Kinoamiguu
JF-Expert Member
- Nov 29, 2018
- 10,526
- 13,014
Hawa watu wanashangaza sana, wapo kimya kama hakuna kilichotokea tena wakiendeshwa kwa mikwara ya hali ya juu.
Wengine wamepewa vipande wapande magari ya wenzao bure kisa anawajali? Mbona sio mishahara aliyopandisha? Mmeambiwa haipandii mpaka uzalishaji uongezeke, sijui mwalimu anazalisha nini.
Kutokana na ukimya wenu wamewaletea sheria mpya ya kikotoo cha fao la kustaafu toka 50% mpaka 25% tu na hii ni baada ya manyanyaso kedekede huko nyuma kutoka kwa watawala hawa wenye roho mbaya na viburi utadhani walijichagua.
Najiuliza ukimya huu wa watumishi ni kutojua madhara ya sheria hii amma nì uoga wa kuishi bila vibarua? Awamu zote tumeona watumishi wakienziwa na waligoma.
Mkapa ndiye aliyeinua maslahi ya watumishi hata wakaanza kukopa benki. Kikwete yeye aliongeza maradufu. Lakini huyu anawatukàna hadharani na kutunga sheria mbovu na mpo tu.
Wale wa Kenya juzi walitishia kugoma kisa kuhamishwa nyie mnapelekeshwa tu. Hamna nyongeza, hamna marupurupu, nauli za likizo unadai milioni 1 mtu anakulipa kalaki.
Enyi watumishi amkeni sasa, semeni basi! Ukimya wenu huo mtakuja chapwa bakora mcheke kwa kale kawimbo ka hapa kazi tu