeana semina na kulipana maposho. Endapo wakipita kwenye mashina ya mahala pa kazi watapata changamoto na kuwa na uwakilishi utakaozingatia maslahi ya wanachama wao. Hii tabia yao ya kutatua matatizo ya wanachama kwenye semina haitowafaa kitu na daima wataendelea kuwa wasaliti
 
Je wewe umefanya jambo/jitihada gani kuwasadia? Hata kama wewe sio mtumishi. Mathalani Nelson Mandela alipigana na kufungwa miaka 27 kwa ajili ya wana_Africa kusini wote sio kwa manufaa yake pekee. Je wewe huwezi kujitoa kuwatetea watumishi kama tayari ushaona wanaonewa?

"Ukombozi unaweza ukaletwa na mtu wa ndani ama wa nje" ndo watu kama akina MARCUS GARVEY walifanya hivyo kipindi cha kuonewa kwa watu weusi America (kipindi kile ikiitwa New world)
Duh umenichekesha sana kwani watumishi wanamatizo gani mpaka washindwe kuchomoka kwenye kikokotoleo wenyewe bila kusaidiwa na mtu acha wazisome namba za kikokotoleo, Mbona kuna sheria nyingi za kazi mtu alieajiriwa uwezi kunfukuka bila kufata sheria za kazi tofauti na watu wanavyo fikiria awamuhii kila kundi kwenye jamii limewekewa kikokotoleo nani akaangaike kutegua kikokotolea cha mwezeka wakati chakwake kinamshida?
 
Naamini magufuli atayaweka mambo mazuri kwa watumishi,naikumbuka kauli yake siku ya mei mosi kuwa atawaongezea watumishi mishahara kwekikweli,hili bado halijachelewa, watumishi wawe na subira,watumishi ni serikali,hivyo ni lazima muamini kuwa mmehaidiwa, kuhusu swala la kikokotoo,naamini mkiwasilisha kwa raid wetu vizuri, atayaweka vizuri,kiukweli mh rais anafanya mambo makubwa sana kwa maslahi wa Taifa ingawa ni ngumu sana kuiona, 2012 nilipokuwa marekani niliwazia nchi yangu lini tutakuwa na ndege kubwa,Leo hii rais amenunua, transition mnaopitia ni ya muda tu,
ni jukumu la kila mmoja kuisifia nchi yake ndani ya mtandao, ili kuivutia wageni kuingia nchini, nchi ya swarsland watalii walipopungua, raia wema walijitikeza barabarani wakiwapokea wageni wachache wanaoingia kwa kutabasam
nawe tabasamu na nchi yako,mtumishi wa uma wewe ni serikali usiyumbishwe mambo yatakaa vizuri,
Tanzania ni yetu zote na Tanzania itajengwa na sisi
 
Ni rahisi sana kuwatuhumu Watumishi wa umma kuwa ni waoga,wajinga, na kondoo,lakini nani ni kondoo zaidi ya mwingine.Ninyi ambao si watumishi wa umma ambao tangazo la nafasi za kazi za utumishi wa umma zikitolewa mnajaza uwanja wa taifa kwa nafasi 50 tu za kazi,mnashinda njaa mkiwa na bahasha za kaki, vibegi vyenu ili kuutafuta ukondoo,ujinga,upimbi na uoga.Na ninyi mliojiajiri TRA inapowafanya kitu mbaya mmechukua hatua gani zaidi ya kujinyonga na kujipiga risasi,wakulima mazao mnalala nayo na kuishia kujipiga nayo picha huku yakioza mmefanya mnayowashauri watumishi wa umma?.Mlio ajiriwa kwenye mashirika binafsi mnaponyanyaswa huko huwa mnafanya mnayowashuri watumishi wa umma wafanye ili wasiwe makondoo.Kikotoo ni cha wote watumishi wa umma na sekta binafsi mbona ninyi mnataka watumishi wa umma wafanye jambo bila ninyi kuanza kwanza ili watumishi wa umma wawaunge mkono?.
 
Kwaiyo wewe ni mtumishi auni mwenye kikokotoleo?
 
Watumishi wana wawakilishi wao vyama vya wafanyakazi tena wanakatwa malipo ya kuendesha vyama hivyo.Kuna wabunge waliowachaguwa .Je wawakilishi wote hawa kazi yao ni nini? Je wewe mbunge kazi yako ya kumutetea mtumishi munyonge, mpiga kula wako ni kwenda bungeni kusema NDIYO na support motion 100% ya watumishi wapunguziwe mafao yao? from 50% to 25% unasema wapunguziwe?Je nyie viongozi wa vyama vya wafanyakazi inatosha kukaa kimya badala kuendeleza majadiliano na serikali ilegeze msimamo wake.?
 
Mbunge ni mtetezi wa tumbo lake
 
Back
Top Bottom