UKAWA hapa nimewakubali

UKAWA hapa nimewakubali

UKAWA UKAWA

Member
Joined
Sep 24, 2014
Posts
53
Reaction score
15
UKAWA wabuni mbinu mpya ya urais 2015

KIKAO cha pamoja
kilichowakutanisha viongozi
wa Umoja wa Katiba ya
Wananchi (Ukawa), kimetoa
mikakati ya pamoja
ikiwamo kuandaa ratiba ya
uteuzi wa wagombea wa
nafasi ya urais kwa kila
chama.
Hatua hiyo imekuja baada
ya kikao cha siri cha siku
mbili kilichowakutanisha
viongozi wa juu wa Ukawa
ambao ni Mwenyekiti wa
CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba, Freeman Mbowe
(Chadema), James Mbatia
(NCCR-Mageuzi) na Dk.
Emmanuel Makaidi (NLD).
Chanzo cha kuaminika
kiliambia MTANZANIA jana
kuwa katika kikao hicho,
viongozi hao
wamekubaliana kuweka
mikakati hiyo ikiwamo ya
kushika dola katika
Uchaguzi Mkuu
unaotarajiwa kufanyika
Oktoba, mwaka huu.
Katika kikao hicho, viongozi
hao wametoa ratiba
ambayo inakitaka kila
chama kuteua mgombea
wake wa urais ili ajulikane
mapema kabla vikao vya
Ukawa kuteua jina la
mgombea mmoja.
“Imewekwa mikakati hii
kwa lengo la kuimarisha
demokrasia kwa kila chama
husika, hasa vinavyounda
Ukawa vipate muda wa
kutosha wa kuweza
kufanya uteuzi mapema.
“Lakini pia sasa ni wakati
kwa wale wazalendo wa
kweli, hasa kutoka upande
wa Chama Cha Mapinduzi
(CCM), ambao wana
uchungu na nchi yao
wajitoe mapema na kuja
kushiriki uchaguzi kupitia
Ukawa badala ya kusubiri
hadi mwisho, kwani
wakifanya hivyo wanaweza
wakakuta milango
imefungwa.
“Hili linaweza kuwafanya
washindwe kupata nafasi
sasa, maana ni wazi Ukawa
ndiyo tegemeo la
Watanzania wengi kwa sasa
ambao wapo tayari
kukabidhi dola katika
uchaguzi ujao,” kilisema
chanzo hicho.
Mbali na kuweka mkakati
hiyo, viongozi hao wa
Ukawa wameandaa kanuni
za uchaguzi ambazo kila
chama kinatakiwa
kuwasilisha katika vikao
vyake vya uamuzi na
kuweza kujadili kama njia
ya kushika dola.
Mikakati hiyo ya Ukawa
inatarajiwa kuwekwa wazi
leo ambapo wenyeviti wote
wanatarajiwa kuzungumza
na waandishi wa habari.
Katika kinachoelezwa
kutekeleza mikakati ya
Ukawa, tayari Kamati Kuu
ya Chadema, imekutana
jijini Dar es Salaam
ambapo ilijadili hali ya
kisiasa nchini, Katiba
inayopendekezwa na
kanuni za uchaguzi za
Ukawa kama njia ya
kuelekea kuteua mgombea
mmoja wa urais katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba.
Pamoja na kuratibiwa kwa
vikao vya Ukawa vya
kupata mgombea mmoja
wa urais, kwa upande wa
CUF, wamekuwa
wakipigana kufa na kupona
kuhakikisha, Profesa
Lipumba anakuwa
mgombea wa urais kupitia
umoja huo.
Nao Chadema wamekuwa
wakiendesha harakati za
kile kinachoelezwa
kuhitajiwa na Watanzania
kwa Dk. Willibrod Slaa
kuwa mgombea urais kwa
kigezo kwamba ana mvuto
na kipenzi cha watu wengi
hali iliyomfanya ashike
nafasi ya pili katika
Uchaguzi Mkuu uliopita.
Hata hivyo, katika harakati
hizo tayari Mwenyekiti wa
NCCR Mageuzi, Mbatia
amekuwa katika harakati
za kugombea ubunge
katika Jimbo la Vunjo, huku
Dk. Makaidi naye
akitarajiwa kufanya hivyo.
Ikiwa Mbatia na Dk.
Makaidi wataendelea na
misimamo yao ya kuwania
ubunge kinyang’anyiro cha
kuwania urais kupitia
Ukawa kitakuwa kwa
Profesa Lipumba na Dk.
Slaa.
Ushirikiano wa vyama
hivyo ulianza katika Bunge
Maalumu la Katiba na
kuendelea hadi Bunge la
Jamhuri ambapo vyama
washirika viliingizwa
kwenye baraza kivuli
ambalo lilikuwa likiongozwa
na Chadema peke yake.
Vyama hivyo vimepata
msisimko zaidi katika
umoja wao baada ya
kufanikiwa kushinda viti
vingi katika Uchaguzi wa
Serikali za Mitaa.

Chanzo:Mtanzania
 
ukawa wabuni mbinu mpya ya urais 2015

kikao cha pamoja
kilichowakutanisha viongozi
wa umoja wa katiba ya
wananchi (ukawa), kimetoa
mikakati ya pamoja
ikiwamo kuandaa ratiba ya
uteuzi wa wagombea wa
nafasi ya urais kwa kila
chama.
Hatua hiyo imekuja baada
ya kikao cha siri cha siku
mbili kilichowakutanisha
viongozi wa juu wa ukawa
ambao ni mwenyekiti wa
cuf, profesa ibrahim
lipumba, freeman mbowe
(chadema), james mbatia
(nccr-mageuzi) na dk.
Emmanuel makaidi (nld).
Chanzo cha kuaminika
kiliambia mtanzania jana
kuwa katika kikao hicho,
viongozi hao
wamekubaliana kuweka
mikakati hiyo ikiwamo ya
kushika dola katika
uchaguzi mkuu
unaotarajiwa kufanyika
oktoba, mwaka huu.
Katika kikao hicho, viongozi
hao wametoa ratiba
ambayo inakitaka kila
chama kuteua mgombea
wake wa urais ili ajulikane
mapema kabla vikao vya
ukawa kuteua jina la
mgombea mmoja.
“imewekwa mikakati hii
kwa lengo la kuimarisha
demokrasia kwa kila chama
husika, hasa vinavyounda
ukawa vipate muda wa
kutosha wa kuweza
kufanya uteuzi mapema.
“lakini pia sasa ni wakati
kwa wale wazalendo wa
kweli, hasa kutoka upande
wa chama cha mapinduzi
(ccm), ambao wana
uchungu na nchi yao
wajitoe mapema na kuja
kushiriki uchaguzi kupitia
ukawa badala ya kusubiri
hadi mwisho, kwani
wakifanya hivyo wanaweza
wakakuta milango
imefungwa.
“hili linaweza kuwafanya
washindwe kupata nafasi
sasa, maana ni wazi ukawa
ndiyo tegemeo la
watanzania wengi kwa sasa
ambao wapo tayari
kukabidhi dola katika
uchaguzi ujao,” kilisema
chanzo hicho.
Mbali na kuweka mkakati
hiyo, viongozi hao wa
ukawa wameandaa kanuni
za uchaguzi ambazo kila
chama kinatakiwa
kuwasilisha katika vikao
vyake vya uamuzi na
kuweza kujadili kama njia
ya kushika dola.
Mikakati hiyo ya ukawa
inatarajiwa kuwekwa wazi
leo ambapo wenyeviti wote
wanatarajiwa kuzungumza
na waandishi wa habari.
Katika kinachoelezwa
kutekeleza mikakati ya
ukawa, tayari kamati kuu
ya chadema, imekutana
jijini dar es salaam
ambapo ilijadili hali ya
kisiasa nchini, katiba
inayopendekezwa na
kanuni za uchaguzi za
ukawa kama njia ya
kuelekea kuteua mgombea
mmoja wa urais katika
uchaguzi mkuu wa oktoba.
Pamoja na kuratibiwa kwa
vikao vya ukawa vya
kupata mgombea mmoja
wa urais, kwa upande wa
cuf, wamekuwa
wakipigana kufa na kupona
kuhakikisha, profesa
lipumba anakuwa
mgombea wa urais kupitia
umoja huo.
Nao chadema wamekuwa
wakiendesha harakati za
kile kinachoelezwa
kuhitajiwa na watanzania
kwa dk. Willibrod slaa
kuwa mgombea urais kwa
kigezo kwamba ana mvuto
na kipenzi cha watu wengi
hali iliyomfanya ashike
nafasi ya pili katika
uchaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo, katika harakati
hizo tayari mwenyekiti wa
nccr mageuzi, mbatia
amekuwa katika harakati
za kugombea ubunge
katika jimbo la vunjo, huku
dk. Makaidi naye
akitarajiwa kufanya hivyo.
Ikiwa mbatia na dk.
Makaidi wataendelea na
misimamo yao ya kuwania
ubunge kinyang’anyiro cha
kuwania urais kupitia
ukawa kitakuwa kwa
profesa lipumba na dk.
Slaa.
Ushirikiano wa vyama
hivyo ulianza katika bunge
maalumu la katiba na
kuendelea hadi bunge la
jamhuri ambapo vyama
washirika viliingizwa
kwenye baraza kivuli
ambalo lilikuwa likiongozwa
na chadema peke yake.
Vyama hivyo vimepata
msisimko zaidi katika
umoja wao baada ya
kufanikiwa kushinda viti
vingi katika uchaguzi wa
serikali za mitaa.

Chanzo:mtanzania
kitaeleweka tu
 
UKAWA wanapiga kimya kimya - ndiyo habari ya mjini kwa sasa.
 
mgombea wa UKAWA ni vita kati ya Wakristo na Waislamu

Pia usisahau Kusema kuwa Ugombea Urais ndani ya CCM ni Ukiristo v/s Uislam; Pia Utanganyika V/s Uzanzibar: Na kwa taarifa yako Safari hii ndani ya CCM kwa Urais wa URT ni zamu ya Zanzibar.
 
UKAWA hatuwezi kushiriki uchafu uliofanywa na wabunge wa ccm kutengeneza katiba ya ccm ambayo imeandikwa na fisadi mkubwa Andrew chenge mzee wa vijisenti
 
mwaka huu ndiyo mtajua chama cha udini na ukabila ni kipi ndani ya UKAWA
tunakupuuzia kama ulivyo mpuuzi ukabila na udini tunajua ndo sera ya ccm tumesikia hata yule mwanasheria wenu anataka kujengewa msikiti karibu na ofisi kwake.
 
Back
Top Bottom