UKAWA na kampeni eneza Lowassa vijijini

UKAWA na kampeni eneza Lowassa vijijini

mkafrend

JF-Expert Member
Joined
May 12, 2014
Posts
3,045
Reaction score
1,503
WanaJF, Salaam!

Kusema kweli mimi ninawiwa kuwaalika wote wenye mapenzi mema na nchi hii hususan wananchi wa kipato duni kuhakikisha kwamba tunatoa sehemu ya kipato chetu kueneza uzuri wa EDWARD LOWASSA katika vijiji tutokavyo au mahali ambapo ndugu zetu, rafiki zetu na jamaa zetu wanaishi.

Tuwaaminishe kabisa kabisa kuwa ilani ya ccm ni mbovu kwa kuwa haitoi nafasi kwa watoto wetu kupata elimu bure lakini ilani ya Edward LOwassa ni nzuri kwa kuwa kuanzia mwezi Januari, 2016 watoto wetu wote wataanza kusoma bure shuleni kuanzia chekechea hadi chuo kikuu. Aidha, watoto wa maskini wakihitimu elimu ya chuo kikuu watapata mikopo ili wajiajiri wenyewe kwenye sekta mbalimbali.

Lowassa pia ndiye anayeweza kupigana na kurudisha viwanda na nyumba zilizouzwa na CCM

Msisitizo: Tumia muda mwingi kushawishi ndugu zetu vijijini tuiondoe ccm
 
Ondoa shaka hii kazi tumeifanya kikamilifu subiri siku ya kupiga kura amna atakaye amini wingi wa kura atakazo pata lowassa
 
Oooooooh! asante kwa faraja
Mimi ni ccm damu damu lakini nikilinganisha wagombea na sera zao hizi za LOWASSA zinanipa ahuweni ya maisha
 
Ni kweli vijijini hapakukaa vizuri sana. Haya Magamba yanatumia umaskini wao na shule ndogo (uelewa) kuwapa vitisho, zawadi ndogo ndogo, fiesta nk
 
Tumeanza rasmi na hatuachi nafasi hata kidogo.Kule Nzega Lowassa anasaidiwa na MBUNGE WA sisiem kupata kura vijijini.
 
Sjui ni Lowassa anajua siasa au ana watu wanajua siasa

Juzi nikiwa na safari za kikazi nimepita eneo ndani kijijini nikakuta watu Wanaitwa "Team Lowassa" au "4UMovement" huko

Nilizungumza na mmoja akanishangaza kuwa movement yao ina watu karibu zaidi ya 5000 na wameshaganwanyika maeneo tofauti

Nikajaribu kuwaza nguvu hii M4C wangeweza kupambana nayo kama Lowassa angekuwa CCM??

Hakika huu ni uchaguzi wa aina yake
 
Back
Top Bottom