Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
Udhaifu mkubwa wa wana UKAWA ni kutowashirikisha wanachama wao na kutanguliza njia za mkato ambazo ndizo huzua migogoro isiyo na ukomo.
1) TEUZI ZOTE ZITOKANE NA MAONI YA WANACHAMA.
Mgogoro mkubwa uliojitokeza uchaguzi uliopita nafasi ya URAIS na kwa kiasi kidogo ubunge na udiwani ni kutowauliza wanachama wanataka nini. UKAWA walijipima bila ushahidi wowote wenye mashiko ni chama kipi kinakubalika bila ya kupiga kura za maoni za maeneo husika.
Matokeo yake Dr. Slaa na Prof. Lipumba na wafuasi wao hawakumuunga mkono Lowassa katika nafasi ya URAISI. Jibu lilikuwa ni kura ya maoni nchi nzima na ambaye angeshinda kura hizo za maoni za nafasi ya Urais angeliungwa mkono kwani hakuna utata.
Pia nafasi za ubunge na udiwani kama nafasi ya Urais walipaswa kupitishwa kwenye tanuru la UKAWA la kura ya maoni na atakayeibuka kidedea kuwakilisha UKAWA kupitia chama chake.
Vurugu nyingi zilizojitokeza katika kambi ya UKAWA na migogoro mingi ambayo iliacha makovu leo ingelikuwa haipo.
USHAURI.
UKAWA wajifunze juu ya umuhimu wa demokrasia kama silaha muhimu ya uteuzi. Hata hizi nafasi za EALA zimekumbwa na malalamiko kwa sababu ni maamuzi ya wachache tu.