UKAWA tumejipangaje? Hawa wanaohamia wafuate kanuni

UKAWA tumejipangaje? Hawa wanaohamia wafuate kanuni

Manjagata

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2012
Posts
16,549
Reaction score
18,673
Wakuu habari za Alasiri?

Kumeibuka wimbi la raia kutimka Magambani na kuja UKAWA, hapa namaanisha viongozi na wanachama wa kawaida. Sasa hivi ni kila kona ya nchi ninasikia mara waliokuwa madiwani wa ccm wahamia CHADEMA, mara wahamia CUF, mara wahamia NCCR. Kidogo unasikia mwenyekiti wa ccm mkoa fulani ahamia CHADEMA au abwaga manyanga, sasa najiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu lakini swali kubwa kabisa linalonisumbua "TUMEJIPANGAJE?". Haitakuja kutokea kwamba vyama vyetu vikawa ccm B?

Hawa jamaa tutawadhibiti vipi ili wafuate misingi ya vyama vyetu vinavyounda UKAWA? Je, hayatatokea kama ya Mbingu wa Mutharika kule Malawi kwamba baada ya kukorofishana na chama chake akatimka na watu wake na kwenda kuanzisha chama kingine (ingawa hapa kwetu sina uhakika kama sheria zinaruhusu hili).

Hayatatulazimisha kuvaa manguo ya kijani haya? Nawaomba viongozi wetu wa UKAWA wawe makini na hili isije ikawa akina Makongoro, Kimbisa, Mgana n.k. wamekimbilia kwetu ili tuwapitishe kugombea ubunge halafu wakifika bungeni waanze kutusumbua kama Shibuda na Lety!

Mwisho viongozi wetu wamwagize rais wetu mtarajiwa aanze sasa kuvaa gwanda ili tumtambue kwa mavazi!! Kwa mfano kesho anapoenda kuchukua fomu anatakiwa atinge ndani ya Gwanda ili magamba yapukutike!!
 
Mi nabuku
Wakuu habari za Alasiri?

Kumeibuka wimbi la raia kutimka Magambani na kuja UKAWA, hapa namaanisha viongozi na wanachama wa kawaida. Sasa hivi ni kila kona ya nchi ninasikia mara waliokuwa madiwani wa ccm wahamia CHADEMA, mara wahamia CUF, mara wahamia NCCR. Kidogo unasikia mwenyekiti wa ccm mkoa fulani ahamia CHADEMA au abwaga manyanga, sasa najiuliza maswali mengi yasiyokuwa na majibu lakini swali kubwa kabisa linalonisumbua "TUMEJIPANGAJE?". Haitakuja kutokea kwamba vyama vyetu vikawa ccm B? Hawa jamaa tutawadhibiti vipi ili wafuate misingi ya vyama vyetu vinavyounda UKAWA? Je, hayatatokea kama ya Mbingu wa Mutharika kule Malawi kwamba baada ya kukorofishana na chama chake akatimka na watu wake na kwenda kuanzisha chama kingine (ingawa hapa kwetu sina uhakika kama sheria zinaruhusu hili). Hayatatulazimisha kuvaa manguo ya kijani haya? Nawaomba viongozi wetu wa UKAWA wawe makini na hili isije ikawa akina Makongoro, Kimbisa, Mgana n.k. wamekimbilia kwetu ili tuwapitishe kugombea ubunge halafu wakifika bungeni waanze kutusumbua kama Shibuda na Lety!

Mwisho viongozi wetu wamwagize rais wetu mtarajiwa aanze sasa kuvaa gwanda ili tumtambue kwa mavazi!! Kwa mfano kesho anapoenda kuchukua fomu anatakiwa atinge ndani ya Gwanda ili magamba yapukutike!!
 
Target sasa ni kushika dola..

Hayo mengine ni rahisi sana kuyashughulikia, tuna uzoefu wa kutosha katika hilo
 
Hii ya UKAWA wamejipangaje haihitaji maelezo marefu

11836673_953253784715859_8748747612183064738_n.jpg
 
Back
Top Bottom