Mu-sir
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 3,621
- 1,640
Someni huu waraka tuna ya kujifunza👇
Siasa za Kenya za Mwaka 2002 ni miongoni mwa siasa zilizokuwa na msisimko wa aina yake katika Ukanda wa Afrika Mashariki. Ni mwaka ambao KANU iliondolewa madarakani Rasmi na Wakenya na hatimaye kufifia katika ulimwengu wa siasa.
Hata hivyo uchaguzi huu, pamoja na kuwa Wakenya wengi walishachoka na KANU na complacency yao (ikichagizwa zaidi na kuondoka kwa kundi kubwa la wanasiasa wa KANU baada ya Mzee Moi kuleta "jina la mfukoni" la Uhuru Kenyata kugombea Uraisi kwa tiketi ya KANU), bado NARC walikuwa na wakati mgumu sana kutokana na Mgombea waliemsimamisha (pamoja na kuwa Raila Odinga wakati wa Mkutano wao pale Uhuru Park alisema "Kibaki Atosha"
Nina sababu tatu ambazo nazichukua kulingana na hali inayozunguka mgombea wa UKAWA
Moja, Emilio Mwai Kibaki umri wake ulikuwa umeenda sana. Hakuwa tena Mwai Kibaki yule wa siku za Nyuma ambae angeweza kusimama bungeni au kwenye majukwaa ya kisiasa akipanga hoja bila kusoma popote na mara nyingi kengele ikimkuta ili akatishe hotuba yake.....Kibaki wa 2002 hakuwa Kibaki yule tena...hakuwa na nguvu wala uwezo huo tena. Hakuwa tena Kibaki yule aliyekuwa na mvuto bali alionekana mchovu na mzee
Mbili, Mzee Kibaki alipata ajali siku chache mara baada ya kuanza kwa kampeni akiwa anatoka kwenye mkutano wa kampeni huko Machakos. Hili lilifanya Mzee Kibaki akalazwa hospitali Nairobi lakini pia London. Hili lilifanya ushiriki wake kwenye Campaign kuwa mdogo sana zaidi ya hili neno lenyewe mdogo
Tatu, Mzee Mwai Kibaki alilkuwa Waziri wa Fedha serikali ya KANU chini ya Mzee Kenyatta mwaka 1969 mpaka mwaka 1981 lakini pia a mekuwa makamu wa Raisi wa KANU mwaka 1978 mpaka 1988 chini ya Mzee Daniel Arap Moi....Kutokana na hali isingekuwa rahisi kumtenga Mzee Kibaki na sababu za kudorora kwa uchumi wa Kenya....maana allihesabika kama mingoni mwa waliochangia kudorora kwa uchumi
Nini timu yake (ikiwa chini ya the Late Kijana Wamalwa na Raila Odinga) ilifanya??
Katika moja ya Speech za Kijana Wamalwa alisema hivi na nukuu "The captain has been injured in the field...but the rest of the team shall continue.." (Kwa tafsiri ya Kiswahili isiyo rasmi......"Nahodha ameumia uwanja wa mapambano....wengine tutaendelea na mapambano"
Timu hii ilifanya kampeni kwa sehemu kubwa sana na kama kumbukumbu zangu zitakuwa sawa katika moja ya mikutano yao ilifika mahali waliongea timu yake woote na mwisho kabisa Raila Odinga alimkaribisha Kibaki akasema (kwa mujibu wa kumbukumbu ninazozivuta)...."Bwana Msee Sasa ni samu yako, hebu nyorosha tu mikono juu, salimia hii mutu yote hapa mbele yako"...ilikuwa ni shangwe, vifijo na vigelegele
Timu hii ilifanya kazi nzuri ikiwamo kuelezea Wakenya kile wanataka kuwafanyia na sababu nyinginezo ikiwa ushiriki wake kama sehemu ya KANU kudororesha uchumi wa KENYA
Katika hali ya ajabu kabisa NARC alishinda kwa ushindi wa 62% dhidi ya 31% za KANU
Kwa nini Wakenya walikubali risk ya "fear of the unknown" pamoja na kuchagua Raisi "Mgonjwa" ambae haikuwa raihisi kujua ataishi au lah?
Kumbukumbu zangu zinarejea miongoni mwa Wakenya waliohojiwa wakati ule na BBC walisema hawana Imani tena na KANU maana imesababisha "stagnation and mismanagement of Kenya's economy" na kwa kuwa sasa wako tayari kujaribu muelekeo mpya wa kisiasa ambao unaweza ku-revive uchumi wao.....
Wengi walionekana kufurahia pia sera zao ikiwa ni pamoja na mikakati ya kukuza uchumi pamoja na elimu ya bure.
Kwa ufupi waliielewa Ilani ya NARC pamoja na kuwa "Le Capitain" Mwai Kibaki alikuwa hoi......wakaamua kuitupilia mbali KANU na ku-risk kumchagua Mwai Kibaki na NARC yake japokuwa alikuwa mgonjwa.....walibeba risk zote mbili..."the fear of the unknown" lakini pia "kuchagua Rais Mgonjwa"
Je Imani yao ililipa?
Hili tunaweza kuliona maana Kenya ni majirani zetu....Mwai kibaki alijitahidi kubadili mwelekeo wa uchumi wa Kenya pamoja na huduma ya uhakika ya elimu.
GDP yao ilikua kutoka 0.6 wakati anaichukua serikali mwaka 2002 mpaka 7% mwaka 2007 huku sekta nyingi za kiuchumi zikiinuka ikiwa ni pamoja na mashirika mengi ya umma yaliyokufa yalifufuliwa na kuanza kujiendesha kwa faida.
Hii iliambatana na kukua kwa miundombinu, mawasiliano na kutanuka huku akipata sifa kubwa sana kweny kupunguza utegemezi wa Kenya kwenye misaada ya nje huku akisisitiza zaidi uchumi wa Kenya kujijenga wenyewe.
Aliyafanya haya yote wakati mwingine akiwa kwenye wheelchair huku akisoma hotuba kuanzia neno la kwanza hadi la mwisho........Alisifiwa sana na wengi kama kiongozi aliyekuwa na msimamo mkali na uwezo (intelligency) ya kusimamia serikali yake na kutoa miongozo mbalimbali ambayo ingeweza kubadili uchumi wa Kenya ikiwamo kuanzishwa kwa Constituency Development Fund (CDF) mwaka 2003 ambayo wengi wa wachambuzi wa Siasa za Kenya wanasema "logic" yake ndiyo iliyoasisi ugatuzi wa madaraka ambao ulijitokeza kwa mapana kwenye Katiba yao ya 2010.
Hata hivyo criticism pia zilikuwepo ikiwamo baadhi ya watu kudai "anaendesha serikali kwa kutumia kikundi kidogo cha Wakikuyu" pamoja na criticism za "over-delegation" iliyofanya serikali yake kuonekana dysfunctional...
UKAWA wana la Kujifunza
Ni ukweli usiopingika kuwa afya ya Mh. Lowasa haiko vizuri. Sumaye alinisaidia kuthibitisha hili maana katika maelezo yake hakuna mahali alipinga kuwa Lowasa haumwi bali alimlinganisha na wengine kuwa nao wanaumwa....sababu kuu aliyoitoa Sumaye ni kuwa Mzee Lowasa ana umwa maradhi ya "umri"......Kwa wasiofahamu, kwa sasa Mzee Lowasa ana umri wa Miaka 62....hatutarajii anaweza kuwa na makeke yale ya kuzungumza lakini hasa pia ukizingatia kwa haiba siyo mzungumzaji mzuri wala mtu mwenye vibwagizo kibaao anapozungumza
Mpaka sasa nimesikiliza mazungumzo ya watu wengi....wengi wako tayari "kujaribu" maendeleo nje ya CCM....hata hivyo ni dhahiri kuwa wanachangamoto ya kuhofia afya ya Mh Lowasa lakini pia bado hawajaridhika kwa ile "kutokusikia sera" wakihukumu kutokana na mkutano wa juzi Jangwani....
Wengine, kutokana na kupenda maneno mengi sana, waliumia sana na Lowasa kuzungumza muda mchache...
Haipingiki kuwa Lowasa kwa haiba yake siyo mzungumzaji sana kwa sasa siyo mtu wa kuweza kuhimili jukwaa na kulishambulia kiasi cha kukata kiu ya "mazoea" ya Watanzania wengi ya kusikia sera zinachambuliwa kwa undani....tunapenda Ungwini sana
Kwa waraka huu, niwashauri UKAWA kunakili walichofanya NARC....Wenye uwezo wa kusema wapo wengi, wapewe nafasi kuisemea Ilani ya UKAWA....wazungumze kwa undani wake, waeleze watakavyokuza uchumi, waeleze namna gani watakuza sekta ya kilimo, waeleze elimu itatolewaje bure n.k
Mwisho wamlete azungumze kwa muda mfupi,....au kama vipi na yeye aambiwe "msee karibu salimia hii mutu hapa mbele yako"
Ni kweli anao uwezo wa kusimamia...anaouwezo wa kutoa miongozo ya utekelezaji na akaisimamia....lakini hili halitoshi kama hatutasikia sera kwa mapana yake...
lakini pia msimlazimishe kusema zaidi ya uwezo wake kama ambavyo watu wengi wanajaribu kushauri hapa....haiba yake si mtu wa maneno mengi...msimtake awe na maneno mengi ili kuridhisha watu....anaweza kujikuta anatamka hata yasiyotakiwa kutamka maadamu tu kufikia mahitaji ya watu wanaotaka aongee saaaanaaa....
Wa kuongea kunadi sera waongee (wakina Sumaye wanaweza) kisha wamlete mzee agonge "signature" tu hata kwa kusema maneno machache kwa dakika tano tu......
BINAFSI NIMECHOKA MARAISI WANAOONGEA KUHUTUBIA 3HRS mpaka tunawapa na matuzo ya kuongea saanaa lakini utekelezaji wa SERA ni wa Kusuasua....Bora uongee dk 2 lakini utekeleze hitaji la mabadiliko tunayohitaji
Credit to lane

Last edited by a moderator: