UKAWA Wanatumiwa Kuleta Machafuko


WAJINGA ndiyo waliwao, wabunge wa UKAWA wanapata huo mgao au ni viongozi peke yao ndiyo wanalamba?
 

Umeshaambiwa UKAWA wanafadhiliwa na Uholanzi na oman, haya na wewe pika uzushi wako, CCM wanafadhiliwa na nani?
 
CCM hawakudhani kuna siku CUF na CDM wanaweza kukaa meza moja na kuungana!! kweli hii ndiyo dawa ya hawa wababaishaji wa Lumumba - Tumewashika.

UKAWA mpango mzima!! UKAWA habari ya mujini.
 
Wakamatwe kama uzi huu ni waukweli na mtoa uzi naye anaswe alete vielelezo
 
Huyo Agustino Matefu kama amesema haya nje ya bunge kwa nini asishtakiwe mahakamani?
 
Kama wafadhili wanatoa fedha kutetea maoni ya wananchi kuna ubaya gani? Huyo anayepinga maoni ya wananchi ana ajenda gani zaidi ya kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumiwa kwa maslahi ya wageni na CCM? Wafadhili please ongezeni misaada kwa watetezi wa maoni ya wananchi.
 
AO WATU WA NJE (oman & uholanzi) WANATUVURUGA VIPI ? Kwani MADAI YA UKAWA NI NINI? Na pili watu kupewa pesa ndo kiashiriano cha kwamba tunavurugwa mbona ata mimi HUPEWA PESA NA BABA KWA AJILI YA MATUMIZI YANGU BINAFSI LAKINI PIA KAKA/MJOMBA/RAFIKI HUNIPA PIA je io inadhihirisha kua huvuruga familia yetu?


EMU FIKIRI KWA UMAKINI AFU NDIO USEME TENA
 
hata shetani akisaidia kuyatoa mapepo (CCM) nitampongeza
 
Uholanzi na Oman waivuruge Tanzania ili wanufaike na nini?..mawazo yakipumbav kweli!
 
Jamaa wa tz 01 anatafuta umaarufu tu ni kumpotezea
 
Jamani mnisaidie pengine mi macho yangu. Awamu ya kwanza wametoa sh 1,700,000......Uholanzi watoe mil moja na laki saba..........mbona kama vihela kiduchu sana.......huu uongo haukupangwa vizuri.
 
Ungetuwekea ushahidi wa hizo transaction tungeamini lakini maneno matupu ni BURE, kuingiziwa Millioni moja na laki saba ndizo zisaidie kuvuruga Katiba!!!Lete Data kamili unaweza ukatushawishi. Harafu serikali iko wapi? Polisi wako wapi? Usalama wa Taifa wako wapi? DHAIFU!!!
 
kadanganye wa kwenu

Akadanganye wa kwao wapi kwani hata wanamtambua?.Kama nilivyosema bado hawa wazee wanadhani wanaweza kufikiri kwa niaba ya vijana ambao ni asilimia 65 ya wananchi wa taifa hili.Wanajidanganya wanaoelewa taratibu za benki kuu kuruhusu fedha za nje kuingizwa nchini tena kwenye akaunti ya mtu ni wao tu.Aelezwe siku hizi kuna mitandao na teknologia ya kisasa kila kitu kiko wazi kwa yeyote kujua sio wakati wao wa typewritter,simu za kuzungusha na landrover za kuwasha kwa hendeli. Hii ndio taarifa kwa umma baada ya siku saba kumalizika? Tunachotaka ni katiba itakayokubalika na wengi na si taarifa za nani kapokea nini. Kwani umoja wao ulipewa na madaraka ya vyombo kama usalalma wa taifa na benki kuu?Kwa hiyo tutegemee raisi atakapokutana na wapinzani atahoji na hilo la kupokea fedha? Yeye Matafu atakuwepo ikulu atoe ufafanuzi wa hilo?
 

Huu ni uongo. Kwamba huyo anaefadhili ndo aliwaambia CCM wajadili Rasimu3 iliyosukwa kusikoeleweka. Muundo wq S2 haumo ndani ya Rasimu2 kama wangeamua kuukataa kwanza kwa kura za siri za kila mmoja
 
Mwambieni haya awaambie watu wenye IQ ndogo kama yake, hii habari siyo size yetu sisi wenye kujitambua, sisi tuna-deal na mambo makubwa na genuine kwa Taifa, sasa huu udhaifu wa serikali yanu na vyombo vya dola mnatueleza sisi tufanye nini?
 
Haya ndiyo matatizo ya kuishi Tanzania huku akili zako na fikra zako zikiwa zimeolewa na wazungu.Kwamba watanzania hawawezi kuwachangia UKAWA mpaka wachangiwe na wazungu?Kwamba watanzania hawawezi wakafanikiwa mpaka wasaidiwe na nchi za nje?Kwamba hakuna jambo jema linalo weza kufanywa na wananchi bila kusaidiwa na wazungu?Kwamba watanzania hawawezi kutumia haki yao ya kuandamana kwa ajili ya kupinga maovu yanayo fanywa na serekali iliyoko madarakani mpaka watumiwe na wazungu?.Kwamba watanzania wenyewe wamejiwekea haki ya kuandamana lakini hawawezi kuandamana mpaka watumiwe na wazungu?.Hii ina onyesha ni jinsi gani ambavyo viongozi wengi wa CCM walivyojaa uongo wa kuwadanganya wananchi kuwa hakuna jambo jema linalo weza kufanywa na wanao tofautiana nao kimtazamo pasipo kutumiwa na wazungu.Ndiyo maana nchi imekuwa na deni kubwa kwa sababu CCM walipo kuwa wanatekereza sera yao ya uwekezaji walijikuta wamewekeza na akili zao kwa wazungu,Wakati wanabinafsisha mashirika ya serekali kwa wazungu wakajikuta wamebinafsisha na akili zao kwa wazungu.Sasa kila kitu ni mzungu,mzungu,Haki ya kuandamana mzungu,UKAWA mzungu,Kuendesha nchi haiwezekani mpaka ukakope kwa mzungu.Hii ndiyo CCM ya wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…