GENTAMYCINE
JF-Expert Member
- Jul 13, 2013
- 56,747
- 109,201
Sijielewi jamani kwani muda si mrefu nimetoka kuwakaribisha Watu ambao walinitangulia katika Kazi yangu ya Udereva katika DalaDala moja hivi maarufu liitwalo Tanzania Express Coach waje tule wote Chakula na kama ikibidi basi wanipe tu ushauri wao wa namna ambavyo naweza nami nikaliendesha vyema hili Basi kwani ni aina mpya kutoka huko nchini Japan.
Kilichonishtua na kunisikitisha tu ni kwamba hawa Wageni wangu wote niliowaalika hapa Sebuleni Kwangu muda wote walikuwa hawana furaha japo nilijitahidi sana kuwachekesha chekesha ila haikusaidia ndipo nikahisi kuwa huenda nina tatizo kubwa hivyo nilifanyie Kazi upesi nisije nikaliangusha Basi la Watu halafu nikaja kuonekana ni Dereva wa ' hovyo hovyo ' na hisia za hawa Madereva wangu Wakuu walionitangulia zikatimia.
Sasa najiandaa tena kuwaalika hawa hawa Wageni wangu Madereva walionitangulia kuliendesha hili Gari Kubwa la Tanzania Express Coach ili safari hii wakifika tu Sebuleni Kwangu nitawapigia wote magoti ili niwaombe radhi kama kuna popote labda nimewakwaza na kuanzia hapo nitawaahidi kubadilika rasmi ili Udereva wangu usiwe na mashaka na usiingiwe ' Nuksi ' halafu Abiria wangu ama wakanichoka au hata wakaniroga yakanipata makubwa bure!
Nawasilisha.