UKAWA, tayari Jiji la Dar lipo chini yetu, pambaneni na changamoto zilizopo

Ritz

JF-Expert Member
Jan 1, 2011
49,680
39,004
Wanaukumbi.

Jiji la Dar es Salaam kuwa sasa lipo chini ya UKAWA ni muda sasa wa UKAWA kupambana na changamoto nyingi za Jiji hilo baada ya kupata mameya na manaibu meya Kinondoni na Ilala.

Tatizo kubwa la foleni kwenye jiji la Dar esa Salaam pamoja uchafu mwingi unaozalishwa ni muda wa UKAWA kutatua ili tatizo.

Pia changamoto ingine ni mfumo wa leseni za biashara maeneo ya Ilala na Kinondoni imekuwa kero kubwa kwa wafanyabiashara ni wakati sasa wa UKAWA kupambana na ili suala la leseni.

Changamoto ingine hii mifumo ya ulipaji ushuru wa masoko kama Tandale, Kariakoo, Buguruni na maeneo mengine ni wakati sasa wa UKAWA kulisimamia ili suala hili wananchi wafanye biashara zao bila usumbufu.

Suala la parking kwenye Jiji la Dar es Salaam ni kero kubwa ni wakati sasa wa UKAWA kulitatua wananchi pamoja na malipo ya parking.

Usumbufu mkubwa wa ukamataji ovyo wa bodaboda na bajaji hii ni miradi ya watu ni wakati sasa wa UKAWA kulisimamia hili.
 
Safiii! At least mnakiri kuwa ccm imeshindwa kutatua changamoto hizo kwa kipindi chote ambapo wao ndiyo walizisimamia halmashauri hizo.
Ni wakati wa UKAWA sasa kutatua kero za wananchi kwenye jiji la Dar es Salaam.
 
Ngoja tusubiri tuone mbinu watakazotumia kuondokana na foleni pia waangalie leseni za biashara wananchi tunalipa kiasi kikubwa sana hasa Kariakoo.
 
Ni wakati wa Ukawa sasa kutatua kero za wananchi kwenye jiji la Dar es Salaam.
Tulia uone mipango na sera madhubuti vinavyotekelezwa chini ya UKAWA. UKAWA itatatua kero zote kwa miaka 5, ambazo zilizoshindikana kwa miaka 50 chini ya serekali ya CCM.
 
Madiwani wa Ukawa na Meya wa Ukawa tuangalizieni hii kero ya leseni ya biashara kuwa laki tatu wakati zamani ilikuwa bure..
 
Mjiandae..mvua za el nino zinakuja..mmeenda mahakamani kuzuia bomoa bomoa mabondeni..sijui mnawaza nini.
 
Hivi pamoja na CCM. Kuita mamluki akiwemo naibu wa mjengoni imekuwaje wakashindwa?
 
Ni wakati wa Ukawa sasa kutatua kero za wananchi kwenye jiji la Dar es Salaam.
Kwanza hongereni.Pili mie naona mtihani kwani hao mameya watakuwa na Kibarua cha ziada kuhakikisha mambo yanaenda sawa ktk wilaya zao. Changamoto ya kukusanya kodi. Kodi nyingi zisizoleta migongano ni zile tu za TRA ama zingine ambazo ziko chini ya halimashauri sins uhakika kama wataweza hata kutupigia greda barabara za mitaani. Tunashangilia tu ila hii kazi itakuwa ngum kwa aliyekabidhiwa maana hizi ni zama za blabla.
 
Suala la Halmashauri kuwa chini ya CDM sio geni. Kilimanjaro nadhani ni muda mrefu sasa, Kigoma Etc. Je kuna jambo kama taifa tunaweza kujivunia kuwa wakati Halmashauri ya Kigoma Ujiji au kilimanjaro IPO chini ya CDM kuna jambo hili na lile vilikuwa tofauti? Au walizifanyia nini Halmashauri zao?
 
CDM wameongoza Halmashauri Ya Karatu Na Moshi Tangu 95 Mpaka Leo Hakuna Tofauti Yoyote Na Halmashauri Za CCM.Refer CAG Report.Kazi Ni Matusi Tu Na Maandamano Na Kusingizia Hawana Serikali.
 
Back
Top Bottom