Mwenyekiti wa Tanzania Kwanza ambao ni umoja wa muungano wa vyama saba vya siasa ikiwamo CCM katika bunge maalum la katiba Ndugu.Agustino Matefu amesema leo kuwa UKAWA inatumiwa ili kuleta machafuko na kuvuruga amani ya nchi.
Mwenyekiti huyo ameeleza hayo katika mohojiano kama mgeni katika kituo cha matangazo cha UHURU Fm.Matefu amesema kuwa nchi za uholanzi na Omani zimekuwa zikitumika kufadhili shughuli mbalimbali za UKAWA kwa kutoka pesa ambazo zimekuwa zukiingizwa katika akaunti binafsi za viongozi wa umoja huo.
Amesema kuwa Mbowe na Slaa mpaka sasa kupitia akaunti zao binafsi wameshapokea kiasi cha Sh.1,700,000(Awamu ya kwanza) huku awamu ya pili na tatu jumla ikiwa ni Dola 850,000/=kutoka Uholanzi.Wakati kwa upande wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba kupitia akaunti yake binafsi amepokea kiasi cha dola 400,000/=kutoka Oman.
Ndugu Matefu ameeleza kuwa viongozi wa UKAWA wanatumika kama kijiko kwa manufaa ya watu wengine nje ya nchi kutaka kutuvuruga. Amesema kuwa Umoja huo hauna lengo zuri na nchi hii ndiyo maana pamoja na vikao vyote vyama usuluhishi bado wameendelea kuwa wagumu hawataki kumsikiliza yeyote.
Awali kabla ya hapo Ndugu Matefu kupitia umoja huyo alishazungumza na waandishi wa habari kuwaagiza Viongozi wa UKAWA ndani ya siku Saba wewe wamerudi Bungeni vinginevyo atamwaga Siri nzito zilizojificha nyuma ya Muungani humo.
Tanzania Kwanza ukiwa ni muungano wa vyama saba vya siasa katika Bunge la Katiba unajitambulisha kuwa ni umoja unaotetea maslahi ya nchi,kujali utaifa na kuangalia kwanza masuala muhimu ya kitaifa bila kujali tofauti zao kichama,kisera,kimtazamo na kiitikadi.
WAJINGA ndiyo waliwao, wabunge wa UKAWA wanapata huo mgao au ni viongozi peke yao ndiyo wanalamba?