UKAWA jiandaeni kisaikolojia 2015

UKAWA jiandaeni kisaikolojia 2015

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
16,252
Reaction score
16,171
Mambo yanayotokea kwenye kutangaza na kuapisha washidi wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni dalili mbaya ya kitakachotokea kwenye uchaguzi wa urais wa 2015 kama UKAWA watashinda 2015.

Ukawa itashindwa tu 2015 kama wasimamizi, wanaotangaza na wanaoapisha mshindi wataendelea kuteuliwa, kupokea na kutii maagizo na amri kutoka kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa wilaya, wakuu wa mikoa na Rais wa nchi (hawako huru).

Kama utaratibu utaendelea kuwa kama ulivyo sasa wapinzani ni bora kuanza kujiandaa kushindwa tu tena 2015. Vinginevyo hamna budi kuanza leo kutafakari namna wasimamizi, watangazaji wa matokeo na waapishaji wa walioshinda watakavyokuwa huru uchaguzi wa 2015 kabla ya kufikiria majina ya wagombea na namna ya mtakavyoiendesha serikali ya UKAWA.

Au mfikirie mapema nini mtakachofanya kama atatangazwa na kuapishwa yule ambae hakushinda kama ilivyotokea kwa Mwai Kibaki na Odinga kule Kenya.
Kimbembe ni pale atakapotangazwa ambaye hakushinda na kuamriwa mwende kulalamikia mahakamani badala ya kupaza sauti zenu kwa aliyemtangaza makusudi aliyeshindwa.
 
Kweli ni muhimu kujiandaa. Maana manyinyiem haya hata aibu. Kushinda ashinde mwingine kutangazwa atangazwe mwengine.
 
Mambo yanayotokea kwenye kutangaza na kuapisha washidi Wa uchaguzi Wa serikali za mitaa ni dalili mbaya ya kitakachotokea kwenye uchaguzi Wa urais Wa 2015 Kama UKAWA watashinda 2015. Ukawa itashindwa tu 2015 Kama wasimamizi, wanaotangaza na kuapisha mshindi wataendelea kuteuliwa na kupokea na kutii maagizo na amri kutoka kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi Wa wilaya, wakuu wa mikoa na Rais Wa nchi. Kama utaratibu utaendelea kuwa Kama ulivyo Sasa wapinzani ni bora kuanza kujiandaa kushindwa tu Tena 2015. Vinginevyo hamna budi kuanza Leo kutafakari namna wasimami, watangazaji Wa matokeo na waapishaji Wa walioshinda watakavyokuwa huru uchaguzi Wa 2015. Au muwe na cha kufanya Kama atatangazwa na kuapishwa yule ambae hakushinda Kama ilivyotokea kwa Mwai Kibaki kule Kenya.
.....hakika kabisa.
 
Bila Tume huru ya uchaguzi itakuwa kujisumbua tu kufanya uchaguzi kwani mshindi atakuwa anajulikana hata kabla! UKAWA msikubali kuingia katika uchaguzi bila Tume huru kwanza!
 
Walikuwa na ndoto ya ushindi wakati sm wamegaragazwa. Kweli wajiandae tu kisaikolojia.
 
Kweli ni muhimu kujiandaa. Maana manyinyiem haya hata aibu. Kushinda ashinde mwingine kutangazwa atangazwe mwengine.
Watu wa ajabu kabisa nyie Chadema UKAWA. ndiyo gia mnayokwenda nayo kwa wananchi. Kwa mtindo huu CCM itaendelea kuwaburuza tu kwenye chaguzi mbalimbali
 
Bila Tume huru ya uchaguzi itakuwa kujisumbua tu kufanya uchaguzi kwani mshindi atakuwa anajulikana hata kabla! UKAWA msikubali kuingia katika uchaguzi bila Tume huru kwanza!
Hata zikiwa tume huru kumi, wananchi hawajaona sera za UPINZANI, zaidi ya kukiponda chama tawala, hayo siyo mahitaji ya wananchi.
 
Bila Tume huru ya uchaguzi itakuwa kujisumbua tu kufanya uchaguzi kwani mshindi atakuwa anajulikana hata kabla! UKAWA msikubali kuingia katika uchaguzi bila Tume huru kwanza!

Nakuunga mkono. Hivi inawezekana vipi mbele ya hadhara mtu bila chembe cha aibu akaweza kusimama na kumtangaza mtu ambaye hajashinda kuwa kashinda na watu wakaangalia na kunyamaza? Jamani, tunakoeleka si kuzuri hata kidogo.
 
Back
Top Bottom