UKAWA jiandaeni kisaikolojia 2015

UKAWA jiandaeni kisaikolojia 2015

Kura zihesabiwe na wapiga kura wote kwa sauti baada ya kuzichambua na kila mwakilishi wa mgombea kushika zake.....teh teh
 
CCM kufanya hivyo ni kulazimisha ya Kenya yatokee hapa tena kwa nguvu kubwa zaidi. watu wameshachoka kuonewa.
 
Hata zikiwa tume huru kumi, wananchi hawajaona sera za UPINZANI, zaidi ya kukiponda chama tawala, hayo siyo mahitaji ya wananchi.
Kwa hiyo mahitaji ya wananchi ni escrow na sera zisizotekelezeka sio? Nikufahamishe. Simply wananchi wameichoka ccm na hawana haja tena ya kusikiliza lolote toka ccm. CCM ishakufa na kuoza, mtuondolee harufu!
 
Kwa hiyo mahitaji ya wananchi ni escrow na sera zisizotekelezeka sio? Nikufahamishe. Simply wananchi wameichoka ccm na hawana haja tena ya kusikiliza lolote toka ccm. CCM ishakufa na kuoza, mtuondolee harufu!

Takwimu hiyo mkuu umeitoa wapi kwamba wananchi wameichoka CCM? mbona mitaani tunakutana na watu wengi waliovaa kofia, fulana na kanga za CCM kwa hiari yao? Mbona mgombea wa CCM anapotangazwa mshindi wanaoshangilia kwa vifijo wapo? au hawa ni mataahira? Takwimu zako hizo nadhani sio sahihi, kilicho sahihi kwako zaidi ni kusema "mimi nimeichoka CCM" badala ya kusema "wananchi wameichoka CCM". Jiandikishe na uwende ukapige kura kwa usahihi siku ya uchaguzi ili kuonyesha demokrasia yako (wewe).
 
Hivi bado UKAWA wanaamini watachukua nchi 2015 hata baada ya uchaguzi wa s/mitaa? Litakuwa ajabu la 8 la Dunia
 
Mmeanza kujitekenya na kucheka wenyewe tafuteni pakutokea mtashindwa vibaya sana maana mko pamoja na shetani.
 
Hivi bado UKAWA wanaamini watachukua nchi 2015 hata baada ya uchaguzi wa s/mitaa? Litakuwa ajabu la 8 la Dunia
Ngoja wajifanye wamechanganyikiwa lakini moto watauona tu hatuchagui waliopagawa na maisha.
 
Mambo yanayotokea kwenye kutangaza na kuapisha washidi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni dalili mbaya ya kitakachotokea kwenye uchaguzi wa urais wa 2015 kama UKAWA watashinda 2015.

Ukawa itashindwa tu 2015 kama wasimamizi, wanaotangaza na wanaoapisha mshindi wataendelea kuteuliwa, kupokea na kutii maagizo na amri kutoka kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, wakuu wa mikoa na Rais wa nchi (hawako huru).

Kama utaratibu utaendelea kuwa kama ulivyo sasa wapinzani ni bora kuanza kujiandaa kushindwa tu tena 2015. Vinginevyo hamna budi kuanza leo kutafakari namna wasimamizi, watangazaji wa matokeo na waapishaji wa walioshinda watakavyokuwa huru uchaguzi wa 2015 kabla ya kufikiria majina ya wagombea na namna ya mtakavyoiendesha serikali ya UKAWA.

Au mfikirie mapema nini mtakachofanya kama atatangazwa na kuapishwa yule ambae hakushinda kama ilivyotokea kwa Mwai Kibaki na Odinga kule Kenya.
Kimbembe ni pale atakapotangazwa ambaye hakushinda na kuamriwa mwende kulalamikia mahakamani badala ya kupaza sauti zenu kwa aliyemtangaza makusudi aliyeshindwa.

Tutalinda kura
 
Back
Top Bottom