GE2025 Ukibadilisha jina baada ya kujiandikisha, bado una haki ya kupiga kura, vijana mshiriki kwa wingi kwenye uchaguzi

GE2025 Ukibadilisha jina baada ya kujiandikisha, bado una haki ya kupiga kura, vijana mshiriki kwa wingi kwenye uchaguzi

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,439
Reaction score
6,692
Wakuu,

Kama swali linavyojieleza hapo juu

Yaani kwa mfano mimi naitwa XYZ muda wa kujiandikisha alafu miezi michache baadae nikabadilisha jina langu kuwa XYS je ina maana nimepoteza haki yangu ya kupiga kura kwa kuwa jina langu limebadilika?

Sasa ukweli ulivyo ni kwamba sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024 inaeleza “Mtu aliyeandikishwa kuwa Mpiga Kura ambaye jina lake limebadilika kutokana na ndoa au kwa sababu nyingine yoyote baada ya kuandikishwa, iwapo hajapoteza sifa za kupiga kura chini ya kifungu cha 14, atastahili kupiga kura kwa jina ambalo ameandikishwa.”

Hiyo ni kwa mujibu wa Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani ya Mwaka 2024, inayotumika upande wa Tanzania Bara na Zanzibar kwa Uchaguzi wa Rais na Wabunge wa Jamhuri ya Muungano, na kwa uchaguzi wa Madiwani kwa Tanzania Bara.
 
Huna kitambulisho cha mpiga kura?Kama unacho ndicho utatumia.Jina hilo ndilo utakalotumia na ndilo litatokea kwenye orodha ya wapiga kura.
 
Mkuu Kwa hiyo baba levo ni disqualified. Nasikia kabadili jina lake anataka asomeke BABA LEVO kwenye karatasi za kura
 
Back
Top Bottom