Ukihisi una Corona ufanyeje?

Ukihisi una Corona ufanyeje?

Masokotz

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2018
Posts
3,832
Reaction score
6,467
Hili ni swali ambalo najua kuna ambao wanajiuliza pia.

Kwa jinsi hali ilivyo na namna jambo hili linavyoshughuikiwa hapa nchini wengi watakuwa wanajiuliza swali hili kwa hofu kubwa na mashaka.

Sababu za mashaka ni ukweli kwamba wengi wameshaona kwamba kupata CORONA ni sawa na KIFO na kwa jinsi ambavyo imethibitika pasi na shaka kwamba mfumo wetu wa afya ni mbovu basi wengi wana hofu kubwa kwa kutokujua cha kufanya.

Le nataka tujadili kwa kina nini cha kufanya iwapo unahisi kwamba una maradhi haya.
  1. Hatua ya kwanza ni kuwajulisha watu wako wa karibu juu ya wasi wasi wako na kwamba ungependa sasa Ujitenge nao na kuwa peke yako na huku ukiwasihi na wao wajitenge na watu wengine na kujitenga baina yao-SOCIAL distancing
  2. Hatua ya pili ni kuzitazama dalili ulizo nazo.Kulingana na dalili ulizo nazo unaweza kuamua aina ya tiba.Kumbuka katika kipindi hiki kinga yako ya mwili lazima iwe imara hivyo basi kula vyakula vyenye kuongeza kinga mwili huku ukkitumia muda mwingi kupumzika na iwpo una dalili kama vile homa,mafua,kikohozi basi tumia dawa za kutibu dalii hizo kama vile -Anti cough syrup,Anti allergy,pain killers kama panadol n.k.
  3. Hatu ya tatu ni iwapo unaona dalili zinakuwa kali basi toa taarifa kwa kituo cha dharura ya Korona waje kukuchukua.Iwapo hawatakuja endelea kukaa hapo na usijaribu kujichanganya na watu ili kufika hospitali kwani utasambaza maambukizi.
Unachopaswa kutambua ni kwamba CORONA kwa sasa haina dawa na kwamba kama ikikushika vibaya kwa hakika utakufa.Unaweza kutumia muda huo wa kusubiri kufa kuandika wosia,kutubia dhambi zako na kuweka mambo yako sawa na muumba wako.Usiogope JILINDE na UWALINDE WENZAKE

NB.KUWA MAKINI SIO KILA HOMA NI CORONA-Vipimo viko DAR ES SALAAM TU kwa hivyo inahitaji uvumilivukuthibitisha iwapo una korona ila ili ujisaidi basi kila unapokuwa na homa basi fikiri kwamba ni korona na uchukue hatua ya kuzuia maambukizi ya ziada
 
Bila kusubiri dalili, mimi nimeongeza ulaji wa limao kila siku asubuhi na kuwa sehemu ya kuyapa maji ladha kwa siku kutwa. Jioni mlo wangu lazima kuwepo mboga za majani, na dessert yangu ni tangawizi kali iliyochemshwa na limao.

Tahadhari nyingine kama kukaa mbali na watu, kunawa mikono mara kwa mara, kutopeleka mikono kinywani, puani au machoni na kuvaa mask hizo nazizingatia pia.

Tusisubiri dalili maana dalili zikija unaweza kuingiwa na woga; tuongezee miili yetu kinga iwe tayari kwa mashambulizi na huyo adui kama akipenya.
 
Hili ni swali ambalo najua kuna ambao wanajiuliza pia.

Kwa jinsi hali ilivyo na namna jambo hili linavyoshughuikiwa hapa nchini wengi watakuwa wanajiuliza swali hili kwa hofu kubwa na mashaka.

Sababu za mashaka ni ukweli kwamba wengi wameshaona kwamba kupata CORONA ni sawa na KIFO na kwa jinsi ambavyo imethibitika pasi na shaka kwamba mfumo wetu wa afya ni mbovu basi wengi wana hofu kubwa kwa kutokujua cha kufanya.

Le nataka tujadili kwa kina nini cha kufanya iwapo unahisi kwamba una maradhi haya.
  1. Hatua ya kwanza ni kuwajulisha watu wako wa karibu juu ya wasi wasi wako na kwamba ungependa sasa Ujitenge nao na kuwa peke yako na huku ukiwasihi na wao wajitenge na watu wengine na kujitenga baina yao-SOCIAL distancing
  2. Hatua ya pili ni kuzitazama dalili ulizo nazo.Kulingana na dalili ulizo nazo unaweza kuamua aina ya tiba.Kumbuka katika kipindi hiki kinga yako ya mwili lazima iwe imara hivyo basi kula vyakula vyenye kuongeza kinga mwili huku ukkitumia muda mwingi kupumzika na iwpo una dalili kama vile homa,mafua,kikohozi basi tumia dawa za kutibu dalii hizo kama vile -Anti cough syrup,Anti allergy,pain killers kama panadol n.k.
  3. Hatu ya tatu ni iwapo unaona dalili zinakuwa kali basi toa taarifa kwa kituo cha dharura ya Korona waje kukuchukua.Iwapo hawatakuja endelea kukaa hapo na usijaribu kujichanganya na watu ili kufika hospitali kwani utasambaza maambukizi.
Unachopaswa kutambua ni kwamba CORONA kwa sasa haina dawa na kwamba kama ikikushika vibaya kwa hakika utakufa.Unaweza kutumia muda huo wa kusubiri kufa kuandika wosia,kutubia dhambi zako na kuweka mambo yako sawa na muumba wako.Usiogope JILINDE na UWALINDE WENZAKE

NB.KUWA MAKINI SIO KILA HOMA NI CORONA-Vipimo viko DAR ES SALAAM TU kwa hivyo inahitaji uvumilivukuthibitisha iwapo una korona ila ili ujisaidi basi kila unapokuwa na homa basi fikiri kwamba ni korona na uchukue hatua ya kuzuia maambukizi ya ziada
hii kitu naona mama kawa mkimya sana sasa hivi hatupatii update kabisaaa ama sijui ndio anaogopa kutuongezea hofu

na raia naona wanaamini kuwa hatuna maambukizi ama wanahisi tatizo limekwisha wanajiachia tu misikitini makanisani mitaani tahadhari haizingatiwi tena ila kwa watu wachache sana

naona hili litazidi kusababisha kuenea kwa maambukizi ni vizuri aendelee kutupatia update tukiona idadi inavyopanda tutaongeza kuchukua tahadhari kuliko hivi alivyoamua kubaki kimya ama ndio kusema hatuna maambukizi mapya?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom