( Ukawa ) msafara wa Mamba na Kenge ni hawa....

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Jul 29, 2013
10,522
24,010
chizi nimerogwa tena. ngoja niseme.

Kumekuwa na kamata kamata nyingi sana hasa kipindi cha chaguzi mbalimbali zinazohusiana na chaguzi za manispaa na pengine hata kwenye Umeya kwa maeneo yenye mwelekeo hasi kwa ccm.
tumeona morogoro na pia sehemu nyingine ambazo kwa chama tawala wamekuwa na wakati mgumu wa kuibuka na ushindi. jambo moja lazima tukubali kuwa kwa nchi zetu za afrika vyombo vya dola si huru hata kidogo. ukiacha hilo pia vimekuwa kama vipo kwa ajili ya kulinda maslah ya chama tawala. mifano ipo mingi ukiangalia kwa uchaguzi wa Uganda hapa juzi juzi lakini pia ilivyokuwa Zimbabwe, Tanzania etc

Kipindi hiki ambacho Ukawa wana nia ya kukamata Majiji kadhaa ni kipindi ambacho walipaswa kuwa makini sana. ningesema wangeitwa madiwani na wabunge wote kufanyiwa counseling ili kuepuka kutenda au kunena mambo ambayo yanaweza leta shida na hatimaye kukamatwa siku au masaa machache kabla ya kupiga kura ya uchaguzi flan. tumeona ili ccm washinde sehemu nyingine ilibidi watu wa ukawa wakamatwe na wawekwe ndani hivyo kusababisha uchaguzi ufanyike wakipa pungufu. ni sawa na kucheza mpira na team ambayo imemnunua refa. hivyo ninyi mnapaswa muwe waangalifu maana mnaweza jikuta wachezaji wenu wnapewa kadi nyekundu nyingi tu ili wabaki wachache au waliopo wakatishwe tamaa na mchezo na hivyo kufungwa.

lakini pia naTOA ANGALIZO HAPA. kuna watu ambao wanaweza kabisa kuwa wanapokea rushwa na kufanya rafu ambazo zitasababisha watolewe nje ya uwanja na hivyo kuwafanya mcheze pungufu na mfungwe. angalieni watu wenu wanaofanya au sema mambo ambayo yanaweza sbabisha dk za mwisho kukamatwa na kuwekwa ndani ili uchaguzi upite then kesi zao baadaye zikose mashiko. hawa wanaweza kuwa wamepokea mlungula na namna ya kuwafanya wasionekane wana makosa ni kukamatwa na hatimaye wao kuonekana walionewa n.k tutegemee kuwa kuna chaguzi zitafanyika siku ambayo wapiga kura wengine jioni yake watakamatwa na kuwekwa ndani.

UKAWA HUO MLIO NAO NI MSAFARA WA MAMBA KENGE NAO WAMO nyuma nyuma. msidhani wote ni Mamba. lakini pia ni wajibu wenu wa kuwaweka watu wenu chini waache utoto na fujo zisizo na msingi. Maana, MICHEZO YENU, MAUTI YETU.

Kutoka Milembe Hospital
Kichaa karogwa tena.
 
Back
Top Bottom