Ukikaribisha Wageni wako Sebuleni ukaona wamenuna, hawana furaha na wanaogopa jua una tatizo kubwa mno

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,352
108,383
Sijielewi jamani kwani muda si mrefu nimetoka kuwakaribisha Watu ambao walinitangulia katika Kazi yangu ya Udereva katika DalaDala moja hivi maarufu liitwalo Tanzania Express Coach waje tule wote Chakula na kama ikibidi basi wanipe tu ushauri wao wa namna ambavyo naweza nami nikaliendesha vyema hili Basi kwani ni aina mpya kutoka huko nchini Japan.

Kilichonishtua na kunisikitisha tu ni kwamba hawa Wageni wangu wote niliowaalika hapa Sebuleni Kwangu muda wote walikuwa hawana furaha japo nilijitahidi sana kuwachekesha chekesha ila haikusaidia ndipo nikahisi kuwa huenda nina tatizo kubwa hivyo nilifanyie Kazi upesi nisije nikaliangusha Basi la Watu halafu nikaja kuonekana ni Dereva wa ' hovyo hovyo ' na hisia za hawa Madereva wangu Wakuu walionitangulia zikatimia.

Sasa najiandaa tena kuwaalika hawa hawa Wageni wangu Madereva walionitangulia kuliendesha hili Gari Kubwa la Tanzania Express Coach ili safari hii wakifika tu Sebuleni Kwangu nitawapigia wote magoti ili niwaombe radhi kama kuna popote labda nimewakwaza na kuanzia hapo nitawaahidi kubadilika rasmi ili Udereva wangu usiwe na mashaka na usiingiwe ' Nuksi ' halafu Abiria wangu ama wakanichoka au hata wakaniroga yakanipata makubwa bure!

Nawasilisha.
 
Usiwaze sana mkuu kuhusu hilo wape kwanza msosi ukiona bado hali si nzuri basi wafukuze
 
Dereva umekua mkali pia mbabe sana lazima waogope na kutetemeka.Pengine wanahisi umewaalika kuwasanifu kwamba wewe umekua dereva bora kuliko wao ,kazi zote za kwenye basi unafanya wewe kuanzia udereva,ukonda,kupakia na kushusha mizigo hata kukata tiketi.
 
Angalia vizuri katika zile picha za wageni wako kuna picha moja ,kuna baadhi ya Makondakta wa zamani wamekaa nusu kiti. Yaani ni hofu na wasiwasi tupu.
Soma lugha ya picha wanatuma ujumbe gani kwa wewe mwenyeji wao.
 
Shikamoo Mkuu!

Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nijitathmini upya kwanini Wageni wangu jana Sebuleni Kwangu walikuwa wanyonge, kama vile wananiogopa na hawajiamini nami? Lakini tatizo kwani ni nini mbona Mimi naona Udereva wangu ni kama waliokuwa nao Wao tu huko nyuma wakati wakiliendesha hili hili Basi letu la Kampuni liitwalo Tanzania Express Coach? au labda nimezidisha tu ' Manjonjo ' yangu? Watanisamehe tu Mkuu kama wao walikuwa ' Waoga ' kuliendesha hili Gari basi Mimi ndiyo nitaliendesha kwa Spidi hadi ikibidi niende nikawagonge nalo tu Mashangazi na Wajomba zao huko Kijijini ili mradi tu hawa Abiria wangu wasafiri kwa raha, amani na starehe.
 
Ni kweli Mkuu kuna Dereva mmoja Mwandamizi kabisa anatokea Zanzibar alinifundisha sana kutia Gia hili Gari muda wote alikuwa amepinda pinda hivi halafu anatizama tu ' darini ' huku anatetemeka. Alinishtua mno! Hivi Mkuu ni kweli kabisa eti Udereva wangu wa sasa unaweza labda ukanisababishia ajali huko mbeleni? Nilikuwa nami nistaafu hii Kazi mwaka 2025 ila naona bado nina nguvu nguvu hivi hivyo nafikiria tena kuwa Dereva kwa kama miaka Saba ( 7 ) hivi mbele. Sijui nitaweza na Abiria wataniamini!
 
Nakushauri uwe unasikiliza na ushauri wa Abiria wako.
Wasaidizi wako hawakupi taarifa za ukweli au hali halisi ya malalamiko ya abiria.
Ni wanafiki chunga sana.
 
Shikamoo Mkuu!

Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nijitathmini upya kwanini Wageni wangu jana Sebuleni Kwangu walikuwa wanyonge, kama vile wananiogopa na hawajiamini nami? Lakini tatizo kwani ni nini mbona Mimi naona Udereva wangu ni kama waliokuwa nao Wao tu huko nyuma wakati wakiliendesha hili hili Basi letu la Kampuni liitwalo Tanzania Express Coach? au labda nimezidisha tu ' Manjonjo ' yangu? Watanisamehe tu Mkuu kama wao walikuwa ' Waoga ' kuliendesha hili Gari basi Mimi ndiyo nitaliendesha kwa Spidi hadi ikibidi niende nikawagonge nalo tu Mashangazi na Wajomba zao huko Kijijini ili mradi tu hawa Abiria wangu wasafiri kwa raha, amani na starehe.
Mkuu Gentamycin inabidi ujitathmini kweli kwa huu uendeshaji wako wa basi kwa sababu sio tu madereva wastaafu hata abiria nao roho mkononi.Juzi basi limepita mikoa ya kusini abiria ukagoma kuwasimamishia basi ili wapakie viroba vyao vya korosho.Wengine ukagoa kuwarudishia chenji zao na wakapiga kelele ukatishia kuwashusha.

Basi linahitaji service ila hutaki kusikiliza ushauri wa mafundi kwani taa za break haziwaki,wastaafu na abiria wana mashaka kama linaweka kufika stendi kuu ya 020 salama.Nakutakia kila la heri katika safari hii.Punguza spidi kwani njia ina mashimo na matuta mengi,kona kali pamoja na milima.waachie makondakta ,mafundi na wapiga debe wafanye kazi zao na pia wasikilize abiria hata kama sio kwa 100%.
 
hehehe. Sina mchango wowote, lakini nikaona nisipite bila kutia neno
 
Shikamoo Mkuu!

Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nijitathmini upya kwanini Wageni wangu jana Sebuleni Kwangu walikuwa wanyonge, kama vile wananiogopa na hawajiamini nami? Lakini tatizo kwani ni nini mbona Mimi naona Udereva wangu ni kama waliokuwa nao Wao tu huko nyuma wakati wakiliendesha hili hili Basi letu la Kampuni liitwalo Tanzania Express Coach? au labda nimezidisha tu ' Manjonjo ' yangu? Watanisamehe tu Mkuu kama wao walikuwa ' Waoga ' kuliendesha hili Gari basi Mimi ndiyo nitaliendesha kwa Spidi hadi ikibidi niende nikawagonge nalo tu Mashangazi na Wajomba zao huko Kijijini ili mradi tu hawa Abiria wangu wasafiri kwa raha, amani na starehe.
Tatizo lako ni kwamba, wajiona kuwa wewe dereva mzuri kuliko wenzako huko nyuma kitu ambacho si kweli. Vitisho vingi vya nini kama kweli wewe ni dereva mzuri?.Dereva gani mzuri analazimisha kukubalika?.Nigongee shangazi yangu uone kama huo uume wako utafanya kazi. Shabash.
 
Shikamoo Mkuu!

Kwahiyo unataka kuniambia kwamba nijitathmini upya kwanini Wageni wangu jana Sebuleni Kwangu walikuwa wanyonge, kama vile wananiogopa na hawajiamini nami? Lakini tatizo kwani ni nini mbona Mimi naona Udereva wangu ni kama waliokuwa nao Wao tu huko nyuma wakati wakiliendesha hili hili Basi letu la Kampuni liitwalo Tanzania Express Coach? au labda nimezidisha tu ' Manjonjo ' yangu? Watanisamehe tu Mkuu kama wao walikuwa ' Waoga ' kuliendesha hili Gari basi Mimi ndiyo nitaliendesha kwa Spidi hadi ikibidi niende nikawagonge nalo tu Mashangazi na Wajomba zao huko Kijijini ili mradi tu hawa Abiria wangu wasafiri kwa raha, amani na starehe.
Mkuu, tatizo ni kwamba mwendo wako ni rafu sana wanakushangaa jinsi unavyoliendesha hilo basi kwani wenyewe walikuwa hawaliendeshi hivyo.

Pia licha ya abiria kulalamika upunguze mwendo wewe ndo unakanyaga pedal vizuri. Kiukweli wanamashaka sana na udereva wako licha ya stori nzuri unazowapatia.
 
Sijielewi jamani kwani muda si mrefu nimetoka kuwakaribisha Watu ambao walinitangulia katika Kazi yangu ya Udereva katika DalaDala moja hivi maarufu liitwalo Tanzania Express Coach waje tule wote Chakula na kama ikibidi basi wanipe tu ushauri wao wa namna ambavyo naweza nami nikaliendesha vyema hili Basi kwani ni aina mpya kutoka huko nchini Japan.

Kilichonishtua na kunisikitisha tu ni kwamba hawa Wageni wangu wote niliowaalika hapa Sebuleni Kwangu muda wote walikuwa hawana furaha japo nilijitahidi sana kuwachekesha chekesha ila haikusaidia ndipo nikahisi kuwa huenda nina tatizo kubwa hivyo nilifanyie Kazi upesi nisije nikaliangusha Basi la Watu halafu nikaja kuonekana ni Dereva wa ' hovyo hovyo ' na hisia za hawa Madereva wangu Wakuu walionitangulia zikatimia.

Sasa najiandaa tena kuwaalika hawa hawa Wageni wangu Madereva walionitangulia kuliendesha hili Gari Kubwa la Tanzania Express Coach ili safari hii wakifika tu Sebuleni Kwangu nitawapigia wote magoti ili niwaombe radhi kama kuna popote labda nimewakwaza na kuanzia hapo nitawaahidi kubadilika rasmi ili Udereva wangu usiwe na mashaka na usiingiwe ' Nuksi ' halafu Abiria wangu ama wakanichoka au hata wakaniroga yakanipata makubwa bure!

Nawasilisha.
 
Sijielewi jamani kwani muda si mrefu nimetoka kuwakaribisha Watu ambao walinitangulia katika Kazi yangu ya Udereva katika DalaDala moja hivi maarufu liitwalo Tanzania Express Coach waje tule wote Chakula na kama ikibidi basi wanipe tu ushauri wao wa namna ambavyo naweza nami nikaliendesha vyema hili Basi kwani ni aina mpya kutoka huko nchini Japan.

Kilichonishtua na kunisikitisha tu ni kwamba hawa Wageni wangu wote niliowaalika hapa Sebuleni Kwangu muda wote walikuwa hawana furaha japo nilijitahidi sana kuwachekesha chekesha ila haikusaidia ndipo nikahisi kuwa huenda nina tatizo kubwa hivyo nilifanyie Kazi upesi nisije nikaliangusha Basi la Watu halafu nikaja kuonekana ni Dereva wa ' hovyo hovyo ' na hisia za hawa Madereva wangu Wakuu walionitangulia zikatimia.

Sasa najiandaa tena kuwaalika hawa hawa Wageni wangu Madereva walionitangulia kuliendesha hili Gari Kubwa la Tanzania Express Coach ili safari hii wakifika tu Sebuleni Kwangu nitawapigia wote magoti ili niwaombe radhi kama kuna popote labda nimewakwaza na kuanzia hapo nitawaahidi kubadilika rasmi ili Udereva wangu usiwe na mashaka na usiingiwe ' Nuksi ' halafu Abiria wangu ama wakanichoka au hata wakaniroga yakanipata makubwa bure!

Nawasilisha.
Kuwapigia magoti tena? unamaanisha unakiri wazi wazi kuwa basi unaweza kulitupa bonden!!? Lakini si vyema kumsemea anayejiona yupo sawa, namaanisha dereva wetu bora wa Tanzania coach hii.
 
Wanakushangaa dereva wa ovyo lakini kwa muda mfupi umenunua makochi na tiivii huku abiria wakilalamika kwa udereva mbovu. Umesababisha ajali na vifo lkn hujali. Hufungi mkanda na hufungi vigungo bya uniform hata zipu hufungi. Yaani wewe usukani haukufai wewe hata ukonda huwezi labda uwe tingo wa gari la taka.
 
Back
Top Bottom