TataMadiba
JF-Expert Member
- Feb 7, 2014
- 9,866
- 5,742
Habari za Jumatano wapendwa,
Baada ya UKAWA kuona Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. John Pombe Magufuli ni kisiki cha mpingo, wameamua kuifanya hali ya kisisa Zanzibar kuwa habari ya mjini. Bahati mbaya kabisa wanaifanya kuwa habari ya mjini kwa hoja mfu kabisa.
Eti Rais aingilie kati mgogoro wa Zanzibar kwa sababu vurugu zikitokea yeye ndiye atakayepelekea majeshi kutuliza vurugu hizo. Wanakwenda mbali na kusema hali hiyo ikitokea Rais hatakwepa kusimama mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya ICC kama ilivyokuwa kwa Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta(anayeyasema haya ni anayejiita Mwanasheria mahiri).
Hizi ni hoja mfu tu tena za kutapatata.Labda Lissu hajui sababu ya Uhuru Kenyatta kusimama kwenye Mahakama ya ICC. UHURU Kenyatta alisimama ICC siyo kama rais wa Kenya bali kama mmoja wa watu ambao alihamasisha wafuasi wa chama chake kufanya vurugu mwaka 2007, na hakuwa rais wa Kenya wakati huo.Hili swala la Rais Magufuli kupeleka jeshi Zanzibar endo kutakuwa na fyokofyoko, nilishalianzishia uzi humu JF.
JPM ni Amri jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Tanzania(Tanzania bara na Zanzibar). Anawajibika kikatiba kuhakikisha watu wake wanaishi kwa amani wao na mali zao. Kwa maaana ya Polisi, JWTZ na vyombo vingine vya ulinzi havina mahusiano yoyote na masuala ya siasa, vitaingia Bungeni, Mahakamani, Ikulu, ndani ya Ofisi ya chama siasa, kanisani, msikitini na mahali popote pale ambapo amani itaonekana kutoweka.
Ghasia zinapotokea Makanisani, misikitini na vyombo hivi kuingilia kati, mbona Lissu na wanasheria mahiri wenzake hawahoji hatua hizo? Majeshi ya Marekani yako Syria, Kongo DRC, Somalia, Elitria, Iraq n.k. Rais Obama wa Marekani alishaonesha juhudi zozote za kuingilia migogoro ya nchi hizo kabla ya kupeleka majeshi? Si hawa Marekani ndiyo baba wa Mahakama ya ICC?
TAFAKURI:
1. UKAWA kutumia hali ya kisiasa Zanzibar kama njia iliyobaki ya wao kupmbana na kasi ya JPM katika kumdhoofisha hakutawaondolea imani Watanzania kwa rais wao. Magufuli atabaki kuwa rais wa Watanzania Wanyonge ambao ndiyo wengi bila kujali itikadi ya vyama vya, dini zao, rangi zao na mahali wanapotokea. JPM kaletwa na Mungu kuwakomboa Watanzania. Tutazidi kumuombea kama ambavyo amekuwa akituomba Watanzania tumuombee ili watu aina ya Lissu washindwe na Walegee.
2. CHADEMA na MAALI SEIF wanaelekea kuwa wanufaika na hali hii ya Zanzibar bila kujali athari wanazozipata Wazanzibari Wenyewe. Bila kuwepo na mgogoro huu CHADEMA ni kama wamefilisika kisiasa kutokana na ukweli kwamba kile ambacho Watanzania walifikiri wangekipata kutoka kwa Wapinzani kabla ya kuingiliwa na Mafisadi sasa wanaelekea kukipata kwa JPM.
Maalim Seif Wazanzibari walishamchoka na wakatamani kuona sura mpya katika siasa za Upinzani ndani ya siasa za Zanzibar, anaamua kutumia mgogoro huu kuzaliwa upya katika siasa za Zanzibar na pia kuendelea kuvuna mlungula kutoka Makundi mbalimbali kwa kisingizio chs kumpa ushirikiano. Ingependeza kama Maali Seif angetangaza kujiuzulu nafasi ya Makamu wa Rais Zanzibar ili kuuoneshea Upinzani wa Zanzibar dhamira yake ya kweli kwenye mgogoro huo.