UKAWA NA MAMBO YAO
Wanamabadiliko jiandaeni kifikra kwa sababu hali ndani ya UKAWA sio nzuri hata kidogo na naweza kusema tumeshapoteza dira kabisa. Kuna mambo mawili makubwa yanayoleta mtafaruku: Hela na Mitandao.
Nianze na hili la fedha
Moja ya mambo yaliyoahidiwa na Mzee Lowassa wakati anajiunga na CHADEMA mwezi Julai, ilikuwa kutoa mchango wa fedha za kuendhesha kampeni.
Kwa muda mrefu CHADEMA haikuwa na hali nzuri kifedha.
Chama kilikuwa kinadaiwa fedha nyingi kutoka kwa Mzee Mtei na Mzee Ndesamburo, watu ambao kwa kweli wamekuwa kimbilio kwa muda mrefu. Mtu mwingine ambaye amekuwa anadai CHADEMA, japo wakati mwingine haileweki alikopesha lini Chama ni Freeman Mbowe mwenyewe.
Baada ya majadiliano, Lowassa alikubali kutoa kiasi cha Shilingi bilioni 19 kwa makubaliano kuwa shilingi bilioni 4 kati ya hizo zingetumika kulipa madeni pamoja na kukisadia shughuli za kiofisi za Chama, na shilingi bilioni 15 zitakazobakia zielekezwe kwenye kusaidia wagombea Ubunge kupitia vyama vinavyounda UKAWA.
Ilikubalika kila mgombea kiti cha ubunge kupita UKAWA apate kati ya shilingi milioni 2 hadi 5 kulingana na uimara/kukubalika kwa mgombea katika eneo husika.
Nini kimetokea?
Tofauti na makubaliano yaliyokwishafikiwa, Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA alichukua hela yote ya UKAWA (takriban bilioni 15) na kuitumia kwa ajili ya wagombea wa CHADEMA tu! Na kama hiyo haitoshi, hata ndani ya CHADEMA ni wagombea wachache (watu wake) ambao wamepata msaada kutokana na hizi hela za Lowassa.
Wagombea ubunge, udiwani wa vyama vingine vinavyounda UKAWA yaani CUF, NCCR-Mageuzi pamoja na mgombea mwenza wa kiti wa urais Mzee Duni wametelekezwa! Watu kama Mbatia, Maalim Seif na Makaidi wamepata hela zao moja kwa moja toka kwa Lowassa kwa utaratibu tofauti (nitaeleza hapo mbeleni) lakini wabunge wao walitakiwa kupata fungu toka hilo alilochukuwa Mbowe.
Baada ya kumaliza awamu ya kwanza ya mabilioni ya Lowassa, Mbowe bila huruma wala aibu, akarudi tena kwa Mzee kuomba fedha nyingine, ambapo alifanikiwa kupata shilingi bilioni moja. Hizi nazo zimeyeyuka kama barafu na Mbowe akiulizwa anakuwa mkali!
Kutokana na mambo yanayokwenda ndani ya UKAWA na hasa CHADEMA pamoja na kuzorota kwa afya ya Mzee Lowassa, familia ya Mzee Lowassa imeingilia kati kwa hofu kuwa watu wanamtumia kama ATM. Hatua waliyochukuwa ni kwamba Mzee Lowassa hawezi kuidhinisha fedha (money withdrawals) bila sahihi za watoto wake (signatories).
Nisingependa sana kujadili afya ya Mzee Lowassa kwa sababu hili ni jambo binafsi ila naomba itoshe nikisema kuwa Mzee wetu anapoteza kumbukumbu kwa haraka sana.
Fedha toka Ujerumani
CHADEMA waliomba msaada wa fedha kutoka kwa wafadhili wao walioko Ujerumani kwa ajili ya shughuli za uchaguzi. Kiasi cha shilingi 15 zilizotumwa na wafadhali hao toka Ujerumani hazionekani na kama kawaida Mbowe hataki kuulizwa chochote!
Imefikia muda watu wanaanza kususa. Kwa sasa juhudi zinafanyika kuokoa jahazi maana Mzee Duni ‘kachoka'. Kwenye kikao cha dharura kilichoitishwa baada ya mkutano wa Tanga, Mbowe alikataa kuhudhuria. Mzee Mtei kuona mambo yako hovyo akaamua kuhudhuria mwenyewe.
Mbatia na hela za wafanyabiashara wa Arusha
Kuanzia awali, James Mbatia, Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi alikuwa na kigugumizi kuhusu afya ya Mzee Lowassa. Baada ya kumkaribisha Mzee, Mbatia hapo hapo alianza mchakato wa pembeni kumpata ‘replacement' na ndipo alipomfuata Sumaye. Mwanzo, Sumaye alisita kwa maelezo kuwa ‘pensheni' itakuwaje?.
Mbatia kusikia hivyo, aliwasiliana na wafanyabiashara wa Arusha ambao walikuwa wanamuunga mkono kwenye huo mchakato wa kumpata Sumaye na wakaahidi kuwa watachakuwa jukumu la kulipa maslahi ya Mzee, hivyo aende UKAWA. Wafanyabiashara hao pia walichanga kiasi cha dola milioni 5 kwa ajili ya kusaidia kampeni. Katika hali ya kushangaza hela hizi, dola milioni 5 zilihifadhiwa chumbani kwenye hoteli moja ya jijini Arusha. (dola milioni tano, ambazo ni zaidi ya shilingi bilioni 10 za Kitanzania zinawekwa chumbani!!!)
Siku chache baadae, wakiwa kwenye kampeni mwishoni mwa mwezi Agosti, wakubwa walipigiwa simu ikiwataarifu kuwa hela zilizokuwa chumbani kwenye hoteli ya Arusha zimeibiwa! Zoooote! Siku tatu baada ya tukio hili la ‘wizi' zilikuja taarifa tofauti kuwa hela hazijaibiwa bali zilichukuliwa kwa maelezo ya Mbatia! Kama ilivyo kwa Mbowe, Mbatia naye amekuwa mbogo, yuko busy na matanuzi. Mbatia kanunua gari la kifahari, brand new (vijana wa mjini wanasema zero mile), mwezi huo huo wa nane. Wakati wagombea wabunge na madiwani wake wanatumia kinuua mgongo kuendesha kampeni zao Mbatia ananunua magari ya kifahari, na amelipa CASHA dola 88,000.
ANGALIENI RISITI.
Madai ya Mbatia kuwa CCM wanataka kumuua ni kukwepa hoja. Ukweli ni kuwa baadhi ya wafanyabiashara waliochanga hela wanataka ‘shingo' yake.
Sumaye na urais
Sumaye ilikuwa ajiunge na NCCR-Mageuzi, na mpango wa Mbatia na wafanyabiashara wake ilikuwa ‘ukifika' wakati wa kum-replace Lowassa basi mgombea atoke NCCR-mageuzi.
Kuna taarifa ambazo hazijathibitishwa zinazohusu mzozo wa kibiashara kati ya Mbowe na baadhi ya watu walio nyuma ya Mbatia na ndio sababu walitaka Sumaye asipitie mikononi mwa Mbowe. Hata hivyo, haikuwezekana maana jina lililopekwa TUME ni la mgombea toka CHADEMA. Kwa sasa Sumaye kabaki anaelea, hajulikani ni wa chama gani?
Siasa za mtandao
Hadi mwishoni mwa Mwezi Julai mtu angeniuliza Lowassa ni nani, ningemjibu, Lowassa ni mwanasiasa wa Tanzania. Lakini ndani ya muda mfupi baada ya kujiunga na CHADEMA/UKAWA nimegundua kuwa Lowassa ni zaidi ya mtu mmoja!. Lowassa ni TAASISI inayojitegemea na yenye malengo yake ambayo hayafanani kabisa na CHADEMA.
Taasisi hii ilishapanga safu yote ya uongozi kuanzia mawiziri, gavana wa benki kuu, wakuu wa Mikoa na Wilaya hadi Wakurugenzi wa mashirika. Ni vituko! Itakuwa vigumu sana kupangua safu iliyowekwa kwa miaka mingi. Kwa kifupi, taasis ya Lowassa haihitaji chochote toka CHADEMA au UKAWA zaidi ya tiketi ya kugombea urais, na ndio maana hata kwenye kampeni muda mwingi Mzee yuko na ‘watu' wake.
Moja ya mbinu iliyotumiwa ni hii taasis ni kuisambaratisha UKAWA bila wao kujua. Ni hivi, Lowassa ameingia makubaliano na UKAWA yaani vyama vyote vinne kwa pamoja. Lakini pia Lowassa ameingia makubaliano mengine ya pembeni na viongozi ‘mmoja mmoja' kwa Chama husika.
Matakeo yake, uongozi wa UKAWA umejikuta hauna nguvu tena juu ya jambo lolote linalotendeka ndani ya umoja huu. Kwa sasa mwenyekiti Mbowe hana nguvu mbele ya Mbatia, au Maalim Seif kwani kila mmoja ana makubaliano na ‘mfadhili' mkuu. Mwenye maamuzi ya mwisho ni taasis ya Lowassa. Na ndio sababu hakuna cha maana kinachofanywa na Bavicha wala mama yake Bavicha.
Ngoyai na Kagame
Tetesi za Kagame kum-support Lowassa ni za kweli. Akiwa Bukoba (tarehe 19 Septemba) Lowassa alikutana kwa siri na ujumbe wa Rais Paul Kagame wa Rwanda ambapo pamoja na mambo alikabidhiwa kitita cha fedha.
Wajumbe kadhaa toka CHADEMA walionesha wasiwasi wao kuhusu mkutano huo na ujumbe wa Kagame lakini kutokana na ukweli kuwa hawana tena nguvu hawakufanikiwa kuuzima.
Tahadhari
Kuna wagombea wengi wa ubunge na udiwani wameambiwa watumie hela zao kuendesha kampeni kwenye maeneo yao kwa ‘maelezo' kuwa watarudishiwa baada ya uchaguzi kuisha! Naomba waachane na hiyo ahadi hewa! Hakuna hela yoyote mtakayopata baada ya uchaguzi. Wengine wanatumia hata hela za kiinua mgongo, mtafilisika!
Vichwa vya habari kwenye magazeti na bashasha kwenye mikutano ya UKAWA isiwapumbaze watu. Hali ndani ya UKAWA vuluvulu. Sijui Mbowe na Mbatia wana akili gani maana hakuna mtu anatoa mwongozi juu ya nini kifanyike! Watu wanapigana vikumbo kila mmoja anatafuta mshiko siku ipite. Sijui tumefikaje hapa?
Na nyie CUF Tanzania bara, jipangeni upya maana chama chenu ndio kimezama kimoja. Maalim Seif hana habari kabisa na wala haelekei kutaka kujua hali ya CUF bara. Kesha lamba bilioni zake kwa ajili ya uchaguzi Zanzibar, huku bara kimya! Chama kinakufa.