Tafadhali embu tuambiane ukweli taifa hili ili lisonge linahitaji ukweli.
Naomba tujadili kwa uwazi na ukweli ni wapi UKAWA walipokosea na kupatia katika harakati za kuandaa katiba mpya?
Kwanza ni kususia bunge kwa sababu ya kipengele kimoja tu cha muundo wa serikali ambacho hata hivyo hata kura kilikuwa hakijapigiwa.Utasusaje kitu ambacho hata conclussion haijafikiwa?Ukiliwauliza hizo serikali mbili au tatu au moja zimeshajadiliwa na kupigiwa kura jibu ni hakuna.Hivyo UKAWA wako nje kwa hoja hewa.
Pili UKAWA wanajionyesha kuwa ni wabunge wa wale laki tatu tu waliofikiwa na tume ya warioba.Watanzania wengine mamilioni ambao hawakufikiwa ambao wana mawazo mazuri tu wao kama wabunge wao ilibidi wayachukue maoni ya hao ambao tume haikuwafikia na waende na maoni hayo na kuyatumia katika mijadala ili kama yakionekana nayo yafaa yaingizwe kwenye rasimu.Kukataa UKAWA kuingia bungeni wamewanyima watu wengi ambao tume haikuwafikia kufikisha mawazo yao kupitia kwao,Ndio maana bunge la katiba la sasa kwa kuona umuhimu huo limetoa muda hadi august 27 wale wananchi ambao hawakufkiwa na tume ya warioba na walikuwa na maoni yao ambayo wanaona kwenye rasimu hayamo basi wayafikishe bungeni.UKAWA kuwa wabeba maoni ya watoa maoni laki tatu tu si sahihi kwao nadhani hawaelewi maana kuwa mbunge ni nini.
Tatu UKAWA hawaelewi kuwa bunge la katiba halina chama kule ni kuwakilisha wananchi tu na si vyama.Lakini UKAWA wameenda kule na kuunda Chama kipya kinachoitwa UKAWA ambacho ni muungano wa vyama vya siasa.Wajue wao kuwa waliowapa kura si watu wa vyama vyao tu,Na waliwapa hizo kura si kwa sababu wanavipenda sana hivyo vyama la.Waliwapa kura kwa kuwa waliwaona wana uwezo.Sasa kugoma wanawavunja moyo watu wasio wanachama wa vyama vyao waliowapa kura.
Nne juzi juzi tu tumeona tume ya warioba ikipeleka maoni mapya kuwa yalisahaulika kuwekwa.Yaani tume yenyewe inaona kuwa hiyo rasimu bado inahitaji msasa.Ajabu UKAWA hawalioni hilo ambalo hata tume imeliona?
Tano UKAWA hawaelewi hata wakiongea waongee na nani.nilisoma gazeti la mwananchi Maalimu SEIF akizungumza na waandishi wa mwananchi kuwa Uraisi kwenye katiba uwe wa kupokezana kwa zamu kati ya Tanzania bara na zanzibar.Sheria ya kuongea jambo ni kuwa inabidi kuongea na AUDIENCE husika.Hilo la kupokezana uraisi mahali pa kuliongelea na kulijadili ni bunge la katiba.Sasa UKAWA kawagomesha wasiende bungeni huku nje yuko na waandishi wa habari akitaka mambo ya kuppokezana madaraka yawekwe kwenye katiba.Hao waandishi maskini watamsaidiaje?Hawana nguvu ya kuandika katiba wenye nguvu ni hao wabunge wa UKAWA.Hayo maneno alitakiwa awambie wabunge wake ili wayajadili bungeni.Lakini katoa macho anafoka ole wake mbunge mwana CUF atakayeenda bungeni huku anataka la kupokezana madaraka liwemo.A big paradox to a leader like him.Anyway UKAWA hawajitambui lakini kadri muda unavyoenda watajiona si tu kuwa walikosea lakini pia wataaibika mbele ya jamii kwa kususa kwao
Sita UKAWA kama wanasiasa mahiri walitakiwa waende mahakamani mapema ili kuomba tafsiri ya kazi la bunge la katiba kabla ya kususia ili wawe na strong ground ya kususa inayotambuliwa hata kisheria.Hawakwenda sasa hivi individuals ambao si wanasiasa wameenda kuomba tafsiri.Sasa mathalani tafsiri ikitolewa kuwa bunge linaloendelea liko sahihi na wagomaji hawako sahihi kisheria hivi UKAWA watajificha wapi na hizo nyuso zao.Nilidhani mgomo wao ungekuwa na nguvu ya kisheria ungekuwa wa maana na wananchi wangwaelewa.Lakini kugoma kwao kwenda mahakamani kuomba tafsiri ya kazi ya hilo bunge kumewashusha hadhi sana mbele ya wasomi,wanasheria na watu wapenda mambo kwenda kwa mipangilio.
Saba UKAWA wanashupalia sana muundo wa serikali na mgawanyo wa madaraka na mapato sababu wana hamu sana ya madaraka kwao hoja zingine hazina maana cha maana ni hicho tu cha mgawanyo wa serikali,madaraka na mapato hayo mengine kwao wanaona ni upuuzi .UKAWA hawako sahihi waanze na mambo ya wananchi kwanza hayo ya idadi za serikali nani anakuwa na cheo gani katika serikali na anapata nini yangekuwa hata baadaye.Kusema lazima waanze na hilo uroho wao wa madaraka unaonekana wazi.Ni kama wanasema hatutajadili mambo mengine yeyote hadi tujue mtatupa nini kwenye bahsha zetu kama mshiko.
Matatizo ya wananchi wangeyaweka mbele na hayo ya madaraka yaje baadaye wangeonekana wazalendo zaidi.