UKAWA waanzishe vyombo vya habari

UKAWA waanzishe vyombo vya habari

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
25,994
Reaction score
25,387
Ipo haja ya UKAWA kuanzisha vyombo vyake vya habari vitakavyosaidia kunadi na kutangaza sera zao ili kuendana na kasi ya CCM wenye vyombo lukuki vinavyowasaidia kunadi sera zao kama vile TBC1, TBC Radio, TBC FM na Radio Uhuru. Lakini pia wana magazeti lukuki yanayosaidia kuwanadi kama vile Habari Leo, Jambo Leo, Uhuru, Mzalendo, Daily News, Majira na vipeperushi vingi tu.

Kwa utitiri huu wa vyombo vya habari vinavyonadi sera za CCM huku vikijitahidi kuficha habari mbaya za chama hicho na serikali yake, ipo haja ya UKAWA nao kuanzisha vyombo vya habari vitakavyosaidia kunadi sera na habari zao. Unajua chama kikisemwa sana...kila siku watu wakilala wakiamka wanaamkia habari ztinazohusu chama kimoja tu, itajenga taswira mbaya miongoni mwa wananchi kwamba ndicho chama chenye sera nzuri.

Ni sawa na kuwa na bidhaa nzuri inayofichwa halafu kukawa na bidhaa mbovu na feki inayotangazwa kila siku...watu watanunua bidhaa hiyo hiyo mbovu kwa kuwa hawana habari juu ya bidhaa bora wasiyojua kama ipo sokoni.

:israel:
 
Wataletewa zengwe kwenye kusajili.
Kila siku vitafungiwa kwa kuwaumbua watawala.
 
mkuu mbona umeweka na vyombo vya habari vya umma! au umesahau?! angalia kwenye bold na red

hayo magazeti wanasoma wenyewe tu. TBC1 wanaangalia lumumba team peke yao

inasikitisha kuona kwamba TBC inaendeshwa kwa kodi za watanzania lakini inawatumikia CCM peke yao.
 
Last edited by a moderator:
Itv inawatosha, na mzee wenu Mengi

kwa hiyo wewe unafurahi opposition wasipate coverage hata chembe wakati vyombo vilivyopo chini ya shirika la TBC vinaendeshwa kwa kodi za watanzania wote bila kujali vyama? mknd wk!
 
mkuu mbona umeweka na vyombo vya habari vya umma! au umesahau?! angalia kwenye bold na red

mkuu, ni vyombo vya umma hivyo? sasa mbona vinaitumikia CCM badala ya umma?
 
Last edited by a moderator:
Waunde na jeshi la police na tume yao ya uchaguzi au sio

hii mada ianzishe kama topic mpya watu wachangie...kwa leo tunazungumzia uanzishwaji wa vyombo vya habari.
 
Mimi nahitaji tuchukue hatua na kulalamika zile no kodi zetu"October"
 
pia ikumbukwe kwamba miundombinu mingi kama vile majengo wanayotumia CCM pamoja na viwanja vya mpira yalijengwa kwa nguvu za umma. so walipaswa kurejesha mali hizi kwa wananchi mara baada ya kuanzishwa mfumo wa vyama vingi badala yake wanaendelea kumiliki mali hizo kimabavu mpaka sasa.
 
Last edited by a moderator:
Jamani tunaomba ukawa wafungue nao kituo chao cha matangazo ili wanainchi tuwe tunaona live wanachokifanya, make vituo tunavyovitegemea kama #itv , #azamtv , na redio one saiv ni shiidaaaa hatupat tarifaa kabisa.
 
Aisee mkuu nakubaliana na wewe 100% kwa 100% maana hivi sasa hakuna matangazo yoyote yanayorushwa yanayohusu ukawa, hata magazetini kwny kituo cha TBC1 habari kuu zote zinazohusu ukawa wanazikwepa kuzisoma kabisa, huu ni ukiukwaji wa haki ya habari.
 
kwa sasa watanyimwa usajiri labda uchaguzi ukiisha watafikiriwa
 
kwa sasa watanyimwa usajiri labda uchaguzi ukiisha watafikiriwa

Hiyo ni kweli ila naona kwa hali inavyokwenda ni kuwa ccm wanajitafutia balaa zaidi kutoka kwa hasira za watanzania
 
Back
Top Bottom