UKAWA watofautiana bungeni

UKAWA watofautiana bungeni

Joined
Jun 8, 2016
Posts
59
Reaction score
31
KWANINI WABUNGE WA UKAWA WALITOFAUTIANA NA KUONEKANA WAKILUMBANA KWA MUDA KABLA YA KUTOKA NJE YA BUNGE?
Kazi ipo mwaka huu, SISI YETU MACHO TU
 
Mie sikuwa karibu na tiviii hata sijui, ngoja nisubirie kudesa kwa wenzangu watakapotoa maoni yao
 
Kwanini wabunge wa UKAWA walitofautiana na kuonekana wakilumbana kwa muda kabla ya kutoka nje ya bunge?

Karibuni sana.
ungetuambia walichokuwa wanalumbania,sasa unatuuliza sisi tuseme nini??mnazidi kukosa cha kuandika.bado kukimbia tu humu.aibu sana
 
Baadhi ya watu humu wanatamani UKAWA warudi bungeni bila kuelewa wala kuzingatia msingi wa hoja zao,sasa wanapost hisia kuliko uhalisia
 
Acha uzushi ww ..mi nimeangalia hakukuwa na malumbano yyte ..wametoka kiustaarabu kabsa
Huenda huyu muungwana aliangalia tukio hilo akiwa ndani ya bunge, ila tulioangalia kupitia bunge Tv tuliona Mbowe akianza safari. Hata hivyo wakati wanawaonesha wengi walikuwa wanatazamana kama kutaka kujua nini cha kufanya.
 
Baadhi ya watu humu wanatamani UKAWA warudi bungeni bila kuelewa wala kuzingatia msingi wa hoja zao,sasa wanapost hisia kuliko uhalisia
Ukawa wenyewe wanatamani kurudi bungeni ika wanaona aibu wanasubiri kubembelezwa...
 
Huenda huyu muungwana aliangalia tukio hilo akiwa ndani ya bunge, ila tulioangalia kupitia bunge Tv tuliona Mbowe akianza safari. Hata hivyo wakati wanawaonesha wengi walikuwa wanatazamana kama kutaka kujua nini cha kufanya.
NDUGU UKO VIZURI SANA....
JARIBU KUWAELIMISHA NA HAO WANACHAMA HEWA WA UKEWENZA
 
Huenda huyu muungwana aliangalia tukio hilo akiwa ndani ya bunge, ila tulioangalia kupitia bunge Tv tuliona Mbowe akianza safari. Hata hivyo wakati wanawaonesha wengi walikuwa wanatazamana kama kutaka kujua nini cha kufanya.
Nani ambaye alipaswa kuwa na uelewa zaidi juu ya kilichokuwa kikiendelea bungeni; ni yule aliyekuwa ndani, yule ambaye alitazama bunge kupitia bunge tv kama unavyodai, au aliyekuwa kazini kuitikia wito wa serikali wa kutoangalia bunge live ili kuunga mkono 'hapa kazi tu'? Hebu tuwekee hiyo clip hapa tuone huko kutazamana ambako wewe umehitimisha kuwa maana yake ni kutaka kujua nini cha kufanya!
 
Baadhi ya watu humu wanatamani UKAWA warudi bungeni bila kuelewa wala kuzingatia msingi wa hoja zao,sasa wanapost hisia kuliko uhalisia
wacha watoke. serikali ya jpm imekumbatia maslahi ya umma hata bunge lote likitoka hakuna shida. wabunge wa ccm pia wengi ni tumbombele ila ukawa wengi pia ni nyumbu.
 
Sio siri mvutano ni mkubwa. Wako wanaoona kupelekwa kama walevi na wanaoona ni poa tu maana akili zao wamesalimisha kwa Mr. Zero watazirejea bunge lijalo.
 
Nani ambaye alipaswa kuwa na uelewa zaidi juu ya kilichokuwa kikiendelea bungeni; ni yule aliyekuwa ndani, yule ambaye alitazama bunge kupitia bunge tv kama unavyodai, au aliyekuwa kazini kuitikia wito wa serikali wa kutoangalia bunge live ili kuunga mkono 'hapa kazi tu'? Hebu tuwekee hiyo clip hapa tuone huko kutazamana ambako wewe umehitimisha kuwa maana yake ni kutaka kujua nini cha kufanya!
Aliyekuwa ndani anayonafasi nzuri ya kujua kilichoendelea mle ndani kuliko anayeangalia kupitia bunge Tv. Huwa sina kihelehele cha kuchukua clip za bunge mara kwa mara. Huchukuwa pale nionapo tukio la kunifurahisha mimi kwa ajili ya kumbukumbu. Hili halikuwa tukio muhimu kwangu.
 
Back
Top Bottom