Ukatili: Mtoto wa mwaka mmoja auawa kwa kunyongwa na baba yake wa kambo

Dotto Mnzava

R I P
Mar 6, 2014
865
427
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa Kijiji cha Kindo katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, amekufa baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati yake na mkewe.

Taarifa ya Jeshi la polisi mkoani humo, inasema imemtaja, Abdalla Hamis, kuwa ndiye aliyenyongwa na baba yake wa kambo, Zamili Shabani (27), muda mfupi baada ya mama wa mtoto kwenda dukani kununua mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto na ndipo alipogundua kuwa mtoto amekufa.

Baada ya hali hiyo muhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbilia mafichoni na kwamba mama wa mtoto huyo
alipiga kelele ya kuomba msaada kwa majirani hadi alipokamatwa.


CHANZO: ITV
 
Back
Top Bottom