UKAWA wanapambana vita waliyoshindwa!

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,171
23,991
A Chinese military general, strategist and philosopher, Sun Tzu once said, If you know the enemy and know yourself, you need not fear the result of a hundred battles. If you know yourself but not the enemy, for every victory gained you will also suffer a defeat. If you know neither the enemy nor yourself, you will succumb in every battle.

Kinachoendelea ndani ya bunge kati ya Naibu Spika, Dkt. Tulia na UKAWA ni ishara kuwa UKAWA wanapambana pambano la kisiasa ambalo hawawezi kushinda.

UKAWA wameendelea kutotumia historia kama mwalimu katika kufanya maamuzi yao ya baadaye.

Kilichotokea kwenye Bunge la Katiba lilikuwa ni somo mbadala ambalo lingewafanya UKAWA kutofanya tena makosa yaleyale yanayohusiana na athari za mashambulizi kutoka kambi ya wabunge wa CCM.

CCM wanafahamu vizuri udhaifu wa Kambi ya UKAWA. CCM wanafahamu vizuri kuwa kama unataka UKAWA watoe maamuzi yenye jazba na yasiyo na manufaa kwa mstakabali wa maisha yao ya kisiasa basi unachotakiwa ni kuwatia hasira za kisiasa( provoke) kwa njia yoyote ile na kama ukifanya hivyo kuna uwezekano mkubwa wakatoa maamuzi ambayo hayatakuwa na manufaa yao kwa kipindi kirefu.

Leo tunashuhudia UKAWA wameamua kutoingia bungeni wakati nguvu za kanuni za bunge haziko upande wao ili kuzuia mijadala ya bunge.

Walichofanya UKAWA ni kama kucheza kamali huku wakitegemea hisani ya CCM ili kamali yao washinde, mbaya zaidi wanawazodoa kisiasa hao watoa hisani.

UKAWA wanatoa maamuzi ya kibunge kama vile hawafahamu historia na taratibu za uendeshaji wa mabunge ya jumuiya ya madola (CPA). Kwa taratibu za party caucus hakuna mbunge wa CCM atakaye mwondoa Dkt. Tulia Ackson katika kiti cha Naibu Spika kwa maslahi ya UKAWA. Never.

Mtu mwenye fikra pana atafahamu kuwa Dkt. Tulia Ackson Mwansasu is the Speaker in waiting and she's here to stay.

Maisha ya bunge la kumi na moja ni miaka mitano. Hili siyo bunge la Katiba kama baadhi ya watu wanaotaka kulinganisha. Ninaamini ndani ya miaka mitano kutatokea mambo mengi nchini na mengine ambayo yatatikisa taifa huku yakitegemea maamuzi ya bunge katika kupata majibu.

Hoja kama za kashfa ya Lugumi ziko mbioni kuletwa bungeni baada ya uchunguzi kumalizika. Mijadala ya wabunge katika sakata kama hili ndiyo itakayotoa ushauri na mapendekezo kwa serikali. Nitashangaa sana kuwaona wabunge wa UKAWA wakitoka nje ya bunge kwenye mijadala ya aina ya kashfa ya Lugumi kwa sababu tu kuna Naibu Spika, Dkt. Tulia amekaa kwenye kiti cha Spika.

Kama ni kukurupuka basi katika suala hili ninaamini wabunge wa UKAWA wamekurupuka na kilichobaki kwa sasa ni kura matapishi yao!

Kuendelea kususia kwa muda mrefu kunaendelea kufanya maamuzi yao ya kurudi bungeni kuwa magumu zaidi.

Kurudi pia kwa kutumia sababu ya hoja inayosema ''tumekuja kujadili kwa sababu hili suala linahusu maslahi ya kitaifa'' itakuwa ni kichekesho kwa sababu hakuna suala linalojadiliwa bungeni lisilokuwa na maslahi ya kitaifa.
 
Really depends on perspective,UKAWA (read the people) probably lost a battle but are winning the war. Katiba mpya ya watu lazima.
 
ni mtazamo wako, ila kipimo tosha ni pale ambapo watatoka nje na CCM watashindwa kuwajibisha LUGUMI. naona umewai kuwaomba UKAWA warudi ili wabunge wako wasiaibike kwa kushindwa kuwajibisha LUGUMI
 
Kwa mtu mwenye akili Timamau kabisa hastahili kumsifu wala kumpongeza Tulia.Na pili hata hiyo Doctrate yake ina maswali mengi kuliko majibu.

Ukisikiliza michango ya wabunge wa CCM na matusi wayatoayo kwa upinzani na anakaa anajichekesha kwenye kiti anaonyesha kwa kiasi gani siyo kiongozi anayefaa,wala hana Busara wala hekima
 
ni mtazamo wako, ila kipimo tosha ni pale ambapo watatoka nje na CCM watashindwa kuwajibisha LUGUMI. naona umewai kuwaomba UKAWA warudi ili wabunge wako wasiaibike kwa kushindwa kuwajibisha LUGUMI
Kwa kukusaidia kifikra, mimi sina wabunge.

Naomba pia uelewe kuwa walioibua na kushika bango kuhusu suala la Lugumi ni hao wabunge wa CCM kupitia PAC. Kumbuka UKAWA mpaka sasa wamegoma kuchagua Mwenyekiti wa PAC.

Sasa sijui wataaibika vipi kwenye suala ambao wao wenyewe wameibua na kufanya uchunguzi.
 
Ukawa wajiangalie sana..................hizi political movie zitawacost 2020......wakumbuke kilichowabeba mwaka jana kupata ushindi ni udhaif wa serikali kuu hasa kiutendaji..............ila kwa hii ya JPM itawabeba wabunge wengi sana wa ccm......ukibeza hili bas hujawajua watanzania vizuri
 
Kwa kukusaidia kifikra, mimi sina wabunge.

Naomba pia uelewe kuwa walioibua na kushika bango kuhusu suala la Lugumi ni hao wabunge wa CCM.

Sasa sijui wataaibika vipi kwenye suala ambao wao wenyewe wameibua na kufanya uchunguzi.
Acha uongo, ni mbunge gani wa CCM kaibua na kushikia bango issue ya Lugumi?
 
Back
Top Bottom