activisty
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 315
- 107
Habari zenu wakuu wanajf,natumai mnaendelea vizuri na shughuli zenu za kila siku.Nimeuleta huu uzi ili nitoe japo ushauri kwa vyama vinavyounda UKAWA.
Mnamo tarehe 25 june,siku 4 tu zilizopita nilibahatika ufika jimbo la Mtwara Mjini,hapo nilikutana na shamrashamra za watia nia wa ubunge CHADEMA wakirudisha fomu zao.
Katika pitapita Zangu za hapa na pale nililisikia sana jina la Joel Nanauka, nikavutiwa kulifuatilia.Huyu ni kijana ambaye ana nguvu kubwa,yenye ushawishi kisiasa.Mwaka 2010 alishiriki kura za maoni ndani ya CCM ambapo walimpiga chini sababu hakuwa na fedha,jambo hili inasemekana liliwakera watu wengi sana.
Nilifanikiwa kusoma CV yake kutoka kwenye moja kati ya vipeperushi vyake,nilifurahi kuona amewahi kuwa tanzania one na kazi alizozifanya ni mtu aliyepikwa kwelikweli.
Watu wa UKAWA mliopo Mtwara Mjini nina hakika hamtafanya makosa,huyu kijana akipeperusha bendera ya UKAWA mtapata kura za vyama vyote na za wananchi wote wasiokuwa wanachama wa vyama vya siasa ambao kwa hakika idadi yao ni kubwa zaidi.
Licha ya propaganda nilizozisikia juu yake bado kwa nguvu ile ya yeye kuongelewa na watu mbalimbali,bado nashawishika huyu kijana akisimama mtwara mjini atashinda kwa kishindo.
Nilijaribu kufuatilia kuhusu mgombea wa CUF pia anaitwa bwana MUFTAA huyu jamaa kwa taarifa nilizozipata hajiamini sababu tayari wanachama wa CUF wamegawanyika baada ya bwana MATATA ambaye wanachama wa CUF wengi waliokuwa wanamtaka kutopitishwa kama mgombea kupitia CUF.
Nawasihi sana watu wa UKAWA wapime nguvu ya mgombea ili kuhakikisha jimbo la mtwara mjini halirudi mikononi mwa CCM.
Wengne waliotajwa katika kurudisha fomu hizo ni mwenyekiti wa chadema wilaya ya mtwara mjin bwana IBRAHIM MANDOA ambaye anaonekana anayo nguvu ndani ya chama japo watu waliokuwa wanamuunga mkono baada ya kuja JOEL NANAUKA wamemuhama kwa kusema kuwa japo kakitumikia sana chama mtwara mjin lakini hatauzika kwa wananchi ukilinganisha na JOEL.
Nilijaribu kuongea na viongozi wawili wa CHADEMA jimboni Mtwara ambapo wote kwa pamoja walisema wameona ujio wa Joel kama neema ya CHADEMA kushinda kwa kishindo Mtwara Mjini.
Pia yupo bwana MOHAMED HANGA aliyewahi kuwa mkurugenzi wa bodi ya korosho,huyu nasikia alikuwa na ushawishi mwanzoni ila baada ya ujio wa Nanauka na yeye amefifia kabsa..na mwingine ni bwana Mulukozi ambaye na yeye aliwahi kugombea ubunge kupitia chama hicho 2005 ila kwa sasa hana nguvu tena.
Kwa upande wa ubunge viti maalumu yupo binti anaitwa Anne Deo,huyu kwa nilivyofuatilia ni kamanda wa muda mrefu wa chadema ni kati ya wale walioibua vuguvugu za chadema vyuo vikuu...kwa chadema kuwa na binti mdogo kama yule wa kupaza sauti kusini ni jambo la kheri sana.
Huyu jamaa anayeitwa NANAUKA sikubahatika kumuona face to face,ila natamani siku moja nionane naye,nasisitiza sana kama ukawa mnataka kushinda mtwara mjini na majimbo mengine,vijana aina ya joel ni muhimu sana.