UKAWA mbona hatupiganii Katiba ya WANANCHI?

Gangongine

JF-Expert Member
Dec 31, 2015
3,854
1,776
Nakumbuka vema kilichotuunganisha mpaka tuigize kususia Bunge la Katiba ni kuwatetea Wananchi ili Maoni yao yazingatiwe kwenye Katiba Inayopendekezwa. Aidha, wakati wa Uchaguzi tuliwadanganya tena Wananchi kwamba wakituchagua tutapigania Katiba ya Wananchi na kweli tukapata Kura milioni 6. Hata hivyo baada ya Uchaguzi tumesahau kabisa Ajenda hii na wala hatuizungumzii tena kwa kisingizio cha kushindwa Uchaguzi Mkuu 2015. Tumesahau tulianza Ajenda hii kabla ya Uchaguzi Mkuu na tulipaswa kuipigania hata baada ya kushindwa Uchaguzi. Wananchi wenye akili wamatuelewa vizuri kwamba kumbe Ajenda ya Katiba Mpya ilikuwa ujanja wetu wa kushinda Uchaguzi na hatukuwa tunamaanisha toka mioyoni mwetu!!

Ajabu Mgombea wetu alisema kipaumbele kwenye Ilani ya Ukawa ni ELIMU, ELIMU, ELIMU (ELIMUx3) lakini sidhani kama Ilani yetu ilitamka hivyo???? Hapo ndipo usanii wetu ulipobainika mbele ya wenye akili tukapoteza Uchaguzi Mkuu. Kama kweli tuna nia hiyo basi tuoneshe sasa vinginevyo tumewasaliti wananchi na hatuwezi kuaminika tena! MABADILIKOOOOOOOO!
 
Wewe ni mnafiki mkubwa, habari iliyipo ni uchaguzi wa mameya Na kule zenji, tunahitaji majibu nasiyo bla blaa km hizi, elimu, elimu, elimu inakuhusu gamba wewe
 
Unataka tupiganie vip au tushike bunduki ndio ujue tunapigania ??
 
mbona unatupangia njia ya kutumia ?
haya hatutaki njia hiyo
Siku kila jimbo kila chama cha upinzani kikirudi na mfumo wa zamani wa kila chama kuingiza mgombea wake ndio itakua mwisho wa CDM nchini,
Licha ya kusimama mbunge mmojammoja ushindi ulikua ni mwembamba mno kwa wabunge wa UKAWA.
 
Siku kila jimbo kila chama cha upinzani kikirudi na mfumo wa zamani wa kila chama kuingiza mgombea wake ndio itakua mwisho wa CDM nchini,
Licha ya kusimama mbunge mmojammoja ushindi ulikua ni mwembamba mno kwa wabunge wa UKAWA.
WASUBIRI KIPIGO CHA MBWA MWIZI 2019 UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA
 
Back
Top Bottom