UKAWA rudini kwenye katiba ya wananchi, haya mengine yanawapotezea muda tu!


MAHANJU

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Messages
4,934
Likes
5,273
Points
280
MAHANJU

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined Aug 26, 2014
4,934 5,273 280
Nipende tu kusema kwamba hili halitawafurahisha upande mmoja lakini kwa kiasi kikubwa litawafanya wananchi walio wengi kuwaelewa ni nini mnatetea.Kwa sasa bila hilo jambo mtafanya yote lakini haitosaidia.


Kama kuna mtu alitegemea jipya kwa serikali ya CCM chini ya katiba iliyopo sasa ilikua kutokuelewa tu kwa sababu muundo wote wa serikali bado utakua chini ya mamlaka moja kuu tu hasa kwa nafasi kubwa za kiutawala nchini. Tuwe tu wakweli kua na mtawala ambaye jina lake limependekezwa na chama flani na amekabidhiwa ilani ya chama hicho ni lazima atii matakwa ya chama hicho.


Chamsingi ilitakiwa kutumia nguvu zote kuidai katiba mpya iliyo bora nchini kwa namna yeyote ile isiyovunja sheria, inatakiwa viongozi wate wa upinzani wanaougulia maumivu ya katiba iliyopo kwa manyanyaso ya watawala waumize vichwa ni ipi njia bora ya kushinikiza kupatikana kwa katiba mpya. Kuliko watu kuvunjwa miguu kwenye sekeseke la kutaka kuzuia mkutano wa CCM Kule Dodoma ni bora wanetumia muda huo kushinikiza maridhiano ya kupatikana kwa katiba mpya.


Hii hali ya kupeana vyeo kiurafiki,kiuchama,kiundugu,kifamilia na kiukoo haiwezi kuisha chini ya katiba iliyopo, haitakiwi kukaa kimya juu ya hili! Tafsiri ya jina UKAWA ni umoja wa katiba ya wananchi hivyo jina hili litumike kama na lienziwe kama lilivyo.Ni muda mwafaka kwa viongozi wa CUF,CHADEMA,NCCR na NLD kukaa tena mezani kuanza shughuli upya! Ni bora mpambane na polisi kwenye jambo muhimu Kama hili lakini sio kwenye mambo ambayo mnatafsiriwa kama mna maslahi binafsi nayo.


Hakika ikipatikana katiba mpya iliyobora(siyo pendekezwa) hata kama CCM wataendelea kutawala lakini kutakua mabadiliko makubwa sana ya kiuwajibikaji, Msidai katiba Kwa malengo ya kuitoa CCM madarakani! hiki ndicho kinachowafanya watawala kutia mikono yao kufuta maoni ya wananchi na kua na mioyo migumu isiyo na huruma, CCM kwa katiba bora madarakani automaticaly watatoka wenyewe muda ukifika tu.

Kua na tume huru ya uchaguzi haitoshi kabisa kuwapa UKAWA Ushindi, Kama mlisikiliza maneno ya mzee lubuva kwa makini mtagundua tu kwa yale maneno yalikua ni kuwatia moyo baadhi yetu lakini hayana ukweli wowote, huwezi kua na tume huru chini ya katiba iliyopo na hata kwenye ile pendekeza ambapo bado Rais ana mamlaka makubwa! Yaani ateue wakuu wa wilaya, ateue makatibu tawala,wakuu wa mikoa na wakurugenzi ambao ndio bado watawakilisha tume ya taifa ya uchaguzi wakati wa chaguzi zote,haiingii akilini.


Wakuu wa vyombo vyote vya dola bado ni watele wa mtukufu rais, Ni lini wataacha kupalilia vitutumbua vyao? Unafikiri wao hawapendi uheshimiwa? Tume ya uchaguzi itapatikanaje chini ya katiba iliyopo au pendekezwa ikiwa hawa makamishina wa tume watafanyiwa usaili na viongozi wandamizi wa serikali ambao kimsingi bado ni makada watiifu wa CCM? Au kuna njia nyingine ya kuwapata makamishina wa tume ya uchaguzi hata kama rais hatotia mkono wake?

Wenzetu wa Kenya walishayaona haya na ndio maana wanatukimbiza kwa kila kitu,walikimbizana na vyombo vya dola vya Serikali ya Mzee Mwai Kibaki,wengine walivunjwa miguu na mikono lakini mwisho wa siku WA nayo katiba bora ya taifa lao sasa, walitumia nguvu zao zote kushinikiza uundwaji wa katiba mpya na sasa wanajivunia na kidogo wanapata ahueni katika mipango yao ya kimaendeleo.Ni bora kuburuzana na vyombo vya dola kwa suala la katiba hata kama tumeambiwa siasa ni mpaka 2020 kuliko kwenye mambo yasiyo ya misingi, atakayesema kuidai katiba bora ni kufanya siasa basi atakua halitakii mena taifa letu na ndio chanzo cha uvunjifu wa amani ya nchi.

Ndio kazi pekee na ya thamani ambayo UKAWA mnatakiwa kuumiza kichwa zaidi.
 
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2015
Messages
14,085
Likes
13,802
Points
280
YEHODAYA

YEHODAYA

JF-Expert Member
Joined Aug 9, 2015
14,085 13,802 280
.
Ndio kazi pekee na ya thamani ambayo UKAWA mnatakiwa kuumiza kichwa zaidi.
Unapigia mbuzi gitaa na kupoteza muda hao watu hawashauriki.Ajenda zao ni za kuokoteza.Hawajui kipi cha maana na kipi si cha maana na hawashauriki.Kwa mtizamo wangu wanachama wa UKAWA wengi wanataka mabadiliko ya kweli na maendeleo ya kweli ila viongozi wa UKAWA ni sifuri kichwani.Wanachama wa UKAWA wana akili kuliko viongozi.
 
kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2015
Messages
2,500
Likes
1,324
Points
280
kibwenzi

kibwenzi

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2015
2,500 1,324 280
maoni yako mpelekee katibu msomi kuliko wote yuko pale ufipa kajaa tele
 
F9T

F9T

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2015
Messages
1,411
Likes
1,841
Points
280
Age
28
F9T

F9T

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2015
1,411 1,841 280
"msidai katiba mpya kwa lengo la kuitoa CCM madarakani" hahaha ni mpumbavu pekee asiyejua lengo la kuanzishwa UKAWA na kujua kuwa ilianzishwa kwa ajir ya katiba.
 
mtunzasiri

mtunzasiri

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2012
Messages
1,346
Likes
809
Points
280
mtunzasiri

mtunzasiri

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2012
1,346 809 280
Umeambiwa hakuna siasa mpaka 2020 sasa hilo la katiba watafanyia wapi bungeni wanabigwa ban majukwaani marufuku wataenda wapi kuzungumzia katiba mpya au ndo wasubiri 2020? Una lako jambo......
 
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2011
Messages
44,922
Likes
12,875
Points
280
Bavaria

Bavaria

JF-Expert Member
Joined Jun 14, 2011
44,922 12,875 280
Utaidai hiyo katiba mpya bila mikutano ya hadhara.??
 

Forum statistics

Threads 1,237,360
Members 475,533
Posts 29,285,833