UKAWA: Tunaitambua rasimu moja tu

UKAWA: Tunaitambua rasimu moja tu

PISTO LERO

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2011
Posts
2,819
Reaction score
1,455
Dodoma. Bunge Maalumu la Katiba sasa lipo katika hati hati ya kuendelea kutokana na viongozi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutangaza kuwa hawatakuwa tayari kujadili rasimu tofauti na iliyowasilishwa na Jaji Joseph Warioba bungeni.

Wakizungumza katika mkutano na waandishi wa habari jana katika Ukumbi wa Pius Msekwa bungeni, viongozi wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba, James Mbatia, Freeman Mbowe na Tundu Lissu, walisema wataitetea rasimu hiyo, ndani ya Bunge na kwenye Kamati.

"Rais Jakaya Kikwete amekuja bungeni siyo kufungua Bunge la Katiba bali kaja na mapendekezo ya rasimu ya CCM, sisi tutajadili rasimu ya wananchi ya Jaji Joseph Warioba ambayo inazungumzia muundo wa Muungano wa Serikali tatu," alisema Profesa Lipumba.

Kutokana na msimamo huu wa Ukawa huenda Bunge litakwama kwani kwa mapendekezo ya CCM yenye Muundo wa Muungano wa Serikali mbili ni lazima kuandikwa upya Rasimu ya Katiba au kufanyika mabadiliko makubwa.

Profesa Lipumba alisema katika majadiliano juu ya rasimu, Ukawa watajikita kutumia Rasimu ya Katiba waliyopewa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba, ambayo imeeleza mapendekezo kwa nini yamefikiwa katika kila hoja," alisema.

Hata hivyo, alisema wamesikitishwa sana na Rais Jakaya Kikwete, badala ya kufungua Bunge alijikita katika kuchambua rasimu na kuikosoa tume aliyoiunda mwenyewe.

"Rais Jakaya Kikwete siyo tu amemdhalilisha Jaji Warioba pamoja na wajumbe wa Tume,bali amewadhalilisha wananchi waliotoa maoni kwani hata takwimu alizotoa za kupinga rasimu siyo za kweli," alisema Profesa Lipumba.

Alisema muundo wa Serikali tatu ndio mawazo ya wananchi ambayo yamekusanywa na watu wenye heshma wakiwapo Jaji Warioba aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na Jaji Augustino Ramadhani ambaye pia amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji.

Mkuu wa Zanzibar:
Alisema kauli za Rais badala ya kuimarisha umoja zimewagawa Watanzania kwani ametoa vitisho ambavyo havina sababu hasa kwa Wapemba bila kujua kuna Wanyamwezi wanaoishi Zanzibar.

Mbatia: Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi, James Mbatia ambaye pia ni mjumbe wa Bunge hilo,alisema kwa kauli ya juzi ya Rais Kikwete,kutangaza kuwapatia Zanzibar; watu, ardhi,mamlaka kamili na kusimamia uhusiano wa kimataifa ni kuvunja rasmi Muungano,Mbatia alisema Rais Kikwete pia amewagawa Watanzania katika kauli zake ikiwa ni pamoja na ile ya Wapemba kwa kulima vitunguu katika Jimbo la Kibakwe kana kwamba ni makosa.

Alisema wamesikitishwa na Rais kuacha kufungua Bunge badala yake katumia taarifa potofu za mitaani kuligawa Bunge na kuwadhalilisha wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

"Hakuna asiyejua sasa tupo katika mgogoro mkubwa wa kikatiba, Zanzibar tayari ni nchi kamili kutokana na mabadiliko ya 10 ya katiba yao waliyoyafanya mwaka 2010 baada ya kupitisha dhana ya kuwa Zanzibar ni nchi," alisema.

Mbowe: Mbowe alisema Rais amevunja maridhiano na hata kushindwa kusikiliza maoni ya aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Kenya, Seneta Amos Wako kuwa maoni ya wananchi yaheshimiwe.

Alisema Serikali ya Kenya ilichakachua maoni, ilichakachua rasimu na kusababisha vurugu kubwa jambo ambalo linaweza kutokea kwa Tanzania.

"CCM wasijidanganye kwa wingi wao bungeni hakika katika hili tutatetea madai na maoni ya wananchi hadi mwisho," alisema

Source: Mwananchi
 
Hongera kwa maGT wa UKAWA,kilichowapeleka Dodoma ni rasimu ya Tume ya Warioba siyo ya Jk na ccm wake.Watanzania tulio wengi tuko nyuma yenu.
 
Hapo ndipo hoja zenu zitakapo pigwa kumbo, maana humo mtakutana na wajuzi wa mambo hayo, kazi kwenu Ukawa.
 
Naona mnatafuta umaarufu usiokua na manufaa,hao wananchi ni akina nani? Mkoa wa Simiyu nani alipendekeza serikali tatu?
Ngoja niangalie Jambo Tanzania TBC1 Wassira anaongea.
 
Viongozi wa UKAWA achaneni kugombea uwenyekiti wa zile kamati mtafungwa midomo
 
Naona mnatafuta umaarufu usiokua na manufaa,hao wananchi ni akina nani? Mkoa wa Simiyu nani alipendekeza serikali tatu?
Ngoja niangalie Jambo Tanzania TBC1 Wassira anaongea.
Mkuu chuki, hawa viongozi wote wa ukawa wana matatizo yao. Hapo kuna mzinifu na waliberali. Unafikiri ninimkitaendelea?
 
Kumbe UKAWA ni matapeli wanaotoka ccm ambao wameandaliwa kwa mkakati maalymu wa kuja kutoa matamko ya kipuuzi kuwa changanya wananchi
Yani ccm wana mambo ya ajabu sana kwa mfano leo namuona wasira tbc asubuhi anatetea serikali mbili kwa kutoa mfano au kunuu alicho andika mzee nyerere kwenye kitabu chake cha hatma na uongozi eti nyerere aliona serikali mbili inafaa na saizi pia inafaa
Nimeshindwa kumuelewa wasira kwa kutojitambua kuwa huu muungano una miaka karibia 50 na dunia imebadilika watu wana uwelewa mkubwa.
 
Mkuu chuki, hawa viongozi wote wa ukawa wana matatizo yao. Hapo kuna mzinifu na waliberali. Unafikiri ninimkitaendelea?

Unamfurahisha nani kwa kuchangia upuuzi?? Usiwe kama asietaka kumuuzi mumewe kwa kukubali kumpa 0713
 
Bunge lile halipo pale ili kuandika Katiba upya, bali lipo kwa ajili ya kujadili na kuboresha rasimu ya Katiba inayotokana na maoni ya wananchi yaliyokusanywa na Tume iliyoongozwa na Waryoba. UKAWA wanatakiwa wakatae moja kwa moja maagizo ya mwenyekiti wa taifa wa CCM ya kuandika upya rasimu. Ikibidi wapeleke madai mahakamani wapate tafsiri ya kisheria ya jambo hilo.
 
Naona mnatafuta umaarufu usiokua na manufaa,hao wananchi ni akina nani? Mkoa wa Simiyu nani alipendekeza serikali tatu?
Ngoja niangalie Jambo Tanzania TBC1 Wassira anaongea.

Kasome taarifa ya Tume utawajua ni akina nani. Kama simiyu hawakupenedekeza hivyo haiondoi uhalali wa mapendekezo kwanza sheria mlioyoitunga haikusema kama Simiyu hawajapendekeza basi mapendekezo ya wengine hayatakubalika. Wewe unataka kusema kama mtu hamkuchagua Kikwete huyo mtu hatakiwi kusema Kikwete ni Rais wa nchi? Mimi nawalaumu wabunge kwa kutunga Sheria mbovu kuliko zilizowahi kutungwa hapa Duniani na wawakilishi wa wananchi kama hii ya mabadiliko ya Katiba. Haikuwa specific namna ya kufikia maamuzi kuhusu maoni ya wananchi. Kwa msingi huo kilichoandikwa na Tume ni sahihi kwa kuwa kimefuata sheria ambayo iliipa mamlaka Tume kukusnaya maoni, kuyachambua na kuja na mapendekezo.
 
Naona mnatafuta umaarufu usiokua na manufaa,hao wananchi ni akina nani? Mkoa wa Simiyu nani alipendekeza serikali tatu?
Ngoja niangalie Jambo Tanzania TBC1 Wassira anaongea.

Vipi wewe kwani wewe mpaka uone mkoa wa simiyu wanasemaje ndio ukubali serikali tatu, what is mkoa wa simiyu au hujaisoma rasimu ya Jaji warioba nini!... zile enzi za zidumu fikra za mwenyekiti wa ccm, zilishapita
 
hawa watu wa UKAWA nawapendaga sna kwani hawatishiwi nyau wao wanataka maoni ya wananchi yazingatiwe
 
Kikwete alichaguliwa na wananchi milioni tano kwa hiyo hao milioni 44 ambao hawakumchagua basi ni rais batili maana amasemea yake maoni ya tume hayawakilishi maoni ya watanzania walio wengi...huyu jamaa ni janga!!
 
Back
Top Bottom