Ukimchunguza Bata hutomla

Ukimchunguza Bata hutomla

mojoki

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
1,313
Reaction score
291
Unamtumia Demu wako Watu wamtongoze eti
ili UMPIME kama kweli ni Maharage ya Mbeya
au Maharage ya Tandika Sokoni...Ubavu
wenyewe wa kumuacha huna Shauri zenu,Mara
umefanya Uspy wako uliyemtuma kazi
akaifanya kwa Umakini mkubwa unakuja
kupewa matokeo kitu Harage la Tukuyu sijui
utafanya niniUkimchunguza sana Bata wala
hutomla,Moyo wa mtu kiza kinene kama hilo
niloliweka hapo..sometimes tunajitakia tu Stress
wenyewe,Mapenziyametufanya tuwe Wajingaaa
If you Dont Trust a Person DONT FALL IN LOVE
WITH HER Mbona rahisi tu,Sasa unamkabidhi
moyo halafu unaanza Ku-Hack Simu
yake,kapigiwa na nani,Saa ngapi,Kwanini,kwa
Sababu gani amekupigia mara 2 kwa siku na
kwanini wanachat,Mara kwenye text 500 why
unapata 30.. HapoHujamuoa na hata Shangazi
zake tu hawakujui Unamlinda utadhani Server
za BOT SASA HIVI TUTAKULAZA WODI YA
VICHAA...Mapenzi hayana uhusiano wowote na
kujiajiri kuwa Usalama wa Taifa.Kumlinda
Mpenzi ni Sawa na kulinda Bahari,Wewe uko
Bize na Mgambo Coco BEach wenzio wanavua
kiulainiiii Ununio Beach


In this world nothing is certain than Tax and Death.
 
Walinzi wanakuja watatueleza kila kitu
 
Kosa la jinai hilo usije thubutu kwanini demu wako umafnyie majaribio kama hayo
 
Ila ni vema ukamchunguza ili ujue unataka kula wa aina gani.
 
Ujana shida sana, haya bhana tumekusikia.
 
Watu mnasema tu hapa, una mke wewe? Unaujua uchungu wake? Eti uje udokezwe mkeo anachepuka utulie tu "useme ukilinda coco beach ununio beach wanavua"...thubutu! Hata kama ubavu sina- tutajua tu huko mbelembele. Nikishindwa si nakaa naye nikijua kuwa ni mchepuko wa watu? Siku ubavu ukirudi anasepa?(Aka Live today die tomorrow or die another day)
Vigezo na masharti ya "cheaters" kuzingatiwa. Makosa yatatozwa

Hapa bata anachunguzwa na analiwa vilevile
 
Kuchunguza sio mbaya ila uwe umejipanga kwa matokeo. Kama kupima ngoma vile. Yakija mabaya uwe tayari kuyapokea na ukijua umeumia utaweza kujipanga namna ya kukabiliana na huo mtihani. Ukiacha mambo yaendelee utajapigiwa hata nyumbani kwako huko mtaani ukipita unajitanua kumbe wazee wakazi wanakuona bonge la ----.
 
Jiwe linatupwa gizani kidizaini

Ila wangu atachunguzwa tu

Bora kufa mapema kuliko kuchelewa kufa
 
Hivi ni nini kikufanye usimchunguze mtu unayetaka kuishi nae au ambae upo nae..labda unaongelea mchepuko ..lkn kama ni mchumba au mke..ntamchunguza sana na baada ya kumchunguza naweka masharti makali mezani..la sivyo mtakuwa mnafanya maigizo..mke/mchumba wangu lazima nijue anaongea na nani, rafiki zake ni nani, kama anatoka au anasafiri lazima nijue anaenda wapi na atafanya nini..na nk...la sivyo mnakuwa mnaigiza tu..
 
IMG-20140303-WA0000.jpg
 
Back
Top Bottom