Ukienda ugenini Kuna vitoto vinapenda sana sifa

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
5,950
23,263
Nimekuja mkoani kumtembelea bradha. Kuna mzigo aliniagiza nimletee. Hapa kwa bro kuna mtoto wao wa kiume ana umri kama miaka minne au tano hivi. Asee, hiki kitoto ni kitundu sijapata ona. Mbaya zaidi, babaake na mama yake wanamlea kama yai, full kudeka-deka hovyo.

Sasa ni heri wangekuwa wanamlea hovyo, akawa anawasumbua wenyewe ingekuwa hakuna shida, ila akiwa na wenzake ni kakorofi, kanawapiga wenzake. Nimejilipua zangu fulana kutoka kwa vunja bei. Ameshaitanua shingo kwa kunivuta-vuta. Imekuwa kama nanyonyesha sasa. Mara aninyang'anye simu, mara aniparamie usoni kama mbwa, alafu ana vikucha vikali.

Basi naishia kujichekesha chekesha tu mbele ya mama yake. Maisha ya ugenini yana unafiki sana. Wazazi wake wala hawastuki, wanaona poa tu mtoto wao anavyo act kama kingedere. Mamaake ananiambia 'shemeji kama junia anakusumbua mchape.' Namchapaje mtoto wa watu ugenini? Kwa nini asimkataze kusumbua wageni na kukachapa kakiendelea kuleta ubishi.

Sasa mamaake akaenda dukani akaniacha na junia tunavutana-vutana. Happy ndiyo nikambadikilia, nikamwonyesha sura ya ukauzu na kumtoa shingoni maana ilikuwa kama ananidai kwa jinsi alivyokuwa ananikaba. Nikakashika mikono na kukaminya tu vidole vyake kama naminya karanga, huku namwambi acha utundu kwa wageni mtoto. Kakaanza kulia kanaelekea dukani kwa mamaake.

Maisha ya ugenini magumu sana. Nilipanga kukaa siku mbili, ila moja tu inatosha kwa kweli. Wazazi wengine hivi mnaleaje watoto kipuuzi kama hivi? Katoto ni ka-attention seeker. Mpo katika maongezi sebuleni, kenyewe kanapita-pita na kuvuta watu nguo, ili mradi tu kaonekane kapo live. Mkikapotezea, kataangusha hata glass!
 
Fanya shambulizi la kimya kimya hakuna haja ya kushika fimbo.
Shika mkono vizuri kwenye msuli(hawezi kua na msuli) binya na dole gumba kwa nguvu kiasi utakutana na mfupa, kandamiza kama sekunde 10 hivi uone kama katarudia
Looh! Ukatili gani huo?
Akimtia ulemavu mtoto!?
Nyie wanaume mnashida gani lakini? Mbona mnakua makatili kila sehemu!
 
UKILAZIMIKA kwenda ugenini ni kuingia usiku kutoka alfajiri(uwe na timing nzuri sio watu wamelela unaleta vidole vyako kama mafungu ya tangawizi)

Hata kama huna cha kufanya(na kama huna umeenda kufanyaje)? Bora uzuge nje sio kukaa ndani na wakati stori hamna.

NB ni rahisi sana kuona mtoto wa mwenzako ndio hana adabu.
 
Kwa kuvunja mayai ndio usiseme

FlKnauaXgAElwiO.jpeg
 
Hawa watoto watukutu kwa wageni ni kutokana na malezi ya wazazi wao. Kikawaida mtoto anatakiwa aonywe na mzazi wake asizoee wageni. Unatakuta umetengewa chakula safi cheupe, sembe au wali kanakuja katoto kanachafuachafua kwa kupakaza mchuzi kila sehemu. Mbaya zaidi kanachukua paja la kuku ulilotengewa.

Kuna kengine kalinitea usumbufu nikachoka kukukavumilia ikabidi nikakunjie mdomo, ile nakuna mdomo mama yake akaniona akaanza kunipa makavu kuwa nina chuki na mwanae, tukazozana sana. Enzi zetu hatukuruhusiwa kuwa karibu na mgeni hasa wakati wa kula ukijipitisha ili ukaribishwe ule adhabu utaipata mgeni akiondoka. Nidhamu kwa wageni ilijengwa tangu tukiwa watoto wadogo
 
Back
Top Bottom